Uchaguzi Igunga: Tumejifunza nini?

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Binafsi yangu nimekuwa nikijiuliza maswala mengi kulingana na uchaguzi nchini toka mwaka 2000 baada ya CCM kushinda ktk uchaguzi mkuu. Yapo mengi yaliyojitokeza na mengine kujirudia haswa pale vyama vya Upinzani vilipokataa kuunganisha nguvu yao sio dhidi ya CCM bali kupinga kujiunga na uchaguzi kwa sababu mfumo mzima wa uchaguzi nchini hautoa nafasi sawa kwa vyama na kikubwa zaidi TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), sii chombo huru.

Nashindwa kuelewa hivi hawa viongozi wa vyama vya Upinzani kweli wanafikiria wataweza kushinda chaguzi na kuchukua dola kwa kutumia mfumo uliopo ama wanafuata utaratibu uliopo kwa sababu ya kujipatia ruzuku na kuachiwa baadhi ya majimbo ili kuonyesha demokrasia ili hali CCM wakijua hawaezi kukubali kushindwa kwa kupitia sanduku la Kura.

Jambo moja muhimu sana ambalo wengi tumeshindwa kulielewa ni kwamba mshindi huchukua zote (winner takes all) ni mfumo ambao unaweza kabisa kuuthibiti kwa uchakachuaji kuhakikisha rais anashinda kwa popular vote na wabunge wanaohitajika ili kuunda serikali. Rais ndiye mwajiri wa viongozi wote wa NEC, TAKUKURU na Taasisi nyinginezo simamizi ya maadili ya kitaifa tunategemea vipi hawa watu watakuwa royal na wazalendo kwa Taifa hali ni waajiriwa na rais ambaye ni mgombea ktk uchaguzi. Na kikubwa zaidi rais ndiye mwajiri wa wabunge watakaokuwa mawaziri hivyo watajipanga kwa kumtumikia bwana.

Hivi kweli kuna watu walifikiria kwamba Chadema watapewa ushindi Igunga, walifikiria kwamba CCM baada ya kupoteza imani ya wananchi wataendelea kuonyesha wanavyoporomoka baada ya kuondoka kwa Rostam, na kuwapa ushindi Upinzani wakati chama kama chama kilitaka kuonyesha wananchi kwamba kuondoka kwa Rostam sii pigo la chama na chama kitaendelea kuwatumikia wananchi na sii Magamba. Katika hali hiyo tete, hata kama ningekuwa mimi ndiye rais, nisingekubali matokeo yoyote ya kushindwa Igunga.

Sawa wapo watu wanasema vyama vya upinzani kaa Chadema wajikite vijijini ili kuwaelimisha wananchi. Wananchi wameisha elimika vya kutosha kinachotakiwa ni kufungua matawi ya vyama na kuwashirikisha wananchi wazawa na wakazi wa majimbo hayo kuwakilisha chama. hapakuwa na sababu kabisa ya Chadema, CUF vya vyama vingine 6 kupeleka nguvu kubwa Igunga wakati vyama hivi vilikuwa havina ofisi za wawakilishi ktk kata zote ambao kwa muda wote wanakuwa pamoja na wanavijiji. Zaidi ya yote CCM had to win by all means! aliyeshindwa kuliona hili basi yeye ndiye mwenye matatizo.

CCM kwa muda wote wamekuwa wakitumia vyombo vya kitaifa ambavyo wamerithi kutoka CCM ya chama kimoja toka iwajumbe wa nyumba kumi, wamekuwa wakitumia wajumbe wa Halmashauri za miji, walimu na wakuu wa wilaya na kadhalika ili kuonyesha nguvu ya chama hiki kiutawala jambo ambalo vyama vya Upinzani hawana. Kwa kila hali, utaweza vipi kushindana na chama kilichoshika mpini?.

