T2015CCM
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 7,930
- 991
Tangu alipojiuzulu ubunge na nyadhifa zote za uongozi ndani ya CCM. Rostam aziz alifungasha virago vyake na kuelekea dubai.
Ghafla tu aliposikia Tanzania tuna uchaguzi mwaka huu amerudi nchini na zaidi imedokezwa kuwa amechukua mikoba ya master minder wa mipango ya urais ya mgombea mmoja ambaye anatumia sana faranga kutafuta uungwaji mkono katika harakati za urais.
Kwa hali hiyo tuseme kingmaker amekuja kuwachongea watanzania mfalme mpya?
Ghafla tu aliposikia Tanzania tuna uchaguzi mwaka huu amerudi nchini na zaidi imedokezwa kuwa amechukua mikoba ya master minder wa mipango ya urais ya mgombea mmoja ambaye anatumia sana faranga kutafuta uungwaji mkono katika harakati za urais.
Kwa hali hiyo tuseme kingmaker amekuja kuwachongea watanzania mfalme mpya?
By Weston SongoroWana JF;
Hivi karibuni, gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki lilichapisha taarifa za aliyekuwa mbunge wa Igunga kwa tiketi ya CCM, ROSTAM AZIZ kuchukua nafasi ya Apson Mwang'onda kama campaign manager wa Edward Lowasa ambaye anausaka kwa udi na uvumba Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM. Baada ya kusoma taarifa hiyo, nilianza kufuatilia ili kujua ukweli wake. Nilitaka kujua ikiwa Rostam Aziz ambaye alihamishia shughuli zake za kibiashara Nairobi na Dubai baada ya kushinikizwa na CCM kujivua gamba kutokana na kujihusisha na vitendo vya ufisadi amerejea nchini. Pia nilitaka kufahamu amerejea kama mfanyabiashara au mwanasiasa. Pia nilitaka kufahamu mambo ya msingi anayofanya baada ya kurejea nchini.
Kama kumbukumbu zenu zipo sawa, mtakumbuka kuwa baada ya 2005, liliibuka kundi la watu wachache waliohodhi chama tawala, CCM na kufanya maamuzi mengi kwa niaba ya vyombo vya chama ( Party Machinery) kama vile sekretarieti, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Si kwenye chama tu bali pia walikuwa na maamuzi ndani ya Serikali. Hao mabwana ndio waliokuwa wanaamua nani awe Waziri, nani awe Mkurugenzi wa Halmashauri, Nani awe Katibu Mkuu, nani awe Jaji, nani awe Mkuu wa Mkoa au Wilaya nk. Watu walioteuliwa kwa mgongo wa mafisadi hao walianza kuwatumikia mabwana zao huku wakitekeleza maagizo kadhaa ya kuwanyonya Watanzania. Kutokana na hali hiyo, utawala wa JK awamu ya kwanza ukagubikwa na kashfa mbalimbali za kifisadi zikiwahusisha wanasiasa na watendaji wa serikali. Hali hiyo iliendelea kwa kupindi chote cha awamu ya kwanza na mwanzoni mwa awamu ya pili ya utawala wa JK.
Baada ya uchaguzi Mkuu wa 2010 ambapo chama hakikufanya vema kutokana na athari za vitendo vya mafisadi hao, chama kilijitathmini chenyewe na kiliunda kamati ya watu weledi na waadilifu ndani ya chama iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama, Wilson Mukama. Kamati hiyo ilibaini mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na chama kuhodhiwa na watu wachache wenye pesa ambao ndio walikuwa na maamuzi ndani ya chama. Kwa bahati mbaya zaidi image ya watu hao katika jamii ilikuwa ni negative kutokana na kuhusika na kashfa kadhaa za ufisadi uliotokea hapa nchini. Watu hawa walichafua sana taswira ya chama kiasi ambacho madudu yao yalionekana kuwa ni madudu ya chama. Kwa hali hiyo, kamati hiyo ya Mukama ilikuja na maazimio kadhaa moja likiwa ni kujivua gamba na wasipojivua wavuliwe kwa nguvu. Kwa bahati mbaya sana azimio hilo lilipokelewa kwa hisia tofauti kiasi ambacho chama kilitengeneza ufa ambao ulitenganisha baina ya mafisadi wachache na mawakala wao na wanachama wasafi ambao ni wengi.
