Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Tanzanianjema,
lakini zaidi ndugu zetu wa vyama pinzani hawajaweza kuonyesha kuwa ni best alternative ya CCM

Unajua ndugu yangu hapa kuna utata mmoja mkubwa sana.
Inawezekana kuwa kosa na ujinga ni wetu sisi wapiga kura kwa sababu chama huendeshwa na mrengo, sera zake na mwisho kiongozi.
Lakini tunaposimama hapa na kusema kwamba wapinzani hawajaweza kuonyesha kama ni best alternative nadhani itakuwa tunatazama uzuri wa mwanamke kwa umbile lake. tabia, maradhi na hata weusi wake ni kichefuchefu kwetu.
Mrengo na Sera za vyama vya Upinzani zipo wazi kabisa tena nadhani vimejieleza kwa uwazi kuliko CCM kwa sababu hilo neno Ujamaa na Kujitegemea halipo tena ktk kamusi yao na wengi wetu ni jinamizi ambalo tunashindwa kulipa tafsiri nyingineyo zaidi ya Ukomunisti.
Leo ktk pitapita yangu kurudia kutazama tovuti yao nimeona marekebisho ikiwa ni pamoja na lile lengo la chama -Kuhakikisha ushindi ktk chaguzi sikuweza kuliona tena. Na kama lipo bado jaribu kulisoma vizuri kisha jiulize mwenyewe hii lugha kweli ni lugha ya demokrasia ambayo inampa nafasi ya kwanza mwananchi kuchagua mshindi?..
Mawaziri wetu ndio hao wabunge wetu, Kamati kuu, Wawekeshaji wao wakijiita wajasiriamali na kupewa mikopo mikubwa kuliko fedha za JK kwa mkoa mzima wenye wakazi zaidi ya millioni 2. Wake zao ndio wanazidi kuyachukua majumba ya msajiri kwa kauli ya bwana tu. Na hawa ndio wenye mamlaka ya mwisho kuweka mikataba ya nchi wasiulizwe kitu...
Alternative gani kweli tunaihitaji kama sii kujidanganya wenyewe kuzitazama sura na maumbile ya viongozi wa vyama hivi. Ni ktk mtazamo huo pekee tumekuwa tukichagua viongozi na hata vyama vyetu yaani kwanza uwe na address wewe mtoto wa nani imekuwaje upo Upinzani hali mtu kama wewe ulitakiwa CCM. Kuna sura za watu wanaotakiwa kuwa CCM na wengine wote msiokuwa na address ndio mjipange ktk Upinzani.
Tutafika kweli mjomba?
 

Hiki ndicho kilimfika makongoro Nyerere..wakamgeresha na ubunge wa kuteuliwa ili atoke upinzani, baada ya kumtoa upinzani wamem-bwaga kiaina, wana hakika hatarudi tena upinzani
Huu mtindo wa CCM kuua upinzani nao ni ishara ya kutojiamini katika ushindani wa haki..wanategemea sana wizi wa kura na wanajua bila huo nafasi yao ya kuchuana on merit itakuwa mashakani ndo maana wanahangaika kuwatoa wapinzani upepo ili magurudumu yao yasitembee
 
Mzee ES unasema mambo yako sawa CCM lakini habari kama hizi zinatupa picha tofauti. Anyway, labda utupe picha ya ndani!!

CCM mambo magumu


SOURCE: Nipashe
 
hata na mie nimetatizika huyu komandoo ES ndio yule yule Mzee Es au kulikoni?

kumbe unaweza kubadili jina? kama hivyo na mimi nnaomba nibadili niwe Mtu wa pwani
 
"lakini zaidi ndugu zetu wa vyama pinzani hawajaweza kuonyesha kuwa ni best alternative ya CCM.....Hii ndio challenge kubwa anayokumbana mpiga kura wa Tanzania."


End of the story na Full Stop!
 
Mtumwitu na Zero,

You got it right, jina limebadilika kutokana na times na mazingara, lakini mawe ni yale yale ya kumkoma nyani na mpaka ijulikane wasup!
 
sasa uzee basi umekuwa kijana na komandooo? duh sasa hii hatari, na mie hebu nibofyulie hii siri ya kubadili jina
 
sasa uzee basi umekuwa kijana na komandooo? duh sasa hii hatari, na mie hebu nibofyulie hii siri ya kubadili jina
Wapo wengine waliobadili; nenda kwenye profile yako, kwa mfano aliwahi kuwepo Mwanasiasa siku hizi anajiita Kitila.
 