Leo tunakubali matokeo ya Igunga kama tulivyokubali matokeo ya kitaifa na sintashangaa kama nitasoma lawama kubwa ziliel;ekezwa makao makuu ya vyama hivi kwa matumizi mabaya ama kutowekeza ktk vitu kadhaa lakini bado ukweli utasimama ya kwamba pale CCM inataka kushinda itashinda kwa hali yoyote ile. Bila mabadiliko ya Kikatiba, bila mabadiliko ya kimfumo vyama vya Upinzania vitaendelea kuambulia baadhi ya majimbo kwa manufaa ya chama tawala ili wapate kuonyesha mataifa demokrasia inafanya kazi.

Mwisho, inashangaza sana kuona kwamba bunge limekwisha na maombi ya Katiba mpya yaliwekwa kando, miaka inakwenda siku zinayoyoma na uchaguzii wa mwaka 2015 unakaribia hali hakuna mabadiliko yoyote dhidi ya kanuni mbaya zilizotumika toka mwaka 1995. Tumeshuhudia Takrima zikitolewa Igunga, tumeshuhudia vijana wakipewa ajira za muda ktk uchaguzi na sii uzalendo wa kujitolea isipokuwa njia ya kutumikia matumbo yao.

Kila naposoma mada nyingi humu JF hujiuliza hivi kweli wananchi wamejifunza lolote kutokana na uchaguzi hizi, kweli wanaweza matumaini ya kuiondoa CCM madarakani kwa kupitia sanduku la KULA...sanduku ambalo maskini wote ndipo hupatia riziki zao! Kwa mtaji huu nawahakikishieni CCM itashinda mwaka 2015 na mtarudi hapa kuzungumza kwa jazba na matusi lakini sii makosa yenu bali CCM imejiwekea mazingira ya Ushindi toka mwaka 1995 na vyama vya Upinzani vimeridhia wote wakiona usongo kushika nafasi ya pili.
 

Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,162
10,292
Mkuu umenena vyema!!

Kuna usemi mmoja nimeuona mahala kwamba; ukifahamu kwamba refa wa mchezo ni wa upande wa mpinzani wako, halafu ukakubali kuingia uwanjani (kucheza); ina maanisha umekubali pia kuchezewa rafu bila rafu hizo kuadhibiwa, kunyimwa penati na adhabu za wazi kabisa, kupewa kadi nyekunda bila kufuata sheria za mchezo n.k.

Hivyo ndivyo vyama vya upinzani vilivyoshiriki vilifanya makosa. Kwani vyama hivyo vingeunganisha nguvu na kukataa kushiriki uchaguzi mdogo, ingekuaje?! Au vingeungana na kutaka kuwepo na taratibu mpya za dharura (zikiwepo kuwepo kwa tume huru ya muda; kuhakiki upya kwa daftari la wapiga kura n.k.), nini kingetokea?!

Kwa hiyo mkuu, hii ni changamoto kwa demokrasia ya vyama vingi hapa TZ. Hivi vyama vimekua kama vilalamishi wakati vina uwezo kutokuwa vilalamishi kwa kuepuka kujiingiza katika mazingira ya kulalamika.

Suala la kuwa na Katiba mpya itakayozingatia masuala uliyoyasema kwa kweli lina utata sana hadi sasa. Na utata wenyewe umeongezewa nguvu na suala hili kutokuwepo kwenye vipaumbele vya wizara husika (rejea hotuba ya waziri); kipaumbele kikiwa ni suala la uharakishaji wa usikilizwaji wa kesi mahakamani. Sasa kwa namna hii, sijui kama ndio mambo ya wadanganyika kuendelea kudanganywa.

Halafu jambo la mwisho ambalo ndilo la msingi na la kujifunza ni la sisi waTZ kuacha kuwa wapiga porojo tu! Tuanze kufanya mambo kwa vitendo; na tusitarajie mtu au kikundi fulani cha watu wachache ndio watusaidie. Ni sisi wenyewe waTZ kwa ujumla ndio tunapaswa kuchukua hatua. La sivyo hawa CCM watatawala mpaka kiama.

 

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
297
Mkandara umezungumzia ukweli.

Lakini utafikaje unakotaka tufike ?

