Elections 2010 Uchaguzi mkuu: Mawaziri kuanza ziara za mikoani!

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
KATIKA kile kinachoonekana ni kujipanga vema na kujihami kwa maswali magumu wakati wa kampeni za uchaguzi, Ikulu imetoa waraka wa kuzuia mawaziri kusafiri nje na badala yake kuwaagiza kuzunguka mikoani kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne.

Waraka huo, ambao umepewa jina la "Mlitutuma, Tumetekeleza, Tumerudi Kuwaelezeni Tulivyotekeleza na Kuwasikilizeni", pia unawaagiza mawaziri kukutana na watu wa aina mbalimbali kwenye ziara hizo, wakiwemo viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

-Haya ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kabisa kwa sababu sioni watacho ongea huko mikoani kwani hawana walichofanya.

-Sisi wafanyakazi hatuwataki hata kuwaona kwani tulishaambiwa na muajiri wetu mkuu kuwa hanihitaji kura zetu ili awe rais, sasa watuache tuamue cha kufanya wakati ukifika.

-Waende kuongea na wazee wa kila mkoa kama JK alivyofanya ILI WAPIGIWE MAKOFI NA VIGELEGELE, WAKIJA KWETU TUNAWAKIMBIZA.

JAMANI JAMANI TUMECHOKA, SISIWANANCHI TUKISEMA UOZO WA SERIKALI, MAWAZIRI WANAKAA KIMYA ILA DEVELOPMENT PARTNERS WAMESEMA MAMBO MAKUU MATATU KAMA KASI NDOGO YA KUSHUGHULIKIA UFISADI, KUSHINDWA KWA SERIKALI KUPANDISHA UCHUMI NA MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI NA KUSHINDWA KUSIMAMIA HELA ZA SERIKALI WAZIRI WA FEDHA ANAHAHA NA ANAANDAA TAARIFA.JE KIPI HAO MAWAZIRI WATAENDA KUWAAMBIA WANANCHI WAKATI TAYARI HATA WAGENI WANAJUA KUWA SIO WAADILIFU?

Mkereketwa.:rip:

Tatizo kuna watu wasiojua jinsi ya kupambanua hoja. Ukweli ni kwamba, kitendo cha Serikali kuwatumia mawaziri kwenda mikoani "kuelezea" utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni sawa na kufanya kampeni, tena kwa kutumia fedha za Watanzania, walipakodi, wengi wao ambao si wanachama wa CCM.

Kinachojadiliwa hapa ni utawala bora wenye uwajibikaji. CCM na Serikali yake inatumia fedha za wananchi kwa kufanya kazi za Chama, kwa kigezo kwamba Serikali ina wajibu wa kuwaelezea wananchi jinsi ilivyotekeleza ahadi. Kwa nini isingoje wakati wa Kampeni na ifanye hivyo kwa kutumia fedha zake? Huu ni wizi, tena wa mchana kweupe!

./Mwana wa Haki
 
Hata mii nafikiri hawa jaamaaa wameanza kampani kiana kabra ya kipyega kupulizwa
 
Tatizo kuna watu wasiojua jinsi ya kupambanua hoja. Ukweli ni kwamba, kitendo cha Serikali kuwatumia mawaziri kwenda mikoani "kuelezea" utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni sawa na kufanya kampeni, tena kwa kutumia fedha za Watanzania, walipakodi, wengi wao ambao si wanachama wa CCM.

Kinachojadiliwa hapa ni utawala bora wenye uwajibikaji. CCM na Serikali yake inatumia fedha za wananchi kwa kufanya kazi za Chama, kwa kigezo kwamba Serikali ina wajibu wa kuwaelezea wananchi jinsi ilivyotekeleza ahadi. Kwa nini isingoje wakati wa Kampeni na ifanye hivyo kwa kutumia fedha zake? Huu ni wizi, tena wa mchana kweupe!

./Mwana wa Haki

asante...Muelimishe huyu malaria sugu! I wonder what percentage of Tzians dont see this!
 
Tendwa mbona anatendwa halafu kimya?! CCM wameanza kampeni. Kwani kampeni huwa nini? si kwenda kwa wananchi na kuwaeleza sera zako ili wakuchague? Mbona CCM wanaenda kuafanya hivyo sasa, kwa fedha ya walipa kodi?

Tendwa wanakutenda hao mjomba. Wewe unakomalia CCJ isipate usajili wa kudumu watu wanakutenda huko!
 
malaria sugu,shame on you!! nina uhakika hukuisoma hiyo habari between lines japo poits za kuipinga hizo ziara zipo peupe kabisa. CHADEMA hawapingi mawaziri kutembelea mikoani ila suala wanaenda kufanya nini kwa gharama ya nani na kwa wakati gani?
screw up yourself!
 
Back
Top Bottom