mwendapole you are right ...nadhani mako bado angeweza kuwa mbunge mzuri tu kuliko wabunge wengi...wakati wa kampeni nakumbuka jk alienda kuomba baraka za mama maria na kupata wasaa binafsi kuomba kwenye kaburi la mwalimu hadi kufikia kugaragara kwa hisia ....
mama maria na hata mwalimu kabla hajafariki yupo busy na kusomesha wajukuu zake ..i was taken by emmotions walipokua wanamshukuru museveni mbele ya jk kwa kuwalipia wajukuu za mwalimiu ada kwenye nchi mbalimbali ..sijui na mandela labda...siku moja mmoja wao anaweza kurudi kawa atakuwa na uwezo atakuwa na kumbu kumbu ya kusomeshwa na museveni kama babu yao alivyomsomesha museveni....unajua mwalimu angetaka asingeshindwa kufanya tukawa na amani karume ,eyadema jr,joseph kabilla ets..so lazima tumuenzi ..especially jk lazima amuenzi kwa vitendo ..ikiwemo kuliendeleza jina la mwalimu kwenye siasa za tanzania ...kama alivyiofanya mkapa kwa angalao kumkumbuka mmoja wa vijana wake..ie mako..
 
"lakini zaidi ndugu zetu wa vyama pinzani hawajaweza kuonyesha kuwa ni best alternative ya CCM.....Hii ndio challenge kubwa anayokumbana mpiga kura wa Tanzania."


End of the story na Full Stop!

Hivi unataka waonyeshe nini?? Unafikiri upinzani wa TZ na nchi nyingine kama Zambia (Chiluba) na Malawi walipoingia madalakani unatofauti gani? CCM wenyewe hatuoni wanachokifanya zaidi ya kuuza nchi. Infact wanaturudisha nyuma. Sasa hivi tunataka mzalendo wa kweli ili atukomboe siyo Baby Face!!! Tatizo bongo tunachagua rais bila kuangalia uwezo na commitment utafikiri tunampeleka kwenye mashindano ya Mr. President.
 
"Tatizo bongo tunachagua rais bila kuangalia uwezo na commitment utafikiri tunampeleka kwenye mashindano ya Mr. President."


Mzee acha contradictions, kuhusu nani wa kulaumiwa kati ya sisi wananchi na ccm au upinzani, hebu rudia tena nani wa kulaumiwa? Maana at one point unalaumu ccm na hapa unalaumu wananchi, what is up?
 
Komandoo,

Of course CCM ndiyo walaumiwa number one kwa kuwaacha 80 % ya wananchi vijijini bila elimu ya maana ili waendeleze utawala wao (Nafikiri unanielewa). Wananchi nasi kwa kushindwa kutumia busara zetu. Kama tunataka mabadiliko inabidi yaanzie mijini especially Dar lakini TZ mabadilioko yanaanzia Tarime.

Kuhusu Baby face, just a joke kwa kuwa huku ughaibuni watu most of the guys wanamsifu kwa uzuri alafu wanadai rais kijana kumbe hawajui hata BWM 1995 alikuwa na umri huohuo wa JK ila kwa sababu ya sura ya kunyata watu walifikiri ni mzee!!!
 
Jamani mlio nyumbani hamna hata mmoja aliyepata nyeti za nani kapita nani kabwagwa?Mzee ES,tunasubiria breaking news kutoka kwako uliye jikoni.

PS.Najua heading yangu inaweza kumzuga mtu kudhani posting yangu ina majina.Sorry if it misled anybody,which is likely.
 

Mgema alifariki dunia!
 
Mark Mgema alifariki dunia, lakini naye alikuwa Mtandao.
 
Mlalahoi,

Nilidhani una news, kumbe nawe unasubiri kama wengine tu!
 
Swala la nani wa kumlaumu kwa predicament tuliyonayo leo Tanzania, ni swali tete. wote tunahusika katika kuijenga na kuiendeleza hii hali. Wananchi na CCM kwa pamoja tunahusika. Wananchi, wafanyakazi na wakulima tumejifanya kama hatuoni madudu ya CCM...kila uchaguzi ukija tunawapa kura, na baada ya hapo ndo tunaanza kulaumu hali ngumu na matatizo mengineyo. Uchaguzi ukifika, matatizo yote TUNAJIFANYA KUYASAHAU na kuamua kujipa imani kwamba this time it will work, as a result inakuwa vicious circle ya umaskini na ulalamishi. Bila kufanya kinachotakiwa.