Vyama vya upinzani havinabudi kushiriki katika chaguzi hizo wakati mchakato wa mabadiliko unapofanyika.

Kwa kushiriki huko watu watajua umuhimu wa kufanya hayo mabadiliko.
 

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Magwanda have shown, albeit infinitesimally, that they can change politics direction. They have confrontated the ruling CCM with unexpected fierce resistance just to prove their widespread accepatance. CCM victory with such a narrow margin tells it all. However Magwanda should not be complacent at their current success but rather must use more time and resources in consolidating party structure, especially from bottom where most undecided votes dwells.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
Ndugu yangu Mkandara, siyo kila mtu anayekaa darasani anaweza kujifunza. Wapo wanaokaa darasani ili wamalize siku na wao haiwajalishi sana kama wanajifunza au la. Wapo ambao wanakuwa darasani kwa sababu wazazi wao wanasema waende "shule" na hawa watamaliza madarasa yote na hata wakifeli mwishoni hawana wasiwasi kwa sababu kuna "family business" inawasubiria. Kwao kupasi au kufeli hakumaanishi lolote. Kumaliza darasa kwao ndio jambo la msingi.

Sasa unaweza ukawapa wote hawa elimu na wengine naukarudia mara kwa mara lakini si wote wanafunzika. Mtu anayerudia kosa lile lile kwenye swali lile lile huku akitumia majibu yale yale licha ya kuelezwa namna nyingine ya kufikia jibu sahihi huwezi kumsaidia. Anaweza akalalamikia darasa, mwalimu, chaki, wino, au hata kelele za wanafunzi wengine darasani. Lakini mwisho wa siku swali ni je anafundishika? Yawezekana ana matatizo ya ndani ya kujifunza ambayo yanahitaji kugunduliwa kwanza kabla masomo zaidi hayajapatiwa.

Sidhani kama Igunga imetoa somo lolote ambalo halikujulikana Tunduru, Babati, Mbeya Vijijini, Busanda, Biharamulo, Tarime au kwingine. Hivyo badala ya kuuliza twaweza kujifunza "nini" labda swali liwe "kwanini hatufundishiki"...?
 

elimukwanza

Senior Member
Dec 27, 2010
168
23
Mimi nafikiri kuna baadhi ya viongozi wa upinzani hasa cdm wana lao jambo haiwezekani mmetoka kwenye uchaguzi juzi
(2010) mmeona jinsi uchaguzi ulivyokuwa halafu bado hamna evaluation yeyote.katiba ni medium/long term ilitakiwa kwanza waanze na tume huru ya uchaguzi hiyo inawezekana kabisa ndani ya miaka 5 sasa ccm wanacheza nao na muda na wenyewe wameridhika.
Cdm wanatakiwa wawe wazi kabisa kuwa hawataingia kwenye uchaguzi 2015 kama hakuna tume huru ya uchaguzi na watembelee kwenye maneno yao maana hata kama watashiriki kwa tume hii hawatashinda hata kama kutakuwa na ufisadi wa trioni 3 serikalini.
 

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,327
2,227
Mara nyingi hua najiuliza,ni kwanini watu wengi wanasema sana pale tatizo linapo
tokea na sio kusema sana kabla ya tatizo ili kuliepusha tatizo hilo?

Kwa mfano timu ya mpira ikifanya vibaya kila mtu anageuka kocha nakusema wangefanya hivi na hivi.
Achilia mbali kocha kutoa sababu lukuki,lakini kwanini makosa yanayo onekana mwanzoni hua
hayatolewi ushauri kabla ya timu kuingia uwanjani?

Mkandala na MM naamini mawazo yenu ni mazuri,na ni mazuri kweli kweli lakini
nashindwa kuwatofautisha na hivyo vyama "visivyo fundishika",.....

Kama havi fundishiki kweli basi ni sikio la kufa lisilo sikia dawa,...lakini kama havifundishiki
kwa sababu "waalimu" na "walezi" hawatoi ushauri na mafunzo vyema kwa wanafunzi kabla
ya kuingia kwenye "mtihani" ikiwemo kuwakumbusha namna mbali mbali za kuutizama mtihani na
kukabiliana nao.

