Uchaguzi Marekani

Sw: Mieizi 6 iliyopita uliahidi kumuunga mkono mgombea wa GOP
JB: Cruz hapaswi kuniunga mkono, nina watu milioni 2 na delegates wengi
Simhitaji kufanya jambo asilotaka, nilimshinda Jeb Bush. Sihitaji watu wasiwe na furaha

Sijatendewa haki na RNC the establishment. Nilimsaidi mwezi wa mwisho wa kampeni Bw Romney
Alipokuja dhidi yangu, ninaleta mamilioni ya watu kwasababu yangu. Ratingya CNN leo ni excellent

Napenda GOP, mambo mabaya yamesemwa kwangu. Sitafanya kama Cruz alivyomtendea Carson
Nimemuangalia Cruz leo, ni kueleza sihitaji uungwaji mkono wake.

Sihataji Jeb, Ron, Walker, niliwashinda ndio maana wananichukia. Halazimiki kuniunga mkono

Sw'; kama kuna RNC convention utamuuunga mkono mtu kama Ryan
JB: Watu Wangi wananiunga mkono, nimeshinda Missouri

Luisiana, nimeenda na nina mahusiano mazuri na watu. Nilishinda uchaguzi, halafu nikisikia nimeshindwa. Hii ni siasa mbaya, nadhani mshindi ashinde

Sw: Unaweza kunipa mfano ulivyojifunza kitabia na unaweza kubadilika
JB: Unahitaji kuwa flexible kuingia mikataba ya uchumi. Kuna mengi nimefanya, nimebadilika kwa mengi, unaweza kusema ni pro life, original nilikuwa pro choice

Nimebadilika, hata Reagan alibadilika. Alisani sharia kali ya abortion na alikuwa conservative president

Sw; Ni lini uliomba radhi kama ulivyosema katika radio
JB: Siombi radhi bila sababu. Nimeomba msamaha kwa mama kwa lugha chafu.
Mke wangu aliyeniambia Donald kuwa presidential.

Sw: Viwanda vya maziwa vina changamoto za wafanyakazi. Kama hatuna sera nzuri za uhamiaji tutakuwa na tatizo. Unaweza kutupa sera zitakazoweza kutusaidia suala la wafanyakazi.
JB: Watu watakuwa na uwezo wa kuja kisheria. Kama una viwanda kama California na Wisconsin watakuja kwa program

Sw: Baba yangu amehamasika na watoto wako. Anasema kwanini Trump hawi kama watoto wake watulivu. Unaweza kuangalia watoto wako kama mfano
JB: Nina sifa kubwa sana kwa watoto wangu. Ivanka ni Star na anaiunga sana mkono

Watu wangu wanataka watoto wao wawe kama wangu.
 
TATHMINI YA MDAHALO

Tulipata tatizo la kifundi na kutowaletea ya Gav. Kasich. Tutachangia tukisonga mbele

Tuangalie tahmini nzima ya mdahalo. Ikumbukwe kuwa tulichowaletea ni sehemu muhimu za mdahalo zikaicha zile zenye majibishano au zisizo na mashiko kwa ujumla.

Ted Cruz
Kilichojitokeza kwa Cruz ni kushindwa kujibu maswali. Aliwashambulia Obama na Bi. Clinton bila uhusiano na swali. Hata alipotoa majibu, hakutoa kama mwenye kuelewa anataka kufanya nini. Mdahalo umeonyesha udhaifu mkubwa sana wa Seneta Cruz

Alishindwa jimbo alilotoka akisema kwake ni Florida badala yaTexas
Ni kosa dogo lililochangiwa na kuchanganyikiwa akijitahidi kutafuta majibu.

Alilitaja kundi la Muslim Brotherhood kama la Kigaidi. Katika orodha ya US halipo

Trump
Kama kawaida ilikuwa kujisifia. Alikwama ilipobidi kukubali kampeni inachangiwa.
Alisema ni 'peanut' kama milioni 6, lakini takwimu zingine zinasema ni 9.5M

Trump anaonekana kusimama na anachokiamini bila kujali kinaudhi au la
Hili linampa wafuasi, anaonekana japo kwa nje kuwa ni ''mwamainifu'' kwa anachosema.

Maswali ya ulinzi yalimweka pabaya na kulazimu kukana kauli zake za awali
Trump amekubali umuhimu wa NATO akibadili msimamo ifanyiwe marekebisho

Ameondoa kauli ya kuzuia Waislam na sasa anatumia Islamic terrorist
Kwa siasa za nje, Trump ni mtupu. Anajichanganya bila kuonyesha leadership
Ni kama mtu anayesikia habari tu, kiukweli hana details za ulinzi na usalama.

Gavana Kasich
Hakukumbwa na hoja za kashfa za matusi kama ilivyo kwa Cruz na Trump.
Kasich anafahamu anazungumzia nini. Ugavana ni hazina, kila anachozungumza hata kuudhi Republican ana uwezo wa kusimama na kulitetea

Gav anakwenda moja kwa moja katika swali, analifafanua na kulijibu akiwa na solution

Kilichoonekana ni mtu wa 'centre right' Haogopi kutetea misimamo hata kama ni sawa na nadharia ya Democrat. Ameunga mkono free trade, hoja za usalama kupinga patrol neighborhood za Waislam n.k

Gavana Kasich anaonekana 'presidential' na unaweza kuona tofauti kubwa sana kati ya uzoefu wake wa Gavana na akina Trump na Kasich.

Anaongea vitu vinavyoeleweka, mantiki na kama mtu anayejua matatizo katika maamuzi.

Inaendelea...
 
WAKATI MGUMU KWA REPUBLICAN

GOP wana wakati mgumu sana wa kumpata mgombea kwasababu kadhaa

Trump: Anaongoza kwa wajumbe na uwezakano wa kumzuai unapungua
Anatumia 'sensational info' kutia kiwewe, woga na matumaini yasiyoelezeka

Linapokuja suala la sera na details,Trump ana tatizo kubwa. Suala la Mataifa ni mweupe

Hana solution zinazoelezeka au zenye mantiki , solution zake zinahojiwa na zina utata
Kura za maoni anashindwa na Dem(Clinton na Sanders), ukweli unaohofiwa na GOP

Cruz
Hawezi kujibu hoja, hana facts na mwepesi wa kuchukua habari bila kuzifanyia utafiti
Anajipambanua kushambulia Obama/Clinton,sera hazionekani katika maisha ya watu

Ni kiongozi anyebadili misimamo, anataka watu wasikie anasema nini na kuwapendeza
Haielezeki ni mzuri katika siasa zipi,ndani haonekani kuzijua licha ya useneta, za nje anababaisha babisha.Ukimtazama utaona tatizo kubwa mbele ya safari.

