Uchaguzi ndani ya CHADEMA lini?

Uchaguzi ndani ya CHADEMA lini?

Mbowe amekuwa mwenyekiti toka lini yakhe ukilinganisha na hao CCM-B wako?

halafu mtu utakaaje kwenye madaraka tangia 2003 hadi leo na unashindwa kukiwezesha chama kushika dola bado unajiona kuwa unafaa kwenye nafasi hiyo. si waachie wengine wanaoweza. tatizo la chadema ni uchaga, udini na ukanda
 
Mkuu unataka uchaguzi gani tena wakati Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa Chadema na Dr Slaa ni katibu mkuu wa maisha.

Na hampendi kweli kweli kusikia Mbowe na Slaa siyo!?
Kwa hiyo uchaguzi mzuri kwako ni ule utakaohakikisha SI MBOWE WALA SLAA ANAYEKUWA KWENYE NAFASI YOYOTE siyo?!
Wana-CHADEMA ndiyo watakaoamua hatima ya chama chao, si nyie wakuja.
 
uchaguzi utafanyika lakini kuna uwezekano mkubwa msiowapenda magamba wakarudi hao hao, sijui itakuwaje, ebu angalia na ile picha pale juu, ndo maana ukiwa mwana ccm lazima akili ziwe pungufu kumbe mnafanyiwa matambiko
aaah, kumbe matokeo tayari, basi tusichezee ruzuku inayotokana na kodi za wananchi, wafalme wale wale waendelee tu
 
halafu mtu utakaaje kwenye madaraka tangia 2003 hadi leo na unashindwa kukiwezesha chama kushika dola bado unajiona kuwa unafaa kwenye nafasi hiyo. si waachie wengine wanaoweza. tatizo la chadema ni uchaga, udini na ukanda

Hayo maneno ya ukanda mbona hamkuyatamka kwenye kampeni za udiwani Arusha???!
Mnauma na kupuliza eeeh?!
Ujinga bwana!
 
Mkuu ulipewa jukumu la kuwa mamluki ndani ya uchaguzi wetu!! subirini mnyolewe!!
 
Na hampendi kweli kweli kusikia Mbowe na Slaa siyo!?
Kwa hiyo uchaguzi mzuri kwako ni ule utakaohakikisha SI MBOWE WALA SLAA ANAYEKUWA KWENYE NAFASI YOYOTE siyo?!
Wana-CHADEMA ndiyo watakaoamua hatima ya chama chao, si nyie wakuja.
kwani huo uchaguzi ulikuwa uwe wa mwenyekiti na katibu peke yao??? au povu tu. kinachotakiwa ni uchaguzi hata kama watarudi wale wale lakini wawe wamechaguliwa kisheria
 
Mh. Mbowe amemuoa mtoto wa mwenye CHADEMA. Kwa hali ya namna hiyo unaweza kuona kabisa kwamba CHADEMA ni mali ya familia na hakuna wa kuweza kumtoa Mh. Mbowe kwenye nafasi yake ndani ya CHADEMA.
Kwani hayo mnayoyaongea ni mageni kwa CHADEMA!
Tushayazoea na tushayapuuza!
Ila endelea kuandika mkono uende kinywani.
 
nina wasiwasi anguko la chdm litakua kubwa sn. unafiki makao makuu ni mwingi kama alivyosema lwakatare.
 
Hayo ndo maisha halisi tuliyo nayo Tanzania ona wapiga kura wanatoka dunia ya kumi wakati wapigiwa kura wao wanatoka dunia ya kwanza jamani hivi hiyo ndo demokrasia kweli viongozi jaribuni kubadili tabia angarau basi mjaribu kufanana na wapga kura wenu
 
Ni nani aliwaambia hayo? Tupatie ToR za umbea wako huu

mkuu soma taarifa hii ya hapa chini. CHADEMA mbona mnaaibika sana. yaani unajifanya hujui kuwa taarifa za uchaguzi ziliwekwa hadharani kupitia waandishi wa habari

[h=2]Wednesday, January 30, 2013[/h] [h=3]Chadema yatangaza mchakato uchaguzi[/h]

[h=2]NA MUHIBU SAID[/h]



Mnyika1%2821%29%282%29.jpg

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama hicho kwa ngazi zote; kuanzia msingi hadi taifa pamoja na mabaraza yake yote, utakaofanyika sambamba na operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) katika kanda 10 nchini kote Aprili hadi Desemba, mwaka huu.