Yes,chadema na cuf wanaweza (may be) kukubaliana na kususia uchaguzi ili tume irekebishwe kwanza
na kuwe na uwanja linganifu kwa vyama vyote,...lakini tusisahau kwamba Tanzania kuna utitiri wa vyama vya siasa
na vingine ni kama "Duka" kwa waanzilishi wao,..wakipewa vijisenti kidogo tu na ccm ili washiriki
ili kuonesha demokrasia watafanya hivo,....kama MM alivosema hawajali kufaulu au kushindwa maana wanajua mwisho wana pipi ya kulamba.

Kuna haja ya viongozi wa vyama vyote vya upinzani Tanzania kuto dharauliana,...atleast katika hili.
Waitane,wafanye kikao na wakubaliane wote kwa pamoja kuhusu kususia uchaguzi wowote utakao fanyika chini ya
uwanja ulipo sasa hadi utakapo rekebishwa......(japo hii ni kama ndoto za alinacha maana wengi wana njaa sana,wakioneshwa
kipande cha nyama kidogo tu mate yana wadondoka chini).
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Serikali ya CCM, Polisi wa CCM, Tume ya Uchaguzi ya CCM, tutegemee nini kizuri! Majizi yamemweka mwizi mwenzao. Dawa ni kuingia msituni tumechoka!
 

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Ni kweli tatizo kubwa linakuwa/limekuwa kukosekana kwa free and fair competing environments kwa vyama vyote katika chaguzi husika. Kuna wakati huwa najiuliza what if Rais ambaye kimsingi ndiye aliyemteau Mkurugenzi akimwambia atangaze matokeo kadiri anavotaka kwa maana ya kumtangaza mgombea wa ccm kuwa mshindi hata kama ameshindwa. Muundo wa NEC unapaswa kubadilika pia kuwe na sheria ndogo mahususi kwa kila uchaguzi. Lakini pia swala la vyama kuendelea kushiriki licha ya mazingira kuwa kandamizi nadhani inawajenga zaidi na kuzidi kujitambulisha kwa wananchi
 

elimukwanza

Senior Member
Dec 27, 2010
168
23
Na ni kama ni muungano wanaopigania vyama vya upinzani basi waanze na hili la kususia uchaguzi mpaka tume huru ya uchaguzi vinginevyo watu watakuwa wanahudhuria mikutano na maandamano kama fasheni mwisho wa siku wa kupiga kura hamna kitu.huu uchaguzi wa igunga karibu watu wengi niliowasikia mimi mitaani,kazini maoni yao walikuwa wakisema cdm wanawapelekesha ccm lakini hawatashinda ni jf tu ndiyo watu walikuwa na mawazo ya cdm au cuf kushinda.hata kama ni wewe mkandara ungekuwa rais,ccm kushindwa igunga ni uzembe tena wa hali ya juu sana.cdm mtabakiwa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa tu oohh mmejitahidi oohh mmewazidi cuf think big you must fly men.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
Clemmy tafuta makala yangu ndefu ya "CHADEMA toka hapa mpaka kule " iliyotoka Kabla ya uchaguzi mkuu au ya "pembetatu ya ushindi". Zote zipo hapa JF.
 

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Ni kweli tatizo kubwa linakuwa/limekuwa kukosekana kwa free and fair competing environments kwa vyama vyote katika chaguzi husika. Kuna wakati huwa najiuliza what if Rais ambaye kimsingi ndiye aliyemteau Mkurugenzi akimwambia atangaze matokeo kadiri anavotaka kwa maana ya kumtangaza mgombea wa ccm kuwa mshindi hata kama ameshindwa. Muundo wa NEC unapaswa kubadilika pia kuwe na sheria ndogo mahususi kwa kila uchaguzi. Lakini pia swala la vyama kuendelea kushiriki licha ya mazingira kuwa kandamizi nadhani inawajenga zaidi na kuzidi kujitambulisha kwa wananchi
 

