Uchaguzi ndani ya CHADEMA lini?

Uchaguzi ndani ya CHADEMA lini?

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
wana JF
mwanzoni mwa mwaka huu kulikuwa na tetesi kwamba uchaguzi wa ndani wa viongozi wa CHADEMA utafanyika kuanzia mwezi wa nne 2013, cha ajabu hivi sasa ni mwisho wa june lakini kimya na hakuna kinachoendelea.

Demokrasia iko wapi ndani ya CHADEMA??? kuna rafiki yangu nlikuwa naongea naye kuhusu hili akasema uchaguzi wa nini wakati viongozi wapo?? je hilo jibu ni sahihi kwamba mfumo wa kifalme umerudi Tanzania? Tumezoea kumsikia Augostino Lyatonga Mrema akiwa mwenyekiti wa TLP tangu ahamie chama hicho miaka zaidi ya 15, John cheyo wa UDP na Prof Lipumba ni mwenyekiti wa kudumu wa CUF.

Je hivi vyama ni wale wale??

Mleta mada naomba nikupe jibu sahihi.

Viongozi walioko madarakani walichaguliwa mwaka 2009 na kipindi chao kinaisha mwaka 2014 tena mwishoni. Sasa uchaguzi kufanyika mwaka huu wa 2013 ni uamuzi wa busara wa viongozi wetu kuwahisha uchaguzi kwa ili kutobananisha uchaguzi wa ndani ya chama na uchaguzi wa serikali ya mtaa.

Kwa hiyo, wadau badala ya kuwashambulia viongozi wetu wangekuwa wanatumia mashambulio hayo kuandika vitu vya ukweli na pongezi nyingi kwa viongozi kupunguza muda wao wa uongzi kwa mwaka mmoja kwa malahi ya chama. Huu ndio ukweli wa 100%. Sina hakika kama viongozi wa ccm wanaliweza hilo.
 
ni chama cha kifalme hakuna uchaguzi by the way hakuna mtu mwingine chadema mwenye uwezo wa uongozi .

Alitegemewa zito but naye ni kirusi ndani ya chadema.
 
matarajaio yenu ni kuona uchaguzi ukifanyika na wale viongozi wote wanaitoa jasho ccm hawachaguliwi, uchaguzi upo na muda utafika, chama hakiwahusu kelele lundo nyie watu mna matatizo sana eeeh !
 
Vyama vya upinzani tangu lini kuna uchaguzi? Ukisha shika ni unabaki mpaka chama kife.

ahhaaaa kumbe! ndo maana mzee cheyo anabaki kuwa mwenyekiti wa UDP, CHRISTOPHER MTIKILA kuendelea kuwa mwenyekiti wa DP, Mrema naye kung'ang'ania TLP, huku mzee lipumba naye amekuwa Mungu mtu wa CUF. ukienda kwa NCCR Mageuzi unakutana na udicteta wa mliberali Mbatia. Naye mbowe anaendeleza yaleyale
 
wana jf
mwanzoni mwa mwaka huu kulikuwa na tetesi kwamba uchaguzi wa ndani wa viongozi wa chadema utafanyika kuanzia mwezi wa nne 2013, cha ajabu hivi sasa ni mwisho wa june lakini kimya na hakuna kinachoendelea.

Demokrasia iko wapi ndani ya chadema??? kuna rafiki yangu nlikuwa naongea naye kuhusu hili akasema uchaguzi wa nini wakati viongozi wapo?? je hilo jibu ni sahihi kwamba mfumo wa kifalme umerudi Tanzania? Tumezoea kumsikia Augostino Lyatonga Mrema akiwa mwenyekiti wa TLP tangu ahamie chama hicho miaka zaidi ya 15, John cheyo wa UDP na Prof Lipumba ni mwenyekiti wa kudumu wa CUF.Je hivi vyama ni wale wale??