Katika mijadala ya uchaguzi mkuu Cruz ana wakati mgumu sana wa kusimamia hoja zake akionekana mwongo mwongo 'liar'

Ni ngumu sana kumsoma na kuelewa ni kiongozi anayetaka nini na atakuwa wa aina gani
Katika kura, yupo nyuma ya Trump na nyuma ya wagombea wa Dem

Anaungwa mkono na 'the establishment' kama mbadala wa Trump

Kasich
Anavuta independent kwa kuwa 'centre right' haogopi kusema jambo hata kama halipendezi GOP. Haogopi kuunga mkono hata hoja za Dem.

Kwa Dem na GOP wasiopenda wagombea waliopo, Kasich ni chaguo lao kwanza
Lakini pia ana sifa za kuvuta GOP wa kati na kati, na Dem wa kati na kati

Kwa msingi huo, Gav Kasich katika kura za maoni kitaifa anawashinda Clinton na Sanders

Ana ufahamu mkubwa wa anachosema na anajua nini aseme kwa wakati gani na kwanini
Kasich ana wajumbe wachache, ushindi unategemea mkutano mkuu RNC ukiwepo

Ukiangalia hayo hapo juu utaona tatizo katika Republican.

Trump anawatia hofu kuhusu uwezo wake wa kushinda uchaguzi mkuu.
Wanatafuta njia za kumzuia kinamna.

Cruz haonekani kuwa mshindani, ni mbabaishaji anayetumia udhaifu kukwea ngazi
Ujenzi wake wa hoja ni hafifu, hana wajumbe wa kutosha. GOP wana hofu mbele ya Dem

Kasich:
Huyu ndiye anaonekana kama kweli mtu ambaye GOP wangemsimamisha na kushinda

Ana uwezo na sifa ambazo GOP hawakuziona kutokana na utitiri wa wagombea wengine wakipewa nafasi kwa 'charisma' kama Marco Rubio, Fiorina, Scot Walker n.k.

Hana nafasi ya kushinda uchaguzi unaoendelea. Ushindi utapatikana mkutano mkuu RNC

GOP wanajiuliza, nini wafanye ili aweze kufikia huko?
Wampaishe Cruz ili kumzuia Trump, au wamsaidie Kasich aendele kushinda huku Trump akipata namba kabla ya mkutano mkuu?

Wamwache Trump aendelee kuwa mgombea wakichukua risk nyingi au waingilie kati wakibeba risks nyingi pia?

Ndiyo maana tunasema Republican wana wakati mgumu

Tusemezane
 
WIKI MBAYA KWA TRUMP

ANAJICHANGANYA , 'WABAYA' WANAMSHIKA PABAYA

Haikuwa wiki nzuri kwa Trump katika kampeni.

Baada ya picha za mke wa Seneta Cruz zilizomletea mjadala na jamii ikihusisha wanawake, ameingia tena katika mzozo na wanawake

Trump anapigwa shinikizo la kumfukuza kazi kampeni meneja wake kwa 'tendo la kumpiga kabali' mwanadishi wa habari mwanadada wakati wanatembea.

Jana katika mdahalo Trump alimtetea Meneja wake, hali inazidi kuwa ngumu Meneja anapofunguliwa 'charge'

Leo akihojiwa, Trump amedai yeye ni pro-life,wanawake wenye kutoa mimba waadhibiwe

Hili limemletea tabu kwasababu mbili
1. Wapo wanawake wanaosema abortion ni hiari na haki yao.
Ni kutoka makundi yote ya jamii

2. Republican wanamkana Trump kuwa si pro life.
Wanasema conservatism ni pro-life na mwanamke na mtoto tumboni ni waathirika. Wanaopaswa kuadhibiwa ni wale wanaotenda siyo victims

Mzozo na akina mama ukiendelea, hoja za Trump kuhusu siasa za nje zinazidi kumwanika

Kuna mjadala mzito kuhusu NATO unaomshambulia Trump kuwa kauli haina maana

Lipo kundi linalohoji silaha la Nyuklia kama Trump alivyodai na kushindwa kutetea hoja

Na kundi la mwisho linahoji kuhusu biashara na kauli za Trump

kuna mtifuano mkubwa Wisconsin Jumanne ijayo.
Ni mtifuano ambao ungempa Trump nafasi nzuri sana ya kudhibiti wabaya wake.

Kura za maoni za baadhi ya taasisi zinaonyesha akiwa nyuma ya Cruz kwa point 10

Ushindi wa Cruz utaongeza nguvu kwa 'the establishment' wakati wa kwenda mbele.

Haijaeleweka kauli zake ndizo zinamshusha au ni mazingira ya kisiasa baada ya kumsoma

Kitu kilicho wazi , makundi ya wanawake, Trump anakubalika katika asilimia chini ya 30

Wakati huu anapata kipigo cha Republican na Democrat hali yake haikuwa nzuri kisiasa

Ni wiki mbovu kwake na matokeo ya Wisconsin yataeleza Zaidi

Tusemezane
 
TRUMP ASHAMBULIWA NA WANADIPLOMASIA WASOMI

VITA YA DEMOCRAT , WISCONSIN NA NEW YORK

Baada ya wiki mbaya kisiasa, Trump amekutana na kiongozi wa RNC Bw Priebus kuzungumzia suala la wajumbe wenye utata hasa wa Luisiana.
Hili ni ujanja wa kubadili mwelekeo wa mazungumzo yanayomweka pagumu sana.

Leo amekutana na timu yake ya washauri wa mambo ya nje, kabla ya kukutana Priebus

Wasomi wamemosoa Trump kuhusu silaha za Nyuklia (Nuclear proliferations).
Waanauleza msimamo wa Trump kama ukosefu na uzoefu wa masuala ya kimatifa.