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
850
508
vyama vya Upinzani vilipokataa kuunganisha nguvu yao sio dhidi ya CCM bali kupinga kujiunga na uchaguzi kwa sababu mfumo mzima wa uchaguzi nchini hautoa nafasi sawa kwa vyama na kikubwa zaidi TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), sii chombo huru

Kaka Mkandala : nakubaliana na wewe kwamba upo umuhimu wa Vyama vya upinzani kuunganisha nguvu kupinga kujiunga na uchaguzi kwa ajili ya mfumo mzima wa ukandamizaji na usio sawa. Swali utanganisha nguvu na chama gani? SAUT? CUF?, UPDP ? je wewe unaona kuna vyama hapo au ni mapandikizi tu ya ku justify demokrasia. Bado tuna kazi kubwa hebu tushauri Chadema wagomee uchaguzi halafu CUF washiriki na utasikia hata kidogo habari za udini, tindikali wala DC feki uchaguzi utakuwa wa haki na hata polisi hawatakuwepo kwa wingi!. kwa sababu hao wote lao ni moja. Tujadili nini cha kufanya.....

Nashindwa kuelewa hivi hawa viongozi wa vyama vya Upinzani kweli wanafikiria wataweza kushinda chaguzi na kuchukua dola kwa kutumia mfumo uliopo ama wanafuata utaratibu uliopo kwa sababu ya kujipatia ruzuku na kuachiwa baadhi ya majimbo ili kuonyesha demokrasia ili hali CCM wakijua hawaezi kukubali kushindwa kwa kupitia sanduku la Kura.

Kaka Mkandala: Hakukuwa na vyama vya upinzani kulikuwa na Chama cha Upinzani Chadema na mapandikizi sita. Tafakali walitakiwa kufanya nini? wasishiriki ili CCM wapate mtelemko?

Hivi kweli kuna watu walifikiria kwamba Chadema watapewa ushindi Igunga, walifikiria kwamba CCM baada ya kupoteza imani ya wananchi wataendelea kuonyesha wanavyoporomoka baada ya kuondoka kwa Rostam, na kuwapa ushindi Upinzani wakati chama kama chama kilitaka kuonyesha wananchi kwamba kuondoka kwa Rostam sii pigo la chama na chama kitaendelea kuwatumikia wananchi na sii Magamba. Katika hali hiyo tete, hata kama ningekuwa mimi ndiye rais, nisingekubali matokeo yoyote ya kushindwa Igunga

Mimi najua hata Chadema hawakwenda igunga wakitegema ushindi wa chee !!! walijua ni mapambano na si dhidi ya CCM tu ni dhidi ya serikali na mabavu ya DC, mawaziri, polisi, Uislam fake{ hapa naomba nieleweke waislamu safi hawashabikii ujinga huu} nk nk. lakini vita ni vita Utaacha watu au wezi wabake mke na watoto wako kisa kwa sababu unajuwa fika kwamba wana nguvu kuliko wewe na uwezi pambana nao . ni boraBila mabadiliko ya Kikatiba, bila mabadiliko ya kimfumo vyama vya Upinzania vitaendelea kuambulia baadhi ya majimbo kwa manufaa ya chama tawala ili wapate kuonyesha mataifa demokrasia inafanya kazi ufe na hata kama mkeo na binti yako bado watabakwa hata baada ya wewe kufa lakini watasema baba alipigana kiume na mbakaji atakiri kwamba hakubaka kirahisi. CCM wanajua joto ya jiwe waliyoipata Igunga. Ni muda tu na tukiunganisha nguvu wote pamoja . Dhuluma itshindwa na Haki.
 

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
850
508
Sidhani kama Igunga imetoa somo lolote ambalo halikujulikana Tunduru, Babati, Mbeya Vijijini, Busanda, Biharamulo, Tarime au kwingine. Hivyo badala ya kuuliza twaweza kujifunza "nini" labda swali liwe "kwanini hatufundishiki"...?
  • Unataka tujifunze nini mh> mzee mwanakijiji ? ulitaka Chadema wakimbie uwanza wa vita ili adui ajitangazie ushindi wa chee? Tujuze kaka yetu nini chadema wafanye?
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Clemmy tafuta makala yangu ndefu ya "CHADEMA toka hapa mpaka kule " iliyotoka Kabla ya uchaguzi mkuu au ya "pembetatu ya ushindi". Zote zipo hapa JF.

