Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014: Matokeo kutoka nchi nzima (TZ Bara)

Nyamagana MBUGANI chadema imeshinda, MIRONGO cuf, MWEMBENI chadema..kiujumla CDM wameshinda maeneo mengi sana.. Aidha kuna mgombea wa ccm sweya malimbe amefariki mchana kwa presha. Taarifa zisizo rasmi Bugarika kuna mauaji ya mgombea Msaliti.. Pasiansi ililazimu Polisi waingilie kati maana wananchi walitaka kutumia silaha baada ya kushuku uchakachuaji matokeo.. Kifupi usiku huu mwz town ni shangwe kila kona people's power..

asante mkuu
 
Kitendo cha UKAWA kupata viti vya uwenyekiti na ujumbe karibu kila kata nchini... Ni ishara ya kuwa watanzania wa nchi hii wameamua kurudisha nchi mikononi mwao.

NOW you are talking. Hayo ndiyo maoni sahihi hata kama ungekuwa sio shabiki wa mabadiliko
 
Labda kitongojini kwako. Sehemu nyingi chadema wamechukua. Kilakala chadema, bigwa chadema Bong`ola chadema ccm imeshinda wapi?

kAMANDA ESTHER TAWETE.ambaye ni Katibu wa wilaya morogoro mjini na mwenyekiti wa kata ya kihonda,kafanya Kazi kubwa sana kwenye kata ya kihonda maana kutoka 0 mpaka mitaa 4 katika mitaa 10 ya kata ya kihonda. chadema imeshinda mitaa ya Kilombero kamanda Mchumila,Kilimanjapo Kamanda Godfrey,Msimamo kamanda Damian Nguzo,mtaa wa Yespa jina la kamanda nimelisahau, Na kwa Wilaya Uongozi Mpya Chini ya mwenyekiti kamanda James na Esther Tawete Umefanya kazi kubwa sana kutoka kiti 1 mpaka viti 30 na bado matokeo ya sua na baadhi ya mitaa.kwa Wilaya ya morogoro ilivyokuwa nyuma kimwamko wa upinzani ni Ushindi mkubwa sana.Kirakala 6,Bingwa 4,Magorofani 3,Lukobe 3,Tungi 2,Mazimbu 2,mlimani 1,mji mpya 1,Chamwino 2,Kihonda 4.
 
Ajabu ni kwamba Wenzetu walikuwa wengi Sana kulinda kura wakati sisi hatukuzidi 10 mpaka matokeo yanatangazwa

hili ndilo limekuwa likuumaliza upinzania mara nyingi kwa kutolinda kura. wamejifunza kwa makosa kuwa kupiga kura ni jambo moja na kulinda jingine. nadhani 2015 ulinzi wa kura za upinzani utakuwa mkali zaidi, muhimu mjikitike kutekelezan ahadi lakini kuiba kura itakuwa ngumu sana.
 
Kama tutalinganisha takwim za sehemu kura zzilikopigwa itakuwa cdm60%ccm40% ila ukijumlisha mapingamizi ccm 67% ukawa33% fuatilia

Katika hiyo 67 % ya CCM ni asilimia ngapi ni viti vilivyo patikana kwa mapingamizi.? Usishangaeni aasilimia zaidi ya sabini
 
Kwa Mara ya kwanza mtaa wangu utaongozwa na CHADEMA Maana CDM kura 700 CCM 260 na wajumbe wote wamekwenda CDM tumejaribu kuokoa chama tumeshindwa kwa Mara ya kwanza nimeonja uchungu Wa kuzomewa na kura zetu za kubumba tunarudi Nazi tukawape mama ntilie wafungie chapati....

huu uchaguzi i'm sure CCM wametumia rafu nyingi,ingekuwa waruhusu democrasia leo ungeshangaa,CCM watapoteza/wamepoteza kura nyingi kutokana na uchaguzi huu kukutana na hasira za escrow,hawakuwaza kwamba escrow itawaharibia
 
CHADEMA morogoro mitaa ya Dark city, kule Rukobe, K ndege, etc CHADEMA tumeweza kuthibitisha kwamba mtu hawezi kuishi kwa tezidume pekee, bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha UKAWA.
PPPOZZZZZ.......

Hii post inaheshima sana.
 
Kwa Mara ya kwanza mtaa wangu utaongozwa na CHADEMA Maana CDM kura 700 CCM 260 na wajumbe wote wamekwenda CDM tumejaribu kuokoa chama tumeshindwa kwa Mara ya kwanza nimeonja uchungu Wa kuzomewa na kura zetu za kubumba tunarudi Nazi tukawape mama ntilie wafungie chapati....

Hahahaa haaaa
Umenichekesha.
Bora ww umejisemea ukweli
 
Wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza ACT tumeshinda kijiji kimoja kwa nafasi ya mwenyekiti wa kijiji,Kijiji cha Mayega Mwenyejiti ni wa ACT anaitwa Ali Kidosha.Wilaya ya Magu ACT tumesimamisha vijiji vinne tu na viwili uchaguzi umeahirishwa na tumeshindwa kijiji kimoja.
 
hili ndilo limekuwa likuumaliza upinzania mara nyingi kwa kutolinda kura. wamejifunza kwa makosa kuwa kupiga kura ni jambo moja na kulinda jingine. nadhani 2015 ulinzi wa kura za upinzani utakuwa mkali zaidi, muhimu mjikitike kutekelezan ahadi lakini kuiba kura itakuwa ngumu sana.

hivi kura italendwaje defender za polisi zikianza kupiga risasi hewani au mabomu ya machozi,upinzani bado wanakumbana sana na hali ngumu
 
hili ndilo limekuwa likuumaliza upinzania mara nyingi kwa kutolinda kura. wamejifunza kwa makosa kuwa kupiga kura ni jambo moja na kulinda jingine. nadhani 2015 ulinzi wa kura za upinzani utakuwa mkali zaidi, muhimu mjikitike kutekelezan ahadi lakini kuiba kura itakuwa ngumu sana.

Mkuu Wenzetu wamelalamika Sana ulinzi Wa CDM kuwa Mkali wakadiriki kuwaita polisi eti ni CDM huwezi amini tumefanya jaribio la kuingiza kura feki Mara 3 limeshindikana....
 
NIMEPENYEZEWA NA RAFIKI YANGU YUKO BUKOBA
Bukoba vijijini; vijiji 84,cuf 32 chadema 36 ccm16,
BUKOBA mjini mitaa 42 cuf 21 chadema 20 ccm1
 
uhalisia ni kuwa cdm ama vyama vingine vilianzishwa ili vikue na si kudumaa,unachokiona ilikua lazima waendelee kutanuka,pengine miaka 25 ijayo wakaweza kubalance level na ccm

kaa hivohivo najua mumeanza kujamba kabla hamjanya
 
Nyamagana MBUGANI chadema imeshinda, MIRONGO cuf, MWEMBENI chadema..kiujumla CDM wameshinda maeneo mengi sana.. Aidha kuna mgombea wa ccm sweya malimbe amefariki mchana kwa presha. Taarifa zisizo rasmi Bugarika kuna mauaji ya mgombea Msaliti.. Pasiansi ililazimu Polisi waingilie kati maana wananchi walitaka kutumia silaha baada ya kushuku uchakachuaji matokeo.. Kifupi usiku huu mwz town ni shangwe kila kona people's power..

aslant e mkuuu
 
Back
Top Bottom