Upande wa pili, mjadala wa abortion unaendelea, kampeni meneja kuleta mtafarufuku
Wengi wanahoji hoja za Trump kama Rais na kuingiwa na uwezo, na utayari kuwa Rais

Japan na Korea kusini kwa pamoja zimemjibu na kutoridhishwa na Trump na huenda ikapelekea mtafaruku wa kidipmomasia ''Diplomatic row''

Nchi hizo zinaonekana kukerwa na kauli za Trump, Korea ikisema msaada wa Marekani ni 'peanut' Kauli inayoonyesha kuchukizwa

The establishment walikuwa wanamtafutia sababu, kwa bahati nzuri au mbaya, mdomo wa Trump umewapa walichotaka.

Hoja yao sasa ni kuwa Trump anaharibu misingi ya conservative, hana uzoefu wa mambo ya Kimataifa kama kiongozi wa Taifa ongozi duniani.

Lakini pia wanatumia namba kuonyesha asivyiokubalika. Katika kundi la wanawake, kila siku kura za maoni zinaonyesha akididimia. Katika kiwango cha asilimia 30, Republican atashindaje mbele ya Dem?

Wanachokitaka ni Trump kuwa na idadi chache au akiwa na wajumbe asifikie 1237.

Pengine awe na 50 au 100 chini ya hapo ili waende mkutano mkuu wa RNC watakapommaliza

GOP establishment wamejikusanya Wisconsin kukampeni kwa Cruz.

Kura za maoni zinaonyesha Trump akiwa 32 na Cruz 42.
Kupoteza Wsiconsin alikokuwa anaongoza kwa kura za maoni ni pigo kwake

Wakati yakiendelea, Democrat wapo katika mtifauno mkubwa.
Inaonekana hali ya kucharurana imeanza.

Kuna majimbo mawili yenye umuhimu tofauti, Wisconsin na New York

Tutajadili bandiko lijalo
 
WISCONSIN NA NEW YORK-DEMOCRAT

Jumanne kutakuwa na primary ya Wisconsin. Jimbo lenye takribani wajumbe 90

Kura za maoni zinaonyesha Bw. Sanders akiwa mbele ya Bi.Clinton kwa point 5
Zingine zikionyesha kufungana katika kile wanachokita 'statistical tie'

Kwa mchuano ulivyo, kura za maoni hazielezi hali halisi Zaidi ya kutoa picha ya jumla

Haikutarajiwa Sanders kushinda Michigan, na Washintong state kwa kutazama kura

Tunaona kukaribiana katika 45%-55%. Hii ina maana kugawana wajumbe kuna wezekana. Lakini Wisconsin ina umhimu kwa wagombe kwa maana zifuatazo

Bw Sanders anataka kuendeleza ushindi ili kujenga hoja ya kushinda hata kama ni 0.5.

Anachojenga sasa ni hoja kuwa anakubalika ili kuvuta super delegates
Kwa Bw Snaders matokeo ya 45-55 hayana maana yoyote kuziba pengo la wajumbe

Anachotaka ni kusikika ameshinda, ajenge hoja ya jumla' kusogeza uchaguzi mbele

Kwa Bi. Clinton, anataka kuzuia Sanders alisiendelee na kauli kushinda
Anataka kutumia fursa za Primary kuonyesha anamudu chaguzi katika upana na si caucus

Naye kama mwenzake ushindi au kushindwa katika 45-55% hakumuathiri katika wajumbe. Katika margin error ya 5, hapotezi wajumbe, lakini ananmpa Sanders kauli

TUANGALIE DYNAMICS NDANI YA DEMOCRAT

Yapo maswali kuhusu mwenendo wa uchaguzi ndani ya Dem.
Kwanini Bi. Clinton anapoteza chaguzi za Caucus, Sanders ana momentum

Zipo nadharia kadhaa kuhusu hali iliyopo. Kwanza, ni kujulikana na rekodi kuwa wazi

Sanders: Hajatokea katika mambo ya kitaifa au kimataifa.
Rekodi yake haipo wazi, wengi hawamjui na hivyo kumshambulia inakuwa jambo gumu.

Bi. Clinton: Kama Sanders, amekuwa seneta, first lady wa Gavana wa Arkans, First Lady wa US, Mgombea Urais wa Marekani na secretary of state katika utawala wa Obama

Rekodi yake ipo wazi kuliko , na hushambuliwa kwa urahisi sana
Bi Clinton anapata mashambulizi kutoka kwa Sanders na Republican kwa ujumla

Inaendelea....
 
DYNAMICS ZA DEM

Nadharia
Pili, utaratibu wa kuchagua

Kwa Dem kuna aina Zaidi ya tatu za aina ya uchaguzi na wapiga kura.
Moja, wapiga kura waliojiandikisha wa Dem.
Mbili, wapiga kura wasio na vyama wanaoweza kushiriki (Independents)

Cahguzi ni caucus , primaries kwa waliojiandikisha, primaries kwa independents .

Kwa mwenendo ulivyo, Sanders anashinda chaguzi za wazi zinazojumuisha independents

Independents wanaweza kuwa wasio na vyama bali mgombea, au ni wanachama wa Republican wanaompendelea mgombe wa Dem.

Pia, independents, wapo wanaopiga kura kwa lengo la kuunga mkono au kudhoofisha

Kwa mfano, katika chaguzi ambazo mgombea wa Republican anaweza kuona Kikwazo, watu wake wanaweza kupiga kura kama independents ili kumdhoofisha 'mbaya' wao

Haieleweki kwa uhalisia kama independents wanaomuunga Sanders kwa wingi ni Democrat au ni Republicana pengine wakita kumdhoofisha Bi. Clinton. Bado ni kitendawili

Nadharia ya tatu ni mchanganyiko (Diversity)

Sanders anaonekana kukubalika na weupe Zaidi na anapata tabu kwa watu wa rangi
Majimbo yenye watu wa rangi kama Luisiana, Florida n.k. ameshindwa kwa % kubwa

Bi. Clinton anaonekana kukubalika katika majimbo ya watu wa rangi na weupe
Tatizo lake ni wapiga kura, wanawake hawamuungi mkono kwa wingi, wala vijana wa 20-30

Bwana Sanders anatatizika na majimbo ya watu wa rangi.
Amepoteza chaguzi maeneo yenye watu wa rangi na Bi.Clinton anapoteza za weupe

Nadharia hizo ndizo zinajenga mtifuano kati ya April Wisconsin na April 19 New York

Wagombea walikuwa New York licha ya mtinange Jumanne.
New York ina wajumbe takribani 250

Tofauti ya asilimia chache za ushindi ina athari sana kwa wajumbe. Kwa mfano, 45-55%