Mkuu hiyo makala ya pembetatu ya ushindi ingekaa hapa juu ikawa ni makala rejea. Niliipenda sana na hiyo makala ina elimu tosha ya kukipatia chama chochote ushindi kama kitajipima na kutatua matizo uliyoyaongela kwenye hiyo makala.
 

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Clemmy,

Mkuu wangu sii kweli kabisa wapo watu kama sisi tukisema hatusikilizwi na kama ungekuwa ukifuatia michango yangu na Mwanakijiji hili swala tumelizungumzia siku nyingi sana. Na kwa taarifa yako ktk fikra zangu, nilisema hapa janvini kwamba Chadema hawawezi kushinda Igunga lakini majibu yaliyokuja yalikuwa matusi ya nguoni. Na sikutaka kuwakatisha tamaa lakini nilijua fika CCM hawawezi kuachia Igunga na walikuwa na kila sababu ya kuweka nguvu kubwa ili kukinusuru chama. Je unafahamu ya kwamba kuna hesabu kubwa ya watu hawapigi kura kwa sababu wanajua matokeo kabla ya kura yao?

Leo hii wanaaminika machoni pa watu ya kwamba bila Rostam inawezekana ingawa Rostam mwenyewe kafanya kazi kubwa kuwapa ushindi.Hivyo swala la ushindi halikuwa kuwawakilisha wana Igunga bali kwa Tanzania nzima kuwajulisha wananchi kwamba CCM bado imara ingawa ndio hivyo. Jamani Igunga yenyewe ikiwa na right handman wa rais maendeleo yenyewe ndio kama hivyo, mnafikiri kuna la maana watakalopata baada ya Rostam!..Sii kosa kwa mwanamme kutumia mamillioni kwa mwanamke asiyekupenda kama unataka kuonyesha dunia!..


Muonamambo,
Mkuu wangu hakuna sababu ya kusindikiza uchaguzi kwa kutumia jina la demokrasia. Mahala isipokuwepo hakuna sababu ya kuwashawishi wananchi kitu ambacho hamuwezi kukamilisha. Vyama vya Upinzani vinatakiwa kuonyesha msimamo wao ktk swala zima la kikatiba. Na wananchi tutasimama nao kaa wao watakubali kuubeba msalaba huo kwa sababu wanaoumia sii wao bali wananchi.

Tusidanganyane na hizi siasa kwa sababu mfumo uliopo hauwezi kuwaletea wananchi mageuzi yoyote pasipo ushindi kiti cha IKULU. Na maadam CCM ndiye mtawala na mwajiri wa NEC na TAKUKURU tusitegemee kabisa kwamba chama kingine kinaweza kutangazwa mshindi.. how? yaani mimi msajili wa vyama leo nione takwimu zinaonyesha Chadema wameshinda kisha napokea simu ya rais akinambia nitangaze CCM wameshinda nitapuuza?... Labda nambieni nyie kweli kuna mtu ambaye anaweza kutangaza majibu tofauti na mwajiri wake! wakati akijua kwamba akitemwa hapo hatapata ajira tena. CCM watahakikisha maisha yake yanakuwa mabaya kuliko maelezo..Hivi kweli kati ya watu 171,019, wapige kura 53,000 hamtaki kufahamu kwa nini inatokea hivyo. Kwa nini hesabu kubwa ya wananchi waliojiandikisha kupiga kura hawapigi na NEC mshipa hauwagongi!..

