Uchaguzi Igunga: Tumejifunza nini?

Okey,kama ushauri umekuwa ukitolewa na viongozi wengi wa chadema wapo humu
basi ni either wana dharau ushauri unaotolewa humu wakidhani wana jua sana kuliko
wanao wapa ushauri,....au wanaweka ushauri huo kama akiba ili wautumie baadae.

Lakini sababu ya mwisho ni dhaifu sana,maana kama ni akiba walisha jifunza toka chaguzi ndogo kibao
zilizo pita na uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Itoshe tu kusema "hawataki ushauri",...ingawa haitoshi kusema "tumechoka kushauri"....

Nakumbuka nilisema chadema hawatashinda Igunga,..watu kama The invincible walinambia naota
Speaker
Comments zako ni interesting. Namkumbuka Maggid Mjengwa. Naye alitabiri kuwa Chadema ingeibuka ya tatu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana based on historical evidence...za nguvu ya kafu na ushindi wao wa huko nyuma. You know what happened.

Utabiri wako, kama wa Maggid, unaacha some important variables in the model.

Nikamwambia

Okey,...
siidharau chadema,na sijawahi ila nachosema ni facts kabisa,...
kwamba wanaenda Igunga sio kwa ajili ya kushinda,ila kwa ajili ya
kukijienga chama maana ni opportunity imepatikana na lazima waitumie
(that is good kwa chama chochote cha siasa,nashangaa kwanini NCCR na wengine hawajatangaza
nia ya kusimamisha wagombea so far,...)

Ila ninacho tofautina na maono ya wengi hapa,ni kama naonekana nawavuta shati wasiende
na nguvu na imani ya kushinda,ila ni vyema kuwa realistic "hata kama siasa ni lazima useme nitashinda tu"

Hakuna jinsi chadema itashinda Igunga,ila wana nafasi nzuri sana kujijenga sasa Tabora nzima na 2015
wakisimamisha watu wasio kua mamluki watashinda majimbo mengi sana

Sababu za mimi kutoa utabiri wangu mdogo ilikua ni kwasababu uwanja walio kuwa wanaenda kucheza ndo
ule ule ambao wamekua wakidai kuonewa siku zote na hawajawahi kutaka uwanja ubadirishwe.

Viongozi wa chadema wako humu,wapo walio niponda kwenye thread ile,....lakini hawa kuchukua hata tone
la ushauri na leo hii hakuna hata mmoja anae onekana mtandaoni (labda wanafuta machozi bado).

Lakini pamoja na kwamba chadema ni chama "kisicho taka ushauri",kitaendelea kuwa chama
kinacho lalamika kila siku,....sitashangaa kisipo chukua dola mwaka 2015 na viti vyake vya ubunge kushuka.
 
Nadhani tumeshindwa kujikwamua kwa sababu akina Mtikila ni wachache sana.

Hivi hakuna mtu au chama kinachoweza kwenda mahakamani leo na kuizuia tume ya uchaguzi kusimamia chaguzi zote hadi sheria itakaporekebishwa ili tume iundwe na kufanya kazi katika hali inayokubalika kwa wadau wote?

Pia nakubaliana na wadau kwamba suala la kupunguza pressure kwenye madai ya katiba mpya litatufanya tuingie kwenye uchaguzi wa 2015 katika mazingira ya 1995, 2000, 2005 na 2010. Ikitokea hivyo, ni bora kutofanya uchaguzi huo kwa sababu madhara yake yatakuwa makubwa kwa watanzania!
 
Okey,kama ushauri umekuwa ukitolewa na viongozi wengi wa chadema wapo humu
basi ni either wana dharau ushauri unaotolewa humu wakidhani wana jua sana kuliko
wanao wapa ushauri,....au wanaweka ushauri huo kama akiba ili wautumie baadae.

Lakini sababu ya mwisho ni dhaifu sana,maana kama ni akiba walisha jifunza toka chaguzi ndogo kibao
zilizo pita na uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Itoshe tu kusema "hawataki ushauri",...ingawa haitoshi kusema "tumechoka kushauri"....

Nakumbuka nilisema chadema hawatashinda Igunga,..watu kama The invincible walinambia naota

Nikamwambia

Sababu za mimi kutoa utabiri wangu mdogo ilikua ni kwasababu uwanja walio kuwa wanaenda kucheza ndo
ule ule ambao wamekua wakidai kuonewa siku zote na hawajawahi kutaka uwanja ubadirishwe.

Viongozi wa chadema wako humu,wapo walio niponda kwenye thread ile,....lakini hawa kuchukua hata tone
la ushauri na leo hii hakuna hata mmoja anae onekana mtandaoni (labda wanafuta machozi bado).