Bw. Sanders ni mzaliwa wa kitongoji cha Brooklyn , NY wakati Bi Clinton ni seneta mstaafu wa NY

Uchaguzi wa NY ni wa wapiga kura waliojiandikisha ilipofika March 25
Hakuruhusiwi independent kujiandikisha mfupi kabla ya kura katika majimbo mengine

Ni kwa mantiki hiyo, Wisconsin na NY ndizo zitaamua urefu wa uchaguzi wa Dem kama tutakvyojaribu kufafanua bandiko linalofuata
 
WISCONSIN & NY CITY

Tumegusia umuhimu wa Wisconsin katika uchaguzi ujao wa Dem na hali za Wagombe
'Cheese state' itatengeneza ramani ambayo NY city itaamua mwenendo wa uchaguzi

Kinadharia, kama bI. Clinton atashinda hata kwa 0.1 point, atakuwa amepunguza kasia ya Sanders. Akishinda NY kwa kiasi hicho hicho, Sanders itabidi abwage Manyanga.

Majimbo yaliybaki itabidi Sanders ashinde kwa asilimia 70 ikiwemo California yenye wajumbe Zaidi ya 300. Ni jambo gumu

Ikiwa Sanders atashinda Wisconsin, kauli mbiu yake ya Wajumbe 'super delegates' waangalie uwezekano wa kumuunga mkono itakuwa na mashiko.

Sanders akishinda WS na NY, uchaguzi lazima utaenda June, California iamue mshindi

Macho yetu yapo Madison, mji mkuu wa Wisconsin.
Wapenzi wa NBA Milwaukee Bucks inatoka mji maarufu wa Milwaukee!

NEW YORK
Hapa kipo kitim tim, kwamba wagombea waliitosa Wisconsin kwa muda kuweka mambo sawa NY. Umuhimu wake ni wajumbe , diversity na kitu kinachoitwa 'swing states'

Kabla hatujaongelea Swing states, kidesturi Wisconsin inaegemea Dem-uchaguzi mkuu.
Kwa sasa inaongozwa na gav. wa GOP ,Scot Walker aliyejitosa Urais na kujitosa nje

Mshindi wa jimbo kwa Dem, atarudisha Imani ya kulirudisha jimbo linalobadilika

Kubadilika kwa majimbo, tutajadili kinachoitwa 'swing sates' ambapo NY ni mojawapo

Swing(bembea) inaweza nkwenda kulianau kushoto. Hivyo swing sates zina maana majimbo yanayobadilika katika uchaguzi mkuu. Kwanini inakuwa hivi?

Kwa desturi kuna Red and Blue states. Red ikiwalikilisha Republican na Blue ikiwa Dem

Kinachoangaliwa ni jinsi majimbo yanavyochagua Rais katika mfululizo wa chaguzi

Yapo majimbo yanayoitwa 'purple states' haya kwa lugha yao ni 'toss up' (sandakarawe)

Swing sates hazitabiriki zitampigia nani kura uchaguzi mkuu na huamua 270 kati ya 538

Ili kushinda Urais lazima mgombea apate viti 270. Kutokana na desturi ya upigaji kura, Democrat wanajua states zinazowapigia kura, huhesabu viti '226',Republican viti '206'

Ili kufikia namba 270 ya Urais, swing sates na purple states ndizo zinaamua kwa uhalisia.
Inapotokea mgombea akapoteza ima Red au Blue, hayo ni maafa. Akipata ni neema

Tunajua dhana ni ngumu kueleweka. Kuna maswali , inakuwaje Dem wana viti '220' na GOP '206' kabla ya uchaguzi?

Na kwamba mbona 220+206 ni Zaidi ya 270 ya Urais? Ile 538 inaeleza nini?
Hizi namba zinakuwaje na zinapatika viti?

Maswali hayo pamoja na mifano rahisi ya kuelewea inafuata bandiko lijalo

Itaendelea?
 
WISCONSIN & NY CITY

Tumegusia umuhimu wa Wisconsin katika uchaguzi ujao wa Dem na hali za Wagombe
'Cheese state' itatengeneza ramani ambayo NY city itaikamilisha kuamua mwenendo wa uchaguzi

Kamanda, unamaanisha New York city au state of New York?

Katika kubadilika kwa majimbo, tutajadili kinachoitwa 'swing sates' ambapo NY ni mojawapo

NY ni swing state? Kwenye uchaguzi mkuu ama?

Manake nijuavyo mimi NY ni solid blue state.

Na kwa zaidi ya miaka 30 hakuna mgombea wa GOP aliyewahi kushinda.

GOPer wa mwisho kushinda NY alikuwa Ronald Reagan, mwaka 1984 ambapo alishinda majimbo 49 kati ya 50.
 
Kamanda, unamaanisha New York city au state of New York? NY ni swing state? Kwenye uchaguzi mkuu ama?Manake nijuavyo mimi NY ni solid blue state.Na kwa zaidi ya miaka 30 hakuna mgombea wa GOP aliyewahi kushinda.

GOPer wa mwisho kushinda NY alikuwa Ronald Reagan, mwaka 1984 ambapo alishinda majimbo 49 kati ya 50.
Mkuu upo sahihi kuhusu NY city na NY state.

'Historically' NY state ni swing, kama ulivyosma miaka takribani 30 ni solid Blue
Historia ya magavana inaonyesha kulalia Dem ingawa zipo nyakati Republican waliwahi kuongoza
Kwa NY City miaka ya karibuni, mameya kama Gulian na Bloomberg ni Republican

GOP wa mwisho kushinda alikuwa Reagan, na wakati huo kama sikosei, Blue state nyingine ya Michigan ilipobadilika na kuitwa Blue Republican
 
Mkuu upo sahihi kuhusu NY city na NY state.

'Historically' NY state ni swing, kama ulivyosma miaka takribani 30 ni solid Blue
Historia ya magavana inaonyesha kulalia Dem ingawa zipo nyakati Republican waliwahi kuongoza
Kwa NY City miaka ya karibuni, akina Gulian na Bloomberg wametoka Republican

GOP wa mwisho kushinda alikuwa Reagan, na wakati huo kama sikosei, Blue state nyingine ya Michigan ilipobadilika na kuitwa Blue Republican

Nimekupata.

Ila, kwenye political spectrum ya Marekani kumbuka kuwa GOP wengi wa NYC ni centrists/ moderates.