Ratiba ya uchaguzi huo ni sehemu ya maamuzi kadhaa yaliyopitishwa na Baraza Kuu la Chadema katika mkutano wake maalum uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.


Mkutano huo ulikuwa na ajenda tano, mapendekezo kuhusu maudhui na mchakato wa katiba mpya na mapendekezo ya haja ya kufanya marekebisho katika kanuni za chama na kutunga muongozo.


Ajenda nyingine ni mpango kazi, mkakati na mwendelezo wa operesheni ya M4C na bajeti ya chama kwa mwaka 2013 na mengineyo.


Maamuzi ya baraza hilo yalisomwa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.
UCHAGUZI NA M4C


Mnyika alisema uchaguzi wa misingi, matawi, majimbo na wilaya, utafanyika Aprili hadi Septemba, kupitia operesheni za M4C kwa kila kanda.


Alisema chaguzi za mikoa zitafanyika Novemba, wakati ule wa ngazi ya taifa utafanyika Desemba.


Mnyika alisema uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) utafanyika Desemba 11 na kufuatiwa na uchaguzi wa Baraza la Vijana (Bavicha) na Baraza la Wazee wa Chama hicho utakaofanyika Desemba 12.


Alisema Desemba 13 Kamati Kuu, Desemba 14 Baraza Kuu, Desemba 15 Mkutano Mkuu, Desemba 16 Baraza Kuu jipya na Desemba 17 Kamati Kuu mpya.


Pia alisema mchakato wa kuwapata wagombea wa uenyekiti wa serikali za mitaa, vijiji, vitongoji, udiwani, ubunge na urais katika uchaguzi wa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 safari hii utaanza mwaka huu.


Alisema miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika mkutano wa juzi wa Baraza Kuu, ni pamoja na kujiwekea malengo ya kusimamisha wagombea ubunge katika majimbo yote katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kote nchini.


Mnyika alisema suala hilo litakwenda sambamba na chama kuwaruhusu wanachama wanaotaka kuwania nafasi yoyote kati ya hizo kutangaza nia mapema.


Pia Baraza Kuu limezingatia kwamba, matatizo yanayoikabili nchi kwa sasa, ikiwamo migogoro mbalimbali, ni matokeo ya sera mbovu na udhaifu wa kiuongozi wa CCM na serikali yake.


Hivyo, Mnyika alisema Chadema itaendelea kuwaongoza wananchi kuiwajibisha serikali mwaka huu, kueneza sera sahihi za Chadema na kuwaunganisha kuiondoa CCM madarakani katika chaguzi zinazokuja za mwaka 2014 na 2015.


NGUVU YA UMMA
Alisema Baraza Kuu pia limesisitiza falsafa ya chama ya "nguvu ya umma" katika kuongoza utekelezaji wa mpango kazi kwa mwaka huu.


Pia alisema limepitisha utaratibu wa mfumo wa utendaji wa kanda kwa kuzingatia misingi ya ‘sera ya majimbo'.
Alisema katika kuonyesha kuwa wako makini na hilo, Baraza Kuu limepitisha asilimia 40 ya fedha za ruzuku ya chama kupelekwa kwenye kanda hizo kwa ajili ya kutekeleza mkakati huo.
"Chadema inakwenda kupambana na CCM kona zote. Hiyo ndiyo dawa pekee ya kuondoa matatizo nchini," alisema Mnyika.


Alisema M4C itafanyika mfululizo ili kudhibiti nguvu, ambazo Jeshi la Polisi linaweza kujianda kuzitumia kama ilivyofanya katika operesheni zilizopita mkoani Morogoro na Iringa kujaribu kuzizuia.
PIKIPIKI M4C


Mnyika alisema ajenda kuu katika M4C itahusu katiba mpya na rasilimali za nchi na kwamba, tayari chama kimeshanunua pikipiki maalum 126 kwa ajili ya kufanikisha operesheni hiyo.


Alisema tofauti na pikipiki nyingine, ambazo zina majina ya kampuni zilikotengenezwa, pikipiki zilizonunuliwa na Chadema zina jina la M4C na zimefungwa vipaza sauti.


