- Thread starter
- #21
Mtazamo wako uko sahihi,uchaguzi huu utatoa picha kama kweli hawa ndugu zetu wanyamwezi/sukuma wamebadilika kama ilivyokuwa kanda ya ziwa.Hakika umaskini na elimu ni chanzo cha mgando wa fikra.Tabora kwa ujumla imekuwa ngome ya CCM kwa muda mrefu, na ukiangalia hakuna jimbo lolote lililowahi kuchukuliwa na chama chochote zaidi ya CCM. pamoja na miundombinu duni na huduma mbovu katika mkoa wa Tabora bado watu wake wamekuwa hawana mawazo mbadala zaid ya kuchagua CCM. Tabora ni moja ya mikoa iliyonyuma sana katika huduma nyingi za kijamii na maendeleo kwa ujumla huu ni mkoa kati ya mikoa maskin katika nchi hii, lakini kuna mambo mengi yanatokea lakin nina mashaka kama wana Tabora wako tayari kuchagua vyama pinzani hili linatokana na sababu mbalimbali ikiwamo uduni wa elimu na umasikini hasa sehemu za vijijini. Lakin hilo halina maana kuwa vyama vya upinzani hawawezi kushinda najaribu kutoa mtizamo wangu.ninachowashauri vyama vyingine vitafute au viweke wagombe wenye sifa na upeo na wanaokubalika na wananchi vinginevyo jimbo hili litarudi mikononi mwa CCM. Katika kampeni za mwaka jana CCM ilishinda majimbo yote kwa urahisi kwakuwa vyama vingine vilikuwa na wagombea wengi wasio na sifa na upeo mkubwa na walikuwa hawakubaliki.Nilikuwa Tabora muda huo.
Ni mtizamo tu.