Kwa mfano, hao uliowataja [Giuliani na Bloomberg; na hata George Pataki] wote ni pro--choice ikija kwenye suala la abortion ingawa Pataki nadhani ana vi-exceptions vyake na pia ni pro gay rights.

Na ndo maana walishinda chaguzi kwenye hilo jimbo. Huyo Bloomberg mwenyewe alikuwa Democract hadi mwaka 2001 alipobadili vyama na kuwa Republican. Mwaka 2007 akaondoka GOP na kuwa independent!

Hata Trump mwenyewe siyo conservative kivile.

La sivyo, conservatives kama Jeff Sessions, Tom Coburn, Nathan Deal, na wengineo, kushinda NY state na NYC ni ndoto.

Katika swing states NY haipo kabisa maana yenyewe ni solid blue state.

Angalia hata uone hata electoral college ratings za Centerforpolitics.org uone NY ilipo.

Ni 'safe' Democratic state.

2016_03_31_pres_600.png


The Crystal Ball‘s 2016 Electoral College ratings (for Hillary Clinton vs. Donald Trump)
 
''BATTLE GROUND ''
KWANINI NEW YORK KWA UPANDE WA DEM?

Kama tulivyosema idadi ya wajumbe ni kubwa, historia za wagombea mmoja akiwa senata na mwingine mzaliwa wa Brooklyn zina mchango.
Vita ya Dem ipo New York ingawa kibwagizo cha awali ni Wisconsin.

NY ni uwanja wa vita kwa Dem, Bi. Clinton akipoteza itamuathiri kisaikolojia
Bw Sanders akishinda, itampa momentum kujenga hoja ya super delegates

Bi. Clinton akishinda itampa nguvu. Kwa mfano ushindi wa 0.1 utagawa wajumbe, hilo ni kikwazo kwa Sanders anayetaka kupata wajumbe, na NY idadi ni muhimu kwake.
NY inaweza kuhitisha safari ya Sanders kama Bi Clinton atafanya vema

Ushindi wa 55 kwa 45 utakata idadi kubwa ya wajumbe aliopata Sanders Washinton state, Idaho na Utah. Sanders akishinda katika kiwango hicho, atapunguza pengo la wajumbe kati yake na Bi Clinton.

Sanders aliposhinda Michigan alisema, hilo ni jimbo kubwa na muhimu na ushindi NY utazshadidia kauli yake. Ni mtihani kwa Sanders endapo ana uwezo wa kushinda 'diverse' population na primaries zenye registered voters zisizotoa nafasi ya independent

NY inatazamwa kama safe state na Dem katika uchaguzi mkuu. Mgombea atakayeweza kuaminisha super delagtes safe state zipo salama ana nafasi ya kuwashawishi

Kitim tim kitahamia katika Swing states, ambazo uchaguzi mkuu huitwa 'Battle ground'

Ni kutokana na umuhimu wake kufikia namba 270 inayomchaguza Rais wa Marekani
270 inatoka katika wajumbe 538.

Ukigawa namba hiyo kwa mbili utapa 269 hakutakuwa na mshindi

Hivyo anayepata 270 ni mshindi. Ikitokea wamefungana au kuwepo kwa chama cha 3, utaratibu upo. Tahadhari tu, upo hakuna mauza uza ya kufuta uchaguzi (Jechasim)

Kwa namba 270 ya viti, Dem wanaingia uchaguzi mkuu wakiwa na takribani 220 , Republican 206. Maana yake ni kuwa , katika Red states na zile zinazoegemea Rep, wanatarajia kupata 206. Na Democrat nao wana hesabu hizo hizo '220'

Kinachoamua tofauti ya 220 na 206 kufikia 270 ni zile swing sates na ndio maana zinaitwa battle ground.

Kwa maneno mengine, kila chama kinaingia uchaguzi mkuu kikiwa na mtaji( 220,206)
Kinachoongeza mtaji au kupunguza ni majimbo yanayobadilika na yale yasiyotabirika(toss up)

Inaendelea....
 
Nimekupata.

Ila, kwenye political spectrum ya Marekani kumbuka kuwa GOP wengi wa NYC ni centrists/ moderates.

Kwa mfano, hao uliowataja [Giuliani na Bloomberg; na hata George Pataki] wote ni pro--choice ikija kwenye suala la abortion ingawa Pataki nadhani ana vi-exceptions vyake na pia ni pro gay rights.

Na ndo maana walishinda chaguzi kwenye hilo jimbo. Huyo Bloomberg mwenyewe alikuwa Democract hadi mwaka 2001 alipobadili vyama na kuwa Republican. Mwaka 2007 akaondoka GOP na kuwa independent!

Hata Trump mwenyewe siyo conservative kivile.

La sivyo, conservatives kama Jeff Sessions, Tom Coburn, Nathan Deal, na wengineo, kushinda NY state na NYC ni ndoto.

Katika swing states NY haipo kabisa maana yenyewe ni solid blue state.

Angalia hata uone hata electoral college ratings za Centerforpolitics.org uone NY ilipo.

Ni 'safe' Democratic state.

2016_03_31_pres_600.png


The Crystal Ball‘s 2016 Electoral College ratings (for Hillary Clinton vs. Donald Trump)
NY ile conservative ya 'evangelica'l ni ngumu. Inabidi wawe centrist

Kama ulivyosema, uzalendo ulimshinda Bloomberg mara 3.
Hata hivyo, alipokuwa independent bado alishinda kuonyesha NY ilivyo na utata

Hii ramani inaonyesha namna viti 270 vinavyopatikana uchaguzi mkuu

Utaona kwa wakati huo hakukuwa na ' toss up' states. Hizi hutokea kutokana na ngvu za wagiombea

Kuna nayakati majimbo yanakuwa hayana 'majority' katika kuunga mkono vyama ni ngumu kujua jimbo linaenda wapi bila kujadili huegemea upande gani

Lakini pia ramani inaeleza kwanini popular vote pekee haiwezi kumpa ushindi mhusika

Mfano, Utah ina wajumbe 4 , Washington state 12 , Idaho 4 kwa jumla ya wajumbe 20

Majimbo haya kwa upande wa uchaguzi wa ndani unaonedelea Sanders kashinda yote

Florida, lina wajumbe 29 peke yake, Illinoi 20 peke yake.