Mnyika alisema Baraza Kuu pia lilipokea na kuridhia taarifa ya Kamati Kuu kuhusu maoni na mapendekezo ya chama kuhusu maudhui na mchakato wa katiba mpya.


Alisema pia limezingatia kuwa katiba mpya bora ni nyezo muhimu ya ufumbuzi wa matatizo ya kiongozi na migogoro inayolikabili taifa, ikiwamo inayohusu rasilimali za nchi.
Mnyika alisema taarifa ya maamuzi ya Baraza Kuu juu ya hatua zitakazochukuliwa kuhusu maudhui na mchakato wa katiba mpya zitatolewa kwa umma.


Alisema vilevile, Baraza Kuu limepokea mapendekezo na kuridhia haja ya kufanyia marekebisho ya kanuni za chama na kutunga muongozo.


Alisema kati ya maeneo ya kanuni yaliyopendekezwa kufanyiwa marekebisho, ni pamoja na kuweka utaratibu wa wajibu na mipaka ya mbunge wa viti maalum kuondoa migongano na wabunge wa majimbo.
Pia kuweka utaratibu wa kuchukua hatua za kinidhamu mapema katika masuala yenye kuhitaji hatua za haraka kwa maslahi ya chama na taifa na mipaka ya wenza wa viongozi kwenye ushiriki wao katika shughuli za chama na nidhamu kuhusu muda wa mikutano.


Alisema vilevile, Baraza Kuu limeridhia kuandaliwa kwa muongozo kuhusu utaratibu wa kutangaza kusudio la kugombea nafasi za uongozi kwenye chama na katika chaguzi za kiserikali kuanzia ngazi za kitongoji, kijiji/mtaa, udiwani, ubunge na urais.
; ikiwamo maoni na



CHANZO: NIPASHE



 
halafu mtu utakaaje kwenye madaraka tangia 2003 hadi leo na unashindwa kukiwezesha chama kushika dola bado unajiona kuwa unafaa kwenye nafasi hiyo. si waachie wengine wanaoweza. tatizo la chadema ni uchaga, udini na ukanda

Unamjua Oliver Tambo? Alikuwa mwenyekiti wa ANC kwa miaka mingapi? Je alikuja kuwa Rais? Hivi MALUMUMBA mnajua siasa kweli?

In 1955, Tambo became Secretary General of the ANC after Walter Sisulu was banned by the South African government under the Suppression of Communism Act. In 1958 he became Deputy President of the ANC and in 1959 was served with a five year banning order by the government. In 1977 Tambo signed the first solidarity agreement between ANC and a Municipality, the relationship starts a relevant strength of the struggle against apartheid. The Italian town of Reggio nell'Emilia was the first city in the world to sign a pact of solidarity.

In response, Tambo was sent abroad by the ANC to mobilise opposition to apartheid. He settled with his family in Muswell Hill, north London, where he lived until 1990. He was involved in the formation of the South African Democratic Front. In 1967, Tambo became Acting President of the ANC, following the death of Chief Albert Lutuli. In 1985 he was re-elected President of the ANC. He returned to South Africa on 13 December 1990 after over 30 years in exile,and was elected National Chairperson of the ANC in July of the same year. Tambo died aged 75 due to complications from a stroke on 24 April 1993.
 

Unalalamikia tetesi? Uchaguzi hufanywa kwa mujibu wa katiba na sio tetesi you dope
mnachojua nyie ni matusi tu sio kingine.look at you!!!!!!!! mbona mleta mada ameuliza swali zuri tu kwann usitumie ustaarabu kumjibu, kwani utapungukiwa nn??
 
mkuu soma taarifa hii ya hapa chini. CHADEMA mbona mnaaibika sana. yaani unajifanya hujui kuwa taarifa za uchaguzi ziliwekwa hadharani kupitia waandishi wa habari

Wednesday, January 30, 2013

Chadema yatangaza mchakato uchaguzi



NA MUHIBU SAID






Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama hicho kwa ngazi zote; kuanzia msingi hadi taifa pamoja na mabaraza yake yote, utakaofanyika sambamba na operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) katika kanda 10 nchini kote Aprili hadi Desemba, mwaka huu.

Sasa Disemba imeshafika?
 
Mbona hamuulizi CHAUSTA, NRA (Mwenyekiti Adam Malima), CCK-formerly CCJ (Katibu Mkuu Nape Nnauye)?
 
Back
Top Bottom