Vile vile CCM, wakija kuomba kura wanakuja na sera na maneno mazuri. Wananchi wanawaamini wanawapa miaka mingine mitano. wakishaingia madarakani, wanaangalia maslahi yao na ni namna gani watashinda uchaguzi ujao. Mwisho wake ni nini? vicious circle ya umaskini kwa walio wengi na utajiri wa kutupwa kwa walio wachache.

Kipi kifanyike. Ni wahusika wote CCM na wananchi tuamke tugundue kwamba hizi siasa za kudanganyana, hazitatufikisha popote. Kwani lazima tulijue hili..wana ccm, wanachadema, wanacuf na wengineo, tunaweza kutofautiana kisera na kimtizamo, lakini wote ni watanzania na aneyeumia ni mtanzania, haidhuru yuko chama gani, Usidhani kila mwana CCM ana neema, la hasha..wengi ni njaa tupu!. Swala kwamba wananchi hawajasoma kwa hiyo hawawezi kulielewa hili..ni utter nonsense! Nchi yetu ni jukumu letu sote. Hili halitafanywa na Mbowe wala Zitto ni mimi na wewe kupiga kura kwa kuamini kwamba tunahitaji kuleta mabadiliko. Hata Zambia na Kenya tunaowatolea mifano, ni WANANCHI period. Ndo waligundua kwamba wanachezewa sanaa. Na siamini kwamba Wazambia wana akili kuliko watz!

Ukiamini kwamba wapinzani hawajaiva kisiasa, je tuliowapa dhamana ya nchi na wako madarakani kwa miongo zaidi ya minne, wamefanya nini kuonyesha kwamba wamekomaa kisiasa? zaidi ya kutuweka katika lindi la umaskini? Mwenye Jukumu la kuibadirisha Tanzania ni mwananchi wa kawaida! Tusitegemee CCM au upinzani kubadilisha mambo. Katiba ni mbovu hilo halina ubishi..je kipi kifanyike? CCM hawatakubali kuibadilisha kwa sababu inawapa nafasi wao, kwa hiyo njia mbadala ni kuingia na kupiga KURA kwa viongozi/chama chenye mwelekeo wa kuongoza juhudi za wananchi kujikomboa. Na wananchi wanalijua hili. Na kikubwa ni elimu..vijana wengi wapiga kura sasa wana hata elimu ya std seven na form four, na hawa ndo hawana kazi, wameahidiwa ajira hewa millioni moja kila mwaka, wakigundua kwamba huu ujinga unaofanywa na watu wachache ndo unaturudisha nyuma, basi twaweza fika mbele. we ukiona watu wako ughaibuni, wanaanzisha matawi ya CCM, unadhani wanaipenda CCM? nagoma kuamini hivyo, ni OPPORTUNISTS wanaamini kwamba inabidi waingie kwenye system ya chama ndo wafanikiwe nyumbani, kitu ambacho wanafanya wasomi walio majuu, iweje alaumiwe babu yangu wa Sengerema kwa kukubali kuipigia kura CCM kwa doti ya khanga au shati? moja kwa moja hapa elimu ya wananchi wetu sio kikwazo kwani wabinafsi namba moja ni wasomi, mimi na wewe tunaokaa kwenye PC zetu na kuandika humu JF na kwingineko! Swala sio Elimu, swala ni kuacha unafiki na kuelewa priorities na changamoto zinazolikabili taifa. Lets try, its possible.

Kwa sasa usitegemee EL na JK kufanya mabadiliko yoyote. wanafikiria namna ya kushinda 2010. Tuamke, twende kupiga kura, taratibu mambo yatabadilika! wachache walio upinzani akina Zitto, ni kizazi ambacho kimeweka historia na Iam sure wengi humu tunalilia changes, lakini hata kuweka jina humu JF tunaogopa! kwa sababu system itatufuatilia...mbona Zitto ameweza? WHATS UNIQUE bout him? he knows the challenges facing our country and he is ready to sacrifice the smallest he has fo the good of his country. Mi na wewe je? wote hatuwezi kuingia siasa, lakini hakika tunaweza kuchangia pale tunapoweza.
 
"Mark Mgema alifariki dunia, lakini naye alikuwa Mtandao"

Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mwanza, hakuwa mtandao bro angekuwa Cheyo (UDP) asingeshindwa uchaguzi mdogo wa bunge maana mtandao wote walikuwa wakimsaidia Cheyo, mpaka vigogo wazito!

Kama angelikuwa hai, alikuwa ndiye target namba moja, kuondolewa na mtandao! Ukienda kwenye thred za huko nyuma tulishayazungumza haya zamani sana bro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…