Ikifika wakati wa kujenga hoja wajumbe wataangalia hoja kwa mitazamo hii
Sanders: Kwa mfano wa wiki moja iliyopita alishinda majimbo 3, Utah, Idaho, Washington

Utah na Idaho ni majibo ya Republican tena yenye viti 8. Ushindi huo umeeleza nini ktk uchaguzi mkuu? Je, independents kutoka maeneo hayo wapo likely kubadilisha rangi ya jimbo?

Hoja ya Sanders itakuwa, ameshinda jimbo la Washington lenye viti 12 likiwa ni 'safe' kwa Dem
Hii ni pamoja na Michigan na NH inayoegemea Dem, kwamba ana uwezo wa kuyalinda

Hoja ya Bi. Clinton ni kuwa ameshinda Florida, ataweza kuitetea ikiwa na viti 29.
Ameshinda Illinoi anaweza kuitetea ikiwa na viti 20

Mifano hiyo ni kuonyesha jinsi gani super delegates wanavyoangalia wagombea na kufanya ''projections'' nini kitatokea siku za mbeleni kabla ya kuwaunga mkono.

Kwa upande wa Republican, hali ikoje?

.....inaendelea
 
KWA REPUBLICAN

IKulekea Wisconasin wiki haikuwa nzuri kwa front runner Trump
Kashfa ya Maneja wake, Abortion na Nuclear proliferation hayakusaidia hali

Seneta Cruza anasaidiwa na 'the establishment' kumzuia Trump Wisconsin
Mahusiano ya Seneta Cruza na 'the establishment' yana utata.
Seneta Cruz hakubaliki miongoni mwao kwa namna anavyokabiliana nao katika Seneti
Imekuwepo mikwaruzano iisyo ya lazima, kwa sasa ndiye kikwazo pekee kwa Trump

Gavana Kasich naye kasema suluhu itapatikana katika mkutano mkuu wa RNC
Anasema kura za maoni zinaonyesha amemshinda Bi. Clinton kitaifa

Hoja ya Gav Kasich ni mchakato uende mkutano mkuu,atakutana na Cruz na Trump

Mategemeo yake ni kutumia umaarufu wa siku chache na kura za maoni anaweza kuwashwaishi wajumbe yeye pekee ndiye anaweza kumshinda Bi.Clinton

Trump anasema ' akikatwa' hajaondoa uwezekano wa kushiriki akiwa mgombea binafsi

HALI ILIVYO SASA HIVI

Jitihada za kumkwamisha Trump zinaendelea zikifanywa na 'the establishment'
Ikifanikiwa, ndani ya mkutano mkuu wa Republican kutatokea mengine yasiyotarajiwa

1. Trump ataondolewa, na kuudhi kundi la watu wake ambao kiasilimia si dogo
2. The establishment' watagawanyika kati ya Cruz na Kasich
3. Kumuondoa Cruz akiwa na wajumbe wengi kuliko Kasich itazua mtafaruku
4. Kasich atasimama na hoja ya kushinda Democrat ndiye awe chaguo

Katika mazingira hayo, hakuna hatua inayochukuliwa na RNC kwasasa yenye afadhali

Kila hatua ina gharama zake, na kuelekea uchaguzi mkuu, mshindi atakuwa na kazi mbili

1. Kuunganisha chama kitakachokuwa vipande vipande
2. Kukabiliana na mgombea wa Dem

Hali ni tete kwa Republican

Tusemezane
 
KWA REPUBLICAN

IKulekea Wisconasin wiki haikuwa nzuri kwa front runner Trump
Kashfa ya Maneja wake, Abortion na Nuclear proliferation hayakusaidia hali

Seneta Cruza anasaidiwa na 'the establishment' kumzuia Trump Wisconsin
Mahusiano ya Seneta Cruza na 'the establishment' yana utata.
Seneta Cruz hakubaliki miongoni mwao kwa namna anavyokabiliana nao katika Seneti
Imekuwepo mikwaruzano iisyo ya lazima, kwa sasa ndiye kikwazo pekee kwa Trump

Gavana Kasich naye kasema suluhu itapatikana katika mkutano mkuu wa RNC
Anasema kura za maoni zinaonyesha amemshinda Bi. Clinton kitaifa

Hoja ya Gav Kasich ni mchakato uende mkutano mkuu,atakutana na Cruz na Trump

Mategemeo yake ni kutumia umaarufu wa siku chache na kura za maoni anaweza kuwashwaishi wajumbe yeye pekee ndiye anaweza kumshinda Bi.Clinton

Trump anasema ' akikatwa' hajaondoa uwezekano wa kushiriki akiwa mgombea binafsi

HALI ILIVYO SASA HIVI

Jitihada za kumkwamisha Trump zinaendelea zikifanywa na 'the establishment'
Ikifanikiwa, ndani ya mkutano mkuu wa Republican kutatokea mengine yasiyotarajiwa

1. Trump ataondolewa, na kuudhi kundi la watu wake ambao kiasilimia si dogo
2. The establishment' watagawanyika kati ya Cruz na Kasich
3. Kumuondoa Cruz akiwa na wajumbe wengi kuliko Kasich itazua mtafaruku
4. Kasich atasimama na hoja ya kushinda Democrat ndiye awe chaguo

Katika mazingira hayo, hakuna hatua inayochukuliwa na RNC kwasasa yenye afadhali

Kila hatua ina gharama zake, na kuelekea uchaguzi mkuu, mshindi atakuwa na kazi mbili

1. Kuunganisha chama kitakachokuwa vipande vipande
2. Kukabiliana na mgombea wa Dem

Hali ni tete kwa Republican

Tusemezane
Nguruvi3, nadhani kuna kitu kinafaa kuwekwa sawa nalo ni kwamba hakuna mtu anaondolewa hivi hivi na Trump hawezi kuondolewa hivi hivi. Tunaposema kuna juhudi za kumuondoa Trump nafikiri si sahihi...Trump ataweza kuondolewa tu kama atashindwa kupata idadi ya wajumbe inayotakiwa. Lakini akiweza kufikisha wajumbe 1,237 kabla ya convention au kwenye convention, hakuna atakayemuondoa na hapo mgombea wa GOP atakuwa Trump watake wasitake.

Hilo ni moja, la pili ni Kwamba Trump kama atafaulu kupata idadi tosha ya wajumbe, establishment ya GOP italazimika kumuunga mkono. Wanaweza wakatokea wajumbe wasimuunge mkono lakini hii itakuwa on individual basis lakini kama chama GOP itakuwa nyuma yake. Inaposemwa kuna jitihada za kumuondoa naamini hii si sawa, ni yeye pekee anaweza kujikwamisha kwa kushindwa kufikisha idadi ya wajumbe wanaotakiwa ambayo ni wajumbe 1237, period.
 
