Bila uchaguzi mdogo Igunga tusingejua haya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
[h=1][/h]
picture-73.jpg

Na Nyaronyo Kicheere - Imechapwa 12 October 2011

Waraka wa Wiki


KILA mtu ana kitu alichojifunza kutokana na vituko vya uchaguzi mdogo wa Igunga. Kwa mfano, nimegundua kwamba hapa Tanzania kuna mabaraza mawili makuu ya Waislamu; BAKWATA na BAKWACHA ambayo nisingeyajua kama uchaguzi mdogo usingefanyika.
Bakwata (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania), wao walibakia Dar es Salaam na katika makao yao mikoani na wilayani na hawakujihusisha na siasa za Igunga. Nimembiwa Bakwata wanashughulika na mambo ya dini na kwamba hawanunuliki kwa mambo ya kidunia.
Kwa upande mwingine, Bakwacha (Baraza Kuu la Waislamu wa Chama cha Mapinduzi), wao walihusika sana na uchaguzi mdogo wa Igunga na walisafiri mpaka Igunga ambako walitoa kauli kali na nzito kupinga wasiowataka na kuunga mkono mgombea wa CCM.
Tofauti nyingine niliyoiona kati ya Bakwata na Bakwacha ni tafsiri yao ya hijabu. Bakwata wanasema vazi la hijabu linafunika mwili mzima wa mwanamke kasoro viganja vya mikono yake na uso, tafsiri ambayo imepingwa vikali na Bakwacha.
Bakwacha wanasema mtandio wa kitambaa chepesi kinachofanana na neti ya mbu kikifunika kichwa nacho ni hijabu na kwamba yeyote anayemfunua mwanamke kitambaa hicho basi huyo ni adui wa Uislamu na hastahili kupigiwa kura!
Kwa mujibu wa Bakwacha, mtu aliyevaa mtandio, ambao kwao ni hijabu, hata kama kifua chake kakiacha wazi na kaacha wazi miguu yake ili wapita njia waamue kama anao usafiri au hana, hastahili kukorofishwa na yeyote.
Kifupi, uchaguzi wa Igunga umetufumbulia fumbo la hijabu ambapo tumegundua kwamba hijabu zipo aina mbili; moja inayotambuliwa na Bakwata na nyingine inayotambuliwa na Bakwacha na hata masheikh na maullamaa nao wapo wa Bakwata na wengine wa Bakwacha.
Uchaguzi wa Igunga pia umetudhihirishia kuwa zipo Tume mbili za uchaguzi; Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Taifa ya CCM. Tatizo letu kubwa ni pale linapotolewa tamko fulani, tunashindwa kupambanua limetolewa na tume ipi, na ipi inafanya kazi gani, ile ya CCM au ile ya taifa?
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Rajabu Kiravu, alikemea kitendo cha CHADEMA kumkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario na kumweka chini ya ulinzi wao akisema ‘ni uhuni!’
Siku mbili baadaye tukapata habari kuwa watu waliodaiwa kuwa ndio waliomkamata Mkuu huyo wa wilaya ya Igunga walikamatwa na kufikishwa mahakamani. Lakini maelezo ya hapo juu kama yalivyoripotiwa na vyombo vya habari tayari Mkurugenzi Kiravu keshawahukumu CHADEMA kwa kosa la kukamata DC!
Tatizo litakuwapo siku washitakiwa hao wakishinda kesi. Hapo ndipo itakapodhihirika kuwa Mkurugenzi yule alikuwa akifanya kazi ya Tume ya Taifa ya CCM na siyo alikuwa akifanya kazi ya ukurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Ndiyo maana sisi wengine tuliposikia na kusoma magazetini kwamba kuna shahada za kupigia kura zilinunuliwa kama njugu hatukushangaa. Nani angekemea tatizo hilo?
Ushangae nini wakati mkurugenzi mwenyewe wa Tume anailaumu CHADEMA kabla ya polisi kukamata na kabla ya polisi kushitaki mahakamani na kabla ya mahakama kusikiliza na hatimaye kuhukumu kama CHADEMA wana hatia au la?
Mengine yaliyojitokeza huko Igunga ni pamoja na namna polisi wetu wanavyofanya kazi. Na siku zote tunamsikia Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa, akilalamika kuwa polisi ni wa CCM na kwamba hakuna polisi wa taifa. Yawezekana kuwa kweli, hebu tuchunguze.
Imeelezwa huko Igunga kuwa wabunge wawili wa CCM wakiandamana na wafuasi wao walivamia hoteli walikofikia viongozi wa kitaifa wa CHADEMA. Ikatolewa taarifa polisi kuwa ulikuwepo uvamizi kwenye hoteli ya CHADEMA. Kilichofuata ni kichekesho.
