Demokrasia ni mfumo unaokutawala, utake usitake.Mimi si muumini wa demokrasia halikadhalika Mimi si muumini wa udikteta.
Baada ya kujifanyia tathmin nikajigundua mimi ni muumini wa MAENDELEO na UZALENDO.
Kuna dhana potofu ya kwamba, wananchi ni majuha hawajui au hawajitambui.Haya yanayoendelea kwenye kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi, yamedhihirisha pasi na shaka kile tunachosema kila siku rais na chama chake hawakubaliki, bali hutisha watu ili waonekane wanakubalika. Haiwezekani useme unakubalika, siasa ufanye mwenyewe ww na chama chako, hujuma ufanyie wapinzani wako, kisha siku ya ukweli wa hiyo hadithi kuwa unakubalika watu hawatokei kupiga kura. Hii inathibitisha wananchi wana uelewa wa kupima mambo, na wanafahamu fika uhuru na demokrasia yao hauporwi kwa sababu ya uwepo wa vitu.
Tunaweza hata tukaacha kulitumia hilo neno "Demokrasia," badala yake tukaamua maksudi kuheshimu HAKI za watu kuchagua kwa uhuru na utashi wao wenyewe kuwachagua viongozi miongoni mwao wanaotaka wawaongoze.Basi katika nchi ya kidemokrasia Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa kinachofanyika ni uchaguzi na siyo uchafuzi, na mfumo ni wa demokrasia na siyo demoghasia na kuwa mwisho wa siku watawala hawageuki kuwa watuwala.
Mkuu na wewe umeshakata tamaa kiasi.hicho?? kama mti mbichi umekuwa hivyo sisi mti mkavu itakuwaje?Uchaguzi au Uchaguzwiii?
Sijawahi kuona Maana ya Uchaguzi kama kamati kuu pale dodoma watu 2000 tu wanaamua kura za watanzania 50,000,000 ?
Mbaya zaid mwaka 2026 Rais ajaye ataamuliwa na mtu mmoja tu Mwenye Vinasaba vya nchi jiran
Swali linalonitatiza ni moja. Tukishawanyima 'uwepo wetu,' na bado wakajitangaza washindi hata kwa kura 50 zilizopigwa na makada; kwa maana kwao lililo mhimu ni 'ushindi' wa aina yoyote.... ni kipi kitakachoonekana tumefaidika nacho sisi ambao hatukupiga kura kwa kugomea uovu wao?Ukisikia wanasisitiza kuhusu kujiandikisha, si kwamba wanahitaji ushiriki wako katika mchakato wa utawala, la hasha! hawahitaji kura yako kwasababu haiwezi kubadili kilichopangwa.
Wanahitaji uwepo wako ili kuhalalisha mchakato wa uchaguzi!
Kwa muda huo ambao tungekaa foleni huku tukionekana mazuzu na wapita njia, badala yake angalau tutafanikisha kazi moja au mbili zenye tija. Hata kama ni kulima bustani, inshalla ipo siku tutakula mboga za majani.Swali linalonitatiza ni moja. Tukishawanyima 'uwepo wetu,' na bado wakajitangaza washindi hata kwa kura 50 zilizopigwa na makada; kwa maana kwao lililo mhimu ni 'ushindi' wa aina yoyote.... ni kipi kitakachoonekana tumefaidika nacho sisi ambao hatukupiga kura kwa kugomea uovu wao?
Sijui kama tuna kundi tena linalojali 'heshima na kuheshimika'.
Mkuu, nimesoma mahala humu JF, kwamba kuna pendekezo la 'kuwasomba', nyote! Mtaadhibiwa!Kwa muda huo ambao tungekaa foleni huku tukionekana mazuzu na wapita njia, badala yake angalau tutafanikisha kazi moja au mbili zenye tija. Hata kama ni kulima bustani, inshalla ipo siku tutakula mboga za majani.
Inasemekana (sijui kama ni kweli); kwamba CCM inao wanachama hai zaidi ya milioni nane (8 milioni).Sasa kama rais mwenyewe ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala alishasema wazi kabisa na bila kificho kuwa hatarajii watu anaowateua na kuwalipa mshahara, kuwapa gari na nyumba halafu wanaposimamia uchaguzi wamtangaze mgombea wa upinzani kushinda, Hivi katika mazingira kama hayo ambapo matokeo "yatalazimishwa" kushinda mgombea wa CCM kwa hali yoyote ile, kuna haja gani ya mtu mwenye akili zake timamu kwenda kujiandikisha achilia mbali kupiga kura?????!!!!!
Magereza hazijajaa. Au watasotesha mahabusu na kubambikia makosa baada ya kukosa kifungu.Mkuu, nimesoma mahala humu JF, kwamba kuna pendekezo la 'kuwasomba', nyote! Mtaadhibiwa!
Watapiga kura CCM wenyeweUmeeleweka vema.
Kinachofanyika Tz ni uchafuzi siyo uchaguzi.
Na apendwe tu hadi kipindi chake cha pili.Kufanya hivyo sio tatizo, lakini yeye mwenyewe anapendwa?
Bandiko zuri kuhusu hali / mazingira ya demokrasia yasivyo huru na haki kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa.
Na muumini wa UNAFIKI pia.Mimi si muumini wa demokrasia halikadhalika Mimi si muumini wa udikteta.
Baada ya kujifanyia tathmin nikajigundua mimi ni muumini wa MAENDELEO na UZALENDO.
Kama vile haujui kinachoendelea nchin,Unafiki bana.Sidhani kama itakuwa shida sana kuunganisha kupungua kwa watu kujiandikisha kupiga kura na hali ya kisiasa nchini. Sasa, watu wanaweza kuandika kwa hisia lakini kuna haja ya kuwa na taarifa sahihi (facts). Ni makosa kudhania tu kuwa watu hawajiandikishi kwa kiwango kikubwa kwa sababu moja au nyingine. Ni muhimu kukusanya taarifa sahihi na za uhakika na hivyo kuwa na data za nini kinaendelea.
Huyu Jafo anajiamini nini?.Hivi TWAWEZA bado wapo?Bandiko zuri kuhusu hali / mazingira ya demokrasia yasivyo huru na haki kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa.
Hata waziri wa wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) iliyo chini ya Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya kusimamia, kuratibu na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, Mh. Jafo anaelezea jinsi hali isivyokuwa nzuri wananchi hawajiadikishi. Waziri Suleiman Jafo akisoma ripoti za awali kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya amebainisha mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha inaongoza kwa kuwa na idadi ndogo ya wananchi kujiandikisha. Lakini serikali na mamlaka zinazohusika wanajifanya hawajui sababu wananchi kutojitokeza kwa wingi kujiandikisha.
11 Oktoba 2019
Waziri wa TAMISEMI Mh. Jafo anatoa ripoti ya takwimu zinazoonesha muelekeo wa wananchi kususa uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania ambapo ktk siku anaongea na viongozi wa mikoa na wilaya ni asilimia 20 tu ya wananchi wenye sifa za kupiga kura ndiyo wamejiandikisha Tanzania (Tanganyika ) nzima.
Mhe lissu alisema, na pia mhe zitto kabwe kasema, watu wakishidwa kuchagua viongozi wanaowapenda kwa sanduku la kura basi watatumia njia zingine, maombi yangu ni hii taifa letu lisifike hapo, maana damu itawagika, maombi yangu ni huyu jiwe aondoke kwa amani hapo 2020, la si hivyo mungu amuondoe katika dunia hii kabla ya 2020, hatujasahau kina akwillina, azory, ben saa nane na wengine, mungu bariki tzHatari itakuja pale ambapo haki haipatikani katika sanduku la kura, Hivyo Watu wakaamua kutafuta Viongozi kwa njia mbadala,
Lissu amewahi kusema hakuna Kiongozi ambaye ametufudisha thamani ya Utu Kama huyu..
Uchaguzi wa Wabunge waliyounga juhudi ulishatoa picha.. Hata kupoteza Maisha kwa Mwanafunzi Akwilina hakukupewa uzito zaidi ya kunyanyasa Viongozi wa CDM,
Hivi sasa hakuna uchaguzi ni bora liende tu.