Nguruvi3, nadhani kuna kitu kinafaa kuwekwa sawa nalo ni kwamba hakuna mtu anaondolewa hivi hivi na Trump hawezi kuondolewa hivi hivi. Tunaposema kuna juhudi za kumuondoa Trump nafikiri si sahihi...Trump ataweza kuondolewa tu kama atashindwa kupata idadi ya wajumbe inayotakiwa. Lakini akiweza kufikisha wajumbe 1,237 kabla ya convention au kwenye convention, hakuna atakayemuondoa na hapo mgombea wa GOP atakuwa Trump watake wasitake.

Hilo ni moja, la pili ni Kwamba Trump kama atafaulu kupata idadi tosha ya wajumbe, establishment ya GOP italazimika kumuunga mkono. Wanaweza wakatokea wajumbe wasimuunge mkono lakini hii itakuwa on individual basis lakini kama chama GOP itakuwa nyuma yake. Inaposemwa kuna jitihada za kumuondoa naamini hii si sawa, ni yeye pekee anaweza kujikwamisha kwa kushindwa kufikisha idadi ya wajumbe wanaotakiwa ambayo ni wajumbe 1237, period.
Mkuu Maga3 ahsante kwa hili. Ningeomba kuliongelea kidogo.

Katika mabndiko tumesema 'magic number ni 1237' na kwamba anayefikisha hiyo ndiye mgombea Republicana, na kwa Dem ni 2000+, ndio msingi wa kuongelea wajumbe wa aina zote kutoka pande zote

Kuna ukweli 'the establishment' hawakubaliani naye. Endorsement alizopata hadi sasa akiwa front runner, Ben Carson, Christie Christie ambao wanaangalia mbele.

Akiwa front runner pengine angeshapata endorsement kubwa. Kwanini haitokei?

'Establishment' wamepiga kambi Wisconsin wakijua ushindi wa Trump ndio basi tena
Wanafahamu kuelekea mashariki kumzuia itakuwa ngumu.

Kwamba kuna sentiment dhidi ya Trump hilo lipo wazi
Kuhusu kumuunga mkono, chama kitamuunga mkono.
Tatizo litalkalotokea ni baadahi kama ulivyosema kumsusia.

Tunakumbuka Mike Huckabee alivyomsusia Mitt Romney kiaina.
Kutakuwa na 'slow go' miongoni mwa watu wenye ushawishi

Watamzuia kwa kuamuru,haiwezekani.
Kwamba,kuna jitihada za kutekeleza hilo kichini chini zipo

Ukiangalia hata Political pundits wamenywea hasa suala la nuclear proliferations alivyo li-handle . Wameshindwa kufanya 'spnning ' katika mazonge zonge ya wiki hii ikonyesha kama vile 'wamesusa'
 
WISCONSI LEO
Tutawaletea kila kinachojiri kuanzia jioni ya leo hadi matokeo ya mwisho

Wagombea walikuwa Wisconsin, Trump akiwa karibu na mkutano wa Sanders

Gavana wa Wisconsin Scott Walker ameonekana akifanya kampeni kwa Cruz sambamba na Carl Fiorina aliyekuwa mwanamke pekee katika kinyang'anyiro

Gavana Kasich naye alikuwa katika kampeni, wakati Bi. Clinton alikuwa New York

Bi. Clinton haieleweki kwanini amekomalia NY ambako ana point takribani 8 mbele ya Sanders. Ilitarajiwa angekuwa Wisconsin

Pengine ni kutambua Wisconsin uchaguzi upo karibu sana na kwamba tofauti itakuwa ndogo ashinde au ashindwe na haina athari kwa wajumbe.

Hata hivyo, Sanders akishinda itakuwa na athari kwa Bi Clinton kwani ataendelea na kauli mbiu ya ushindi kuelekea NY

Inawezekana Bi. Clinton ameona uwezekano wa kushinda ni mdogo na asipoteze muda

Sanders anaonekana kujiamini akisema mazingira ya Wisconsin hayatofautiana na Michigan

Au, Bi Clinton ameona ukaribu wa kura unaweza kumpa ushindi

Kinachoonekana ,amekamia NY kwa mkakati, kwamba anataka ushindi mkubwa utakaompa nafasi akitumaini hatapoteza wajumbe wengi Wisconsin

Wote wawili wamekubaliana kuwa na mdahalo April 14, mdahalo unaonekana utakuwa na timbwili kubwa kutokana na kauli zinazoanza kujitokeza kwa sasa (Rhetoric)

Tutawahabarisha kinachoendelea nyumbani kwa Milwaukee Bucks tukielekea NY Nicks

Tusemezane
 
WISCONSIN MATOKEO

Kama ilivyotarajiwa mshindi wa Republican ni Cruz. Ni baada ya wiki mbaya sana ya Trump, na nguvu ya 'the establishment' wakiongozwa na gavana Scott Walker

Namba kamili hazijapatikana kwa pande zote, Democrat na Republican washindi watakuwa ni Cruz kwa Republican na Bernie Sanders kwa Dem

Ushindi wa Cruz umefanikiwa kwa kiasi kuzuia kasi ya Trump
Kwa maneno mengine wastani wa kushinda Trump umekwenda juu badala ya chini

Kwa upande wa Democrat mshindi ni Sanders kama ilivyotarajiwa
Tutakapopata namba kamili tutawaletea wajumbe watakavyogawanywa

Kwasasa Sanders anaongea. Jana alipokuwa Wisconsin aligusia black America katika hotuba kuashiria safari ya NY.

Kwa mara ya kwanza katika kampeni, amemsifia Rais Obama kwa Obamacare. Hili nalo linaonyesha safari ya NY na kutaka kuungwa mkono na jamii za watu wa rangi

NY ni mchanganyiko wa Raia. Hadi sasa kura za maoni zinaonyesha Hillary Clinton akiwa na point 8 mbele. Sanders ni mzaliwa wa Brooklyn kiasi hicho si cha matumaini.