Polisi walipofika waliwasikiliza wavamizi badala ya kuokoa waliovamiwa. Wavamizi wakasema walikuwa wamerushiwa risasi kutoka ndani ya hoteli. Polisi kusikia hivyo wakaingia hotelini na kumpekua Mratibu wa Uchaguzi wa CHADEMA Mwita Waitara wakisaka bunduki.
Mtu aliyevamiwa badala ya kuokolewa anapekuliwa! Sasa alikuwa anapekuliwa kwa sababu ni kiongozi wa CHADEMA au kwa sababu kavamiwa au kwa sababu ni Mkurya? Ndiyo. Lazima tujue kwa sababu yaelekea polisi wa CCM wanasema Wakurya wagomvi, kukitokea tatizo linawahusu basi wao ndio washughulikiwe.
Hayo ndiyo maelezo pekee kwa nini mtu aliyevamiwa anapekuliwa badala ya kukamata mvamizi. Kisa ni Mkurya mgomvi. Ilionekana polisi walitaka kuhakikisha kama Waitara alikuwa na silaha na hajiokoi kwa kuwapiga risasi wavamizi, bali wavamizi walionekana bora watimize nia yao ya kumdhuru kuliko Waitara kujihami.
Hata hivyo, sheria ziko wazi. Polisi wanatakiwa kulinda mali na maisha. Katika kulinda mali na maisha polisi wanaruhusiwa kutumia silaha. Silaha zinatakiwa kutumika popote pale panapotokea uvamizi.
Hata mila za mkoani Mara zinaruhuu kuua mvamizi na kuna methali isemayo: “Omonto achele isiko leo omteme nomtihache na ng’ana yangekugambwa” yaani mtu akikufuata uwanjani kwako unayo haki kumpiga na gongo na hakuna atakayekusema. Kwa maana hii kama Waitara alikuwa na bunduki alikuwa na haki kuitumia kujikinga na uvamizi.
Hao ndio polisi wa CCM. Na kudhihirisha u-CCM wao, walipowakuta watu waliovaa mashati ya kijani wamebeba mapanga, pinde na mishale wakiwashambulia wapinzani hawakukamata hata mmoja na leo tunasikia wanasifiwa kuwa walikuwa wavumilivu.
Lakini tunajua uvumilivu wa polisi unatokea kama nguo zilizovaliwa ni kijani, zikiwa za bluu shida. Jiulize mwenyewe kama wenye mapanga, mikuki na mishale wangekuwa wapinzani leo hii tungekuwa tumezika maiti ngapi Igunga?
Nasema haya nikikumbuka polisi wa CCM wakiongozwa na IGP mtabiri na mpiga ramli anayeweza kujua maandamano yatakayokuwa na vurugu kesho yake walivyoua Arusha kwa kisingizio cha hofu ya kuvunjika amani. Tusiende mbali jambo hili liko mahakamani.
Hayo ni ya Igunga. Nami natamani Igunga nyingine tuone vituko vya serikali inayodai watendaji wake hawapendelei upande wowote.
Hata kama Waziri wa Ujenzi, John Magufuli anapopigiwa simu mkutanoni kwenye kampeni aahidi ujenzi wa daraja la Mbutu! Hata kama Wziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha anapotembelea kambi ya CCM kuelekeza mikakati ya kampeni!
Ninavyojua mimi yamebaki magamba mawili ambayo bado kubanduka kutoka CCM. Kwanza ni Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond/ Dowans na mbunge wa Monduli Edward Ngoyai Lowasa ni mmojawapo.
Pili ni Mwanasheria mkuu wa zamani na mbunge wa Bariadi Mashariki mkoani Shinyanga, Andrew Chenge, maarufu kama Mzee wa Vijisenti ambaye kajikalia kimya utadhani siye gamba. Wakibanduka hawa tutapata fursa ya kuona vituko vingine – tuachane na ya Igunga.
 

Kimilidzo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
1,346
594
Hawarudii tena kupima upepo wa uchaguzi mdogo. Yaliyowakuta Igunga yanawatosha, hadi wamegeuka kuwa interehamwe kwa kuua wafuasi wa CDM watatu ujue sio chama cha siasa tena. Huko tutakoenda kwa chaguzi ndogo (Kuanzia kwa Mwakyembe) hawa CCM wanaweza kuanza kuua hadharani kwa vile jeshi ni lao haliwafanyi kitu. Walianza kuiba kura kweupe sasa wataamua kufanya mauaji kweupeeee, si wameua mafichoni lakini polisi hawafanyi hata uchunguzi.
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,502
3,041
kuna sheria kwa wenzetu ya watu kuvaa face maskwakati wa maandamano, hiyo ina ruhusiwa lakini ukifanya kitendo cha uvunjifu wa sheria mfano kupiga mawe nk nk basi polisi wanayo mamlaka ya kukuvua hiyo face mask yako, vivyo hivyo kwa muhalifi yoyote ambaye katika purukushani za kumshika au kumtambua .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom