Ziara za mikoani za Rais Samia zageuka kero na mateso kwa wafanyabiashara

change formula

JF-Expert Member
Sep 8, 2020
694
1,463
Kimekuwa kilio cha muda mrefu kwa wafanyabiashara wa mikoani kinachosababishwa na ziara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kawaida Rais anapokuwa mkoa fulani huongozana na kundi kubwa la watumishi wa idara mbalimbali za serikali, kutoka wizarani, mikoani, wilayani, watu wa vyombo vya ulinzi na usalama n.k Kumekuwa na michango ambayo wafanyabiashara tumekuwa tukichangishwa kwa lazima tukiambiwa kuwa ni kuwezesha ziara ya Rais iweze kwenda vizuri.

Suala hili limekuwa kero kwa wafanyabiashara wengi maana biashara ni ngumu sana na pia tunalipa kodi mbalimbali kwenye mamlaka za serikali mfano TRA, OSHA, EWURA, NEMC, Fire, Halmashauri ya manispaa, nk! Kodi ni nyingi mno ila bila huruma wanakuja tena kutuchangisha michango ya kuwezesha ziara ya Rais. Na ukikataa kutoa utaandamwa sana na mamlaka za mikoa ukionekana sio mzalendo inabidi tu utoe kishingo upande.

Kibaya zaidi ni utapeli tunaofanyiwa na hao watumishi wa serikali ambao wanakuja kwenye biashara zetu hasa kwenye mahoteli yetu. Wanalazimisha tusipokee wateja wetu wa kawaida tuwaachie wao nafasi, wakisha tumia vyumba wanakimbia bila kufanya malipo yeyote, wanatuachia madeni. Hata ukipeleka invoice za kudai malipo kwenye ofisi za idara zao, hawataki kulipa wanaishia kukuzungusha tu mwaka mzima mpaka unakata tamaa.

Hasa hizi idara za usalama za Serikali kama wanakuwa hawana bajeti za kulala mahotelini kwanini wasiweke mahema kwenye viwanja vya wazi wakalala humo? Biashara ni ngumu kodi ni nyingi ila bado mtutese kwa kutukopa na kutudhulumu pesa zetu? Mbona sisi tunalipa kodi kwa wakati na tukichelewa tunapigwa faini kubwa.

Naomba ofisi ya Rais na wasaidizi wake walitazame hili kwa umakini linamletea sifa mbaya na chuki kwa wafanyabiashara, au kama hana bajeti ya kutosha asifanye ziara mikoani abaki uko uko Dar es Salaam na Dodoma tumechoka.

Mbona wakienda huko kwa mabeberu kwenye ziara zao wanalipa mahoteli na huduma walizotumia bila ubabaishaji wowote?
 
Back
Top Bottom