Clinton anawekeza sana NY kwenye wajumbe Zaidi ya 250.
Haifahamiki ni hofu ya kupoteza NY kwa Sanders au ni kutaka kutoa pigo la nguvu

Advantage aliyo nayo ni kuwa NY ni kwa registered democrat.
Sanders, registration zikifungwa March 25, alijitahidi kuandikisha. Namba inatosha?

Pili, Clinton akiwa seneta bado ana mtandao katika eneo hilo
Tatu, kuna vitongoji vya watu wa rangi ambavyo Clinton anafasi kubwa

Haieleweki kama Clinton kampeni ime panic, au inajiandaa kwa pigo kuu, haieleweki

Tatizo linalomkabili si idadi ya wajumbe.Katika tofauti iliyopo ni ngumu kwa Sanders

Anachokisema ni kuwa ameshinda majimbo 7 katika 8 hata kama ni majimbo baadhi yakiwa (Red state) ambayo impact yake katika uchaguzi mkuu si kubwa.
Hata hivyo katika primaries na Caucus hesabu inabaki kuwa ameshinda

Hiyo kauli anapokwenda nayo ndiyo mwiba kwa Bi. Clinton. Kwa wajumbe wanaobadilika, siku zijazo tutaona wakiongezeka kwa Sanders, na ameshaanza kuwaomba waangalie uwezekano huo asubuhi hii

Bado njia ya kufikia wajumbe 2000+ ni ngumu lakini anajenga hoja ambayo kwa namba inaweza kusomeka vizuri kwa upande wake kama Clinton ataendelea kudorora

Tutaendelea
 
HALI ILIVYO HADI SASA

Matokeo ya Wisconsin kwa GOP tuliyaeleza siyo 'winner take all' ni ''winner take most'
Tofauti ya hizo hali mbili tumezieleza huko nyuma

Cruz ameshinda districts nyingi na kupata wajumbe trakribani 33, Trump 3 na Kasich 0

Hesabu za kufikia magic number 1,237 Trump lazima ashinde majimbo yaliyobaki wastani wa 62%. Bandiko lililopita tumeeleza wastani wake umeongeza, kwa maana angeshinda leo wastani anaotakiwa kufikia ungekuwa 55(ungepungua)

Cruz ameshinda baada ya 'endorsement' za J.Bush, Carl Fiorina, S Walker baadhi walipiga kambi Wisconsin. Ili kufikia 1,237 ni lazima ashinde 92% ya majimbo yaliyobaki !!!

Swali, ni kwanini 'the establishment' wanampigia kampeni Cruz licha ya ugumu huo ?

Jibu: wanachotaka ni kumzuia Trump kiufundi ili waende mkutano mkuu(RNC)
Hilo wameanza kufanikiwa kwa asilimia nyingi. Uwezekano ni mkubwa sana

Kwa majimbo yaliyobaki kama NY, California n.k. ambako Trump anawakati mgumu kutokana na mahusiano yake na jamii za maeneo hayo, ushindi ni mgumu

Kwanini Gavana Kasich anaendelea na kampeni akipigwa vibaya kila mahali?

Jibu: Mkutano mkuu, kwamba anategemea uchaguzi uende RNC
Anatambua miongoni wa wajumbe hawamtaki Trump , lakini wapo ''wasiompenda Cruz''

Hapa tusisitize kuwa Cruz si chaguo la 'wazee' lakini mazingira waliyo nayo 'the establishment' ina walazimu

Kasich anayeonekana kuja juu katika lala salama , anatumaini kuwa mbadala wa wawili
Na kwavile dalili za kwenda RNC zinaongeza, Kasich haonekani kama ataachia ngazi

Tatizo linalomkabili Trump wakati huu ni kauli zake tata zinazomfanya awe vulnerable.

Kwa mfano leo ameongelea kuhusu namna Mexico itakavyoipa ukuta anaotaka kujenga.
Ukimsikiliza anatia shaka shaka sana na utayari wake

Kadri anavyoongea anazidi kujiweka katika wakati mgumu.

Tutafafanua
 
TRUMP
KAULI NA ALIVYO KATIKA 'MICROSCOPE'

'Base' ya Trump haibadiliki ni watu wanaoamini katika 'Trumpisim'
Wiki mbaya kama iliyopita haibadilisha utiifu wa 'base' yake

Tatizo lipo kwa waliompa benefit of doubt.
Siku zinavyosonga wanapungua kwa kutambua madhaifu ya Trump

Kampeni zilianza na wagombea zaidi ya 10, yakiwemo majina mazito yenye 'charisma' kama Rubio, S.Walker , R.Perry, Christie,J.Bush, n.k.

Focus ya media ilielekea kwa magwiji. Wingi ulisaidia kuficha madhaifu, Kadri walivyoputika akina Trump wakaonekana kwa uwazi zaidi. Wakiwa 3 kuwachimbwa kwa undani bila nafasi ya kukwepa hoja.Ndipo Trump anapokuwa mhanga

Mfano, ujenzi wa ukuta, hakuna aliyewahi kumuuliza Mexico italipa vipi gharama na alipoulizwa alikuwa na nafasi ya kubabaisha majibu.

Sasa anabwanwa na kusema atazuia 'remittances' za Mexicans wanazotuma kwao kadri ya Bilioni 24 kufidia ujenzi wa Bilioni 11.

Obama alipoulizwa kuhusu kauli ya Trump aliifafanua kiasi cha kumwacha Trump utupu.

Kimantiki tu, anachosema Trump ni US kukimbiziana na Western union!!!

Trump amejichanganya masuala mengi kama ya Nuclear yakionyesha udhaifu mkubwa

Lakini pia haishi kuamsha hisia. Jana alikuwa anakejeli ushindi wa Cruz.
Kauli zake ni za kujenga ufa kiasi cha kuhoji,huyo ndiye anajinasibu kuunganisha chama?

Kwenda mbele, Trump atabaki na kikosi cha waaminifu (katika asilimia 30-40).
Tatizo ni kuwa Kasich anavyozidi kupoteza nguvu, Cruz anafaidika na hilo

Lakini, Cruz hawezi kumshinda Trump au kufikia 1,237

Ili kushinda kabla ya RNC, Seneta Cruz lazima apate takribani asilimia 90 ya ushindi
Na kwa Trump lazima apate asilimia takribani 60 ya ushindi

Katika hali hii mkutano mkuu (RNC) ni uwezekano mkubwa kuliko option nyingine

RNC ikitokea, itakuja na gharama kubwa kwa GOP.

Tusemezane
 
Back
Top Bottom