Miongoni mwa mafisadi ambao walipaswa kujivua gamba ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Tabora, Rostam Aziz. Wengine ni pamoja na swahiba wake mkubwa kisiasa, Edward Lowasa ambaye walipiga deal za ufisadi kwa pamoja na Andrew Chenge aka Nyoka mwenye Makengeza. Dhana ya kujivua gamba ilimkolea Rostam na akaona isiwe tabu. Julai 2011, Rostam alijivua gamba na kuachia nafasi zote za kisiasa ndani ya chama ikiwa ni pamoja na ubunge. Baada ya kujivua gamba, Rostam alikimbia nchi na shughuli zake za kibiashara akahamishia Nairobi, Kenya na Dubai, United Arab Emirates. Rostam alisikika akisema kuwa hatarejea tena nchini kwani alihisi kuwa usalama wake ni mdogo.
Miaka minne sasa imepita tangu Rostam ajivue gamba. Umaarufu wake kisiasa ulipotea kabisa kiasi ambacho hakuna mwana CCM ambaye aliona pengo la Rostam. Kibiashara, Rostam alidorora sana. Rostam ambaye aliwahi kushika nafasi ya kwanza kwa utajiri nchini sasa alisahaulika kabisa. Washindani wake kibiashara kama Reginald Mengi walianza kupumua kwa vile vijembe vya kibiashara vilianza kutoweka. Wakaanza kuibuka wawekezaji wa kweli kama akina Said Salim Bakhresa ambao waliamua kujikita kwenye biashara na kuweka kando masuala ya kisiasa. Waliwekeza kwenye biashara halali zinazopimika kwenye mizani ya kibiashara na hivyo kujijengea heshima kwa Watanzania.
Huko ng'ambo, Rostam Aziz hakuwa lolote wala chochote. Kwenye orodha ya wafanya biashara maarufu huko Kenya na UAE, Rostam hayumo. Akaona isiwe tabu. Akaamua kurejea nchini kuweka mikakati ya kupiga deal za kifisadi hasa ikizingatiwa kuwa swahiba wake Lowasa anausaka Urais kwa udi na uvumba. Waswahili wanasema kuwa mwiba unapoingilia ndipo unapotokea.
Kabla ya 2005, Rostam Azizi hakuwa chochote. Kama alikuwa na utajiri basi ni wa kiasi cha mboga. Uchaguzi wa 2005 ndio uliomuibua Rostam. Umaarufu wa mgombea wa CCM wakati huo, Jakaya Kikwete ulimshawishi Rostam kuwekeza kwa mgombea huyo na alitumia chochote alichojaaliwa ili mgombea wake aende Magogoni. Jakaya akamuona Rostam ni mtu mwema. Kumbe wapi. Ni chui aliyejivika ngozi ya kondoo. Kumbe alikuwa na malengo yake. Baada ya uchaguzi na Jakaya kuibuka Mshindi, Rostam akiwa na swahiba wake Edward Lowasa ambaye alikuwa Waziri Mkuu wakaanza kupiga madeal ya mahela kwa pamoja. Wakaunda kampuni nyingi hewa ambazo kwa ushawishi wa Lowasa zikapewa zabuni nyingi za serikali tena kubwa kubwa. Kampuni ya kwanza ilikuwa ni Kagoda ambayo inasemekana kuwa Rostam kwa kushirikiana na Lowasa walipiga zaidi ya bilioni 40 kupitia EPA.
Baada ya EPA, ROSTAM na swahiba wake Lowasa wakahusika na kashfa mbalimbali za ufisadi kupitia makampuni yao. Miongoni mwa kashfa ambazo watanzania hawatazisahau ni pamoja na Richmond ambapo Lowasa na Rostam walipiga zaidi ya bilioni 200. Richmond baadaye ilibatizwa na kuitwa Dowans/Simbion. Baada ya hapo hakika Rostam bila haya wala soni akaamua wazi wazi kufanya ufisadi huku akiamini kuwa anakingiwa kifua na swahiba wake Lowasa.