Unalalamikia tetesi? Uchaguzi hufanywa kwa mujibu wa katiba na sio tetesi you dope
 
ahhaaaa kumbe! ndo maana mzee cheyo anabaki kuwa mwenyekiti wa UDP, CHRISTOPHER MTIKILA kuendelea kuwa mwenyekiti wa DP, Mrema naye kung'ang'ania TLP, huku mzee lipumba naye amekuwa Mungu mtu wa CUF. ukienda kwa NCCR Mageuzi unakutana na udicteta wa mliberali Mbatia. Naye mbowe anaendeleza yaleyale

Mbowe amekuwa mwenyekiti toka lini yakhe ukilinganisha na hao CCM-B wako?
 
Unalalamikia tetesi? Uchaguzi hufanywa kwa mujibu wa katiba na sio tetesi you dope

katiba ya chama chenu inasemaje? mbona tuliambiwa kuwa mchakato wa uchaguzi ulitakiwa uanze mwezi Aprili 2013 na sasa huu ni mwezi wa 7 unaelekea hakuna taarifa yoyote.
 
wana jf
mwanzoni mwa mwaka huu kulikuwa na tetesi kwamba uchaguzi wa ndani wa viongozi wa chadema utafanyika kuanzia mwezi wa nne 2013, cha ajabu hivi sasa ni mwisho wa june lakini kimya na hakuna kinachoendelea.

Demokrasia iko wapi ndani ya chadema???
kuna rafiki yangu nlikuwa naongea naye kuhusu hili akasema uchaguzi wa nini wakati viongozi wapo?? je hilo jibu ni sahihi kwamba mfumo wa kifalme umerudi Tanzania? Tumezoea kumsikia Augostino Lyatonga Mrema akiwa mwenyekiti wa TLP tangu ahamie chama hicho miaka zaidi ya 15, John cheyo wa UDP na Prof Lipumba ni mwenyekiti wa kudumu wa CUF.

Je hivi vyama ni wale wale??
ungekuwa na nia ya kujua kukikoni basi ungesaidiwa, lakini wewe moja kwa moja unajiuliza swali kisha ukajijibu mwenyewe sasa sisi tukusaidie kivipi?
 
Mkuu unataka uchaguzi gani tena wakati Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa Chadema na Dr Slaa ni katibu mkuu wa maisha.
 
Wazee wa matambiko, ndo maana ukiwa ccm lazima uwe na akili kama za zuzu, kumbe ndo mambo wanayofanya ! Tobaaaa
 
katiba ya chama chenu inasemaje? mbona tuliambiwa kuwa mchakato wa uchaguzi ulitakiwa uanze mwezi Aprili 2013 na sasa huu ni mwezi wa 7 unaelekea hakuna taarifa yoyote.

Ni nani aliwaambia hayo? Tupatie ToR za umbea wako huu
 
Mkuu unataka uchaguzi gani tena wakati Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa Chadema na Dr Slaa ni katibu mkuu wa maisha.
uchaguzi utafanyika lakini kuna uwezekano mkubwa msiowapenda magamba wakarudi hao hao, sijui itakuwaje, ebu angalia na ile picha pale juu, ndo maana ukiwa mwana ccm lazima akili ziwe pungufu kumbe mnafanyiwa matambiko
 
Umesahau kusema hata watanzania wamechoka kuendelea kusikia kwamba Tangia mwaka 1977, chama Tawala kimekuwa ni CCM...!
Nao wanataka mabadiliko!
CHADEMA watafanya uchaguzi kwa mujibu wa katiba yao!
 
matarajaio yenu ni kuona uchaguzi ukifanyika na wale viongozi wote wanaitoa jasho ccm hawachaguliwi, uchaguzi upo na muda utafika, chama hakiwahusu kelele lundo nyie watu mna matatizo sana eeeh !

wewe unafikiri nani jeuri ambaye anaweza kuhoji swala la uchaguzi ndani ya chadema labda kama anataka kufa,wangwe alihoji unajua kilichompata.
 
Mh. Mbowe amemuoa mtoto wa mwenye CHADEMA. Kwa hali ya namna hiyo unaweza kuona kabisa kwamba CHADEMA ni mali ya familia na hakuna wa kuweza kumtoa Mh. Mbowe kwenye nafasi yake ndani ya CHADEMA.
 
Back
Top Bottom