Kwa hiyo hatuna hila, viongozi wa vyama vya Upinzani wanaporudi bungeni au hapo walipo leo cha kuzungumzia ni kuvunja uongozi wa NEC na TAKUKURU na viongozi wake watapendekezwa na rais lakini lazima wapitishwe na Bunge kisha vyombo hivi lazima viwe huru ktk kazi zao na sheria ziwe wazi kabisa kuhusiana na miiko ya kampeni. Jamani, Seif Sharrif alishinda uchaguzi wa Zanzibar mwaka 1995, 2000, 2005 na kwa uhakika wangu mimi binafsi Dr.Slaa alishinda mwaka 2005 na hata uchaguzi wa Igunga - Chadema wameshinda! bado mnataka kuendelea kucheza mpira wa mchangani kwa sheria za kimataifa!..Kama kuitwa wahuni mmeisha itwa sana na pengine ndio wakati wa kuwa wahuni kweli..
 

elimukwanza

Senior Member
Dec 27, 2010
168
23
Mkuu mkandara mambo unayosema ni ya msingi sasa ifike mahali viongozi wa chadema wawe wazi its fine walipofika(walipoifikisha cdm) wanahitaji pongezi lakini kama uwezo wa tunakoenda hawana waseme wachukue wenye uwezo lasivyo heshima wanayopewa sasa na wananchi ikipotea kinume chake ni kupoteza thamani kabisa.na watambue mabadiliko wanayotaka ni kwa ajili ya wananchi si chadema kama ni kwa ajili ya chadema basi watambue ya cuf na nccr yatawafuata.wasilaze damu moto walionao ukipungua tu ni rahisi kuuzima.kama mtaendelea na hizo sinema mtaitwa kampuni si chama tena wekeni hapo juu watu wanaoweza ku risk mbona tunawaona mnaweza mnao!
 

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
850
508
Mkandala:
Bado bakubaliana na wewe kuwa si vyema kuwa wasindikizaji wakati unajuwa nafasi ya kushinda ni finyu.Lakini cha kujiuliza hapa ni kwamba
  1. Je ni vyama vyote viko katika mstari mmoja ? je ni kweli viko kwa ajili ya maendeleo ya wananchi? Je kuna uwezekano wa kuviondoa kwa katiba ya sasa vile visivyo kidhi vigezo? je vigezo ni vip? Je katika visivyo kidhi vigezo na CUF nao wapo? Ni maswali magumu kwa maana adui wa upinzani ni wapinzani wenyewe
  2. chadema kama watasusia uchaguzi na vyama vingine vikaendelea nini kifanyike? Nini itakuwa propaganda ya CCM? si watasema Chadema wanapenda kumwaga damu mbona vyama vingine wanashiriki wao wanakataa kwa sabau gani? kwani vyama vingine havioni haya mapungufu ya katiba, Tume ya uchaguzi na mengineyo? Tutafakari
  3. Ni kweli kwamba mfumo uliopo unatoa mamlaka makubwa kwa Raisi na vyombo vyote vinanvyosimamia uchaguzi viongozi wake wanateuliwa naye na ni raisi kukandamiza demokrasia watakavyo. Swali hapa la kujiuliza.... Mfumo huu bado hupo na dawa yake ni kubadilisha katiba tu. Kwa mwenendo wa sasa tunaihitaji serikali ndio iratibu mabadiliko ya katiba[ Jambo ambalo mimi silihafiki. uwezi kumwambia mwizi atunge sheria zitakazomfunga yeye mwenyewe} kitu ambacho ningeshauri ni chadema na vyama vichacahe vingine vinavyohitaji mabadiliko kuandaa maandamano ya mfulululizo yasioisha kuishinikiza serikali kuharakisha uratibu wa kuanzisha katiba mpya.... Naomba kutoa msisitizo kwa kwani haki aiombwi ulazimishwa. swali linakuja ni watanzania wangapi wako tayari kufa ili vizazi vijavyo viweze kupaya haki?
  4. Swala la kwenda bungeni na kushinikiza kuvunja NEC wala TAKUKURU halitawezekana kwenye bunge lenye idadi zaidi ya theruthi mbili ya NDiyooooooo. hilo lisahau ni kupoteza tu kodi ya wananchi.
Nawakilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Top Bottom