Kupitia kashfa hizo, Rostam akawa jeuri. Akawa yeye ndo mwenye maamuzi ndani ya chama na serikali kwa vile alikuwa na pesa za kuwanunua wajumbe wote wa vyombo vya maamuzi ndani ya chama na Serikali. Azimio la kujivua gamba ndilo lilikuwa kifo cha Rostam kisiasa na kibiashara. Mali zake zikaanza kupukutika kiasi cha kuamua kukimbia nchi.
Sasa Rostam karejea nchini. Baada ya kurejea, mnamo tarehe 3 Mei 2015, alifanya kikao na baadhi ya maswahiba wake ambao ni wajumbe wa NEC. Kikao kilifanyika nyumbani kwake. Katika kikao hicho, walikubaliana kuwa kwa namna yoyote lazima Lowasa aingie Magogoni. Rostam aliahidi kutumia utajiri wake kuhakikisha kuwa mzee wa Mamvi anakuwa Mkuu wa Kaya kama alivyofanya kwa Jakaya mwaka 2005. alisikika pia akitamba kwamba yeye ndiye Rostam yule yule ambaye mbele yake hakuna wa kumzuia kufanya kile anachokitaka. Kwamba, ndani ya CCM hakuna mtu mwenye jeuri ya kuzuia harakati zake za kuhakikisha Lowasa anakuwa Rais kwa vile ana pesa ambazo zinaweza kutumika kufanikisha hilo.
Aidha, katika kikao hicho, waliazimia kuwa ikiwa Lowasa atakatwa kwenye mchujo wa kuwapata wagombea, watafanya moja ya mambo mawili. kwanza, wataanzisha vuguvugu la kutokuwa na imani na Sekretarieti iliyo chini ya Jakaya, Kinana, Mangula na wengineo. Hilo wakishindwa wamekubaliana kuwa wakiingia kwenye vikao vya maamuzi kama Kamati Kuu na Halmashauri kuu, wajumbe hao watasimama na kupiga kelele mithili ya wajumbe wa UKAWA ndani ya Bunge la Katiba na ikibidi wataweka mpira kwapani ili vikao visifanyike wakiamini kuwa kutoka kwao nje ya ukumbi wa mkutano kutasababisha akidi isipatikane.
Nimetafakari sana maamuzi haya ya Rostam na genge lake. Hakika imenishangaza sana. Yaani mtu ambaye ametopea kwa kila aina ya uchafu leo hii atuchagulie Rais Watanzania? Watanzania tumelogwa nini mpaka tumshobokee huyu singasinga ambaye utajiri wake unatokana na rasilimali tulizonazo na ameupata kwa njia ya kifisadi? Rostam ana uzalendo gani? Kama aliweza kukimbia nchi na kuhamishia shughuli zake Kenya na UAE, dhamira yake njema kwa watanzania ipo wapi?
Hata hivyo kwa watu wenye akili wanajua kilichomsukuma Rostam kurejea nchini na kumback up Lowasa. Rostam anamsaidia swahiba wake Lowasa kwa vile anaamini kuwa wamepiga deal za ufisadi kwa pamoja na kwamba ikiwa atafanikiwa kuingia magogoni, wataendelea kufanya ufisadi na hivyo kurejesha utajiri wake ambao umepukutika. Kwamba, fedha anazutmia kwa sasa kugharamia harakati za Lowasa kwenda magogoni zimepatikana kwa njia ya kifisadi na zitarejeshwa ndani ya muda mfupi ujao kwa njia ya kifisadi kama vile EPA, RICHMOND nk hasa ikizingatiwa kuwa tunaenda kwenye uchumi wa gesi. Ni ukweli usiopingika kwamba Rostam amerejea nchini kumsaidia swahiba wake Lowasa ambaye yupo hali mbaya kisiasa. Amekuja kutunyonya Watanzania kwa mara nyingine na akishatunyonya vya kutosha anatoweka nchini kama alivyofanya awali huku akitoroka na chumo lote.
Chonde chonde viongozi wangu wa CCM. Msitishike na nguvu ya pesa ya hawa mafisadi. Watanzania wana imani na nyie na nguvu ya Mungu haiwezi kushindana na nguvu ya mafisadi.