Lakini pamoja na kwamba chadema ni chama "kisicho taka ushauri",kitaendelea kuwa chama
kinacho lalamika kila siku,....sitashangaa kisipo chukua dola mwaka 2015 na viti vyake vya ubunge kushuka.
Hapo uliposema Chadema wamekwenda Igunga ili kukijenga chama kwa wananchi wa Tabora ndilo tatizo langu kubwa sana!..Huu sii wakati wa chama kujijenga hata kidogo, ni wakati wa chama kuwahakikishia wananchi watawawakilisha vizuri na kuwapelekea maendeleo na sii swala la chama. Ni nafasi moja kwa miaka mitano waliyopewa wananchi kufanya maamuzi makubwa, wakati vyama vinaweza ifanya kazi hiyo wakati wowote ule nakwa miaka mitano wakipewa ruzuku za kuwawezesha. Ni wakati Chadema ilitakiwa kuwa ktk msiba mkubwa wa kimaendeleo na wananchi wa Igunga sii kujijenga wao kichama. Na kusema kweli husikia hasira zaidi kila naposoma chama kujijenga kwa kutumia wkaati muafaka kwa wananchi kama huo.

Baada ya kumsoma Regia Mtema akieleza mambo aloyaona huko Igunga! nashangaa pia kama alikuwa hajui hali hii ipo sehemu kubwa ya Taifa leo kuliko maendeleo yenyewe..Hawa wananchi hawajui maendeleo zaidi ya kile wanachokiona ktk mazingira yao na wao wanaona poa tu kutokuwa na shule, Zahanati, kwenda maili 10 kufuata maji au huduma za maisha. Takwimu zinajieleza wazi, nchini ni asilimia 14 tu wenye Umeme, asilimia zaidi ya 50 hawana maji na tukizungumzia maji safi ni asilimia 90. Maendeleo ya Shule na Zahanati unapima, mwalimu mmoja kwa wananfunzi wangapi, daktari mmoja kwa wagonjwa wangapi hii ndicho kipimo cha maendeleo ya elimu na Afya kwa sababu kama mwalimu au daktari uwezo wake ni watu 10 waliozidi wote ni hasara na umaskini zaidi kwa Taifa.

Yawezekana makosa ni yetu sisi wananchi kuweka matumaini tk vyama badala ya sisi wenyewe kuchukua maamuzi magumu..Hivi wananchi wakikataa kwenda kupiga kura hadi mfumo bora wa upigaji kura utakapoundwa tunaweza kuyaleta mabadiliiko?.. maana nikiangalia huko Igunga waliojiandikisha ni 171,019 na idadi ya watu ambao hawakupiga kura inafika 128,000 na ukiweka waliovipigia vyama vingine tunapata idadi isiyopungua 146,000. Hawa Laki 146 wasipopiga kura, bado sheria inaruhusu CCM kupewa ushindi hata kama idadi ndogo yimejitokeza kupiga kura? bado vyombo vya kimataifa watasema uchaguzi ulikuwa huru na umekubalika hata kama waliojitokeza kupiga kura ni washabiki wa CCM pekee!..

Tatizo la maamuzi ya wananchi ni kwamba linakuja siku ya uchaguzi, hivyo maamuzi haya hayawezi kuwa ya maana sana. Mathlan tukisema tuweke mgomo 2015 na matokeo yakawa mabaya zaidi ktk wananchi kujitokeza kupiga kura, sheria inasemaje? Je NEC ikiwatangaza CCM kama washindi tena nini plan B ya wananchi kuhakikisha sauti yao inasikika..NGUVU ya UMMA sii Chadema ila ni sisi wananchi tufikirie hilo!

Kusema kweli mimi nimechoka sana na hali ya siasa nchini ambapo vyama vingi vinachumia tumbo. Kulikuwa na vyama 8 jimboni Igunga, hawa wote walijitokeza sii kwa manufaa ya wana Igunga isipokuwa kugombea ruzuku kwa sababu fedha zilizotumika pale Igunga zingeweza kuboresha mambo mengi sana na leo hii wamemchagua mbunge ambaye pato lake ni kubwa kuliko pato la jimbo zima ktk maendeleo yake. Hivyo basi Mbunge ni lazima awe mkazi wa sehemu yake na pia tumegundua kwamba Mbunge anapokuwa waziri hupendelea sehemu inayompa kula yake na kama hakufanya jambo jema kwa jimbo hilo, anaruhusiwa kuhama jimbo na kugombea jimbo jingine, mkoa mwingine ili mradi anatazama uwezekano wa yeye kushinda uchaguzi na sii kuwawakilisha wananchi. Uchaguzi nchini unalenga ushindi wa Wabunge na vyama ktk maslahi yao na sii wananchi. This is very wrong!
 
Back
Top Bottom