UCHAGUZI 2015: CCM dhaifu kisiasa, Kikwete mgonjwa hataweza kampeni, kashfa kila kona

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Ni wazi CCM hivi sasa ni chama dhaifu kisiasa kuliko wakati wowote katika historia yake. Ni wakati huu kikiwa dhaifu hakina hazina ya viongozi wenye nguvu katika jamii ambao wana uwezo wa kukisemea na kukirudishia uhai kama alivyofanya nyerere baada ya mwinyi kuachia madaraka. Ni chama ambacho kiongozi wake mkuu yeye binafsi na familia yake wanatuhumiwa kuifisadi nchi na takribani wagombea urais wote wana tuhuma za ufisadi.

Chama kimepasuka kila kona na ni kama magenge ya mafia yanapigana ili kuchukua nafasi ikulu ili yapate kuiba tena na tena. CCM hii ndiyo inatuma vijana wake kuwapiga wazee wa chama ambao pengine wangeweza kuubadilisha umma kifikra na kuifikiria ccm kama chama na kwamba waovu wasihusishwe nao na kutoa ahadi ya kuwaondoa katika mbio za urais kama nyerere alivyofanya kwa malecela.

Warioba kapigwa,salim ahmed salim yuko kimya,mkapa yuko kimya,nchi inafanana na kuku aliyekatwa kichwa,haina mtu wa kutolea majibu masuala ya kitaifa.Safari hii wapinzani washindwe wenyewe kwa kuwa ni CCM ambayo imetoa mwaka mzima wa kampeni na elimu kwa umma kwa kuanzia sasa kwenye chaguzi za mitaa,kampeni za bunge la katiba,kura ya maoni,escrow,operesheni tokomeza,mchakato wa uchaguzi na mengine mengi yatasaidia wapinzani kuibana vilivyo CCM na kuinyanganya kura nyingi,
 
mukulupapaa

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
2,913
2,000
Mwenyekiti atahutubia hivyo hivyo hata akiwa kwenye machela ili mradi pesa ipo tena bilions za kutosha toka ESCROW sasa ya nn tuwe na hofu ya UKAWA,wakati watanzania wenyew wanapenda rushwa sana,tuko tayar kununua kura ya mtu yeyote hata ya mbowe ikibidi
 
Gor

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,793
1,195
ni wazi ccm hivi sasa ni chama dhaifu kisiasa kuliko wakati wowote katika historia yake. Ni wakati huu kikiwa dhaifu hakina hazina ya viongozi wenye nguvu katika jamii ambao wana uwezo wa kukisemea na kukirudishia uhai kama alivyofanya nyerere baada ya mwinyi kuachia madaraka. Ni chama ambacho kiongozi wake mkuu yeye binafsi na familia yake wanatuhumiwa kuifisadi nchi na takribani wagombea urais wote wana tuhuma za ufisadi. Chama kimepasuka kila kona na ni kama magenge ya mafia yanapigana ili kuchukua nafasi ikulu ili yapate kuiba tena na tena. Mh rais ambaye ndiye mwenyekiti wa ccm ni mgonjwa na kama alivyothibitisha mwenyewe ni kwamba anaumwa kansa,ni dhahiri hatahimili harakati za kampeni tena zaidi ya kuhesabu siku zake na kudra za mungu.ccm hii ndiyo inatuma vijana wake kuwapiga wazee wa chama ambao pengine wangeweza kuubadilisha umma kifikra na kuifikiria ccm kama chama na kwamba waovu wasihusishwe nao na kutoa ahadi ya kuwaondoa katika mbio za urais kama nyerere alivyofanya kwa malecela.warioba kapigwa,salim ahmed salim yuko kimya,mkapa yuko kimya,nchi inafanana na kuku aliyekatwa kichwa,haina mtu wa kutolea majibu masuala ya kitaifa.safari hii wapinzani washindwe wenyewe kwa kuwa ni ccm ambayo imetoa mwaka mzima wa kampeni na elimu kwa umma kwa kuanzia sasa kwenye chaguzi za mitaa,kampeni za bunge la katiba,kura ya maoni,escrow,operesheni tokomeza,mchakato wa uchaguzi na mengine mengi yatasaidia wapinzani kuibana vilivyo ccm na kuinyanganya kura nyingi,
ccm ni chaka la weziu tu,ni dhahifu na imeaza kukosa cha kuwaambia watu...
 
TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,697
2,000
Nashauri nguvu tunayoitumia kuvijadili vyama vya siasa, basi tuielekeze kuelimishana na kuwaelimisha wananchi wenzetu juu ya kuzitambua haki na majukumu yao ya msingi na kuyasimamia na kuyatekeleza kwa maslahi mapana ya nchi.

Vyama vya siasa vitapita, lakini nchi itabaki..
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Mwenyekiti atahutubia hivyo hivyo hata akiwa kwenye machela ili mradi pesa ipo tena bilions za kutosha toka ESCROW sasa ya nn tuwe na hofu ya UKAWA,wakati watanzania wenyew wanapenda rushwa sana,tuko tayar kununua kura ya mtu yeyote hata ya mbowe ikibidi
atahutubia kwenye machela kama hosni mubarak
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,225
2,000

Warioba kapigwa,salim ahmed salim yuko kimya,mkapa yuko kimya,nchi inafanana na kuku aliyekatwa kichwa,haina mtu wa kutolea majibu masuala ya kitaifa.Safari hii wapinzani washindwe wenyewe kwa kuwa ni CCM ambayo imetoa mwaka mzima wa kampeni na elimu kwa umma kwa kuanzia sasa kwenye chaguzi za mitaa,kampeni za bunge la katiba,kura ya maoni,escrow,operesheni tokomeza,mchakato wa uchaguzi na mengine mengi yatasaidia wapinzani kuibana vilivyo CCM na kuinyanganya kura nyingi,

Kwa Kilicho mpata kule ARUMERU hakika hawezi kurudia SIASA, ama sivyo aje atuieleze ni nani AlieyeMUUA BABA WA TAIFA.
 
wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
6,737
2,000
Mwenyekiti atahutubia hivyo hivyo hata akiwa kwenye machela ili mradi pesa ipo tena bilions za kutosha toka ESCROW sasa ya nn tuwe na hofu ya UKAWA,wakati watanzania wenyew wanapenda rushwa sana,tuko tayar kununua kura ya mtu yeyote hata ya mbowe ikibidi
kununua kura, wagombea na ht kununua tume ya uchaguzi kwa watawala wa ccm inawezekana !.

Hakuna lisilo na mwanzo au mwisho.
 
Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,910
2,000
CCM imeshakufa kisiasa maziko yake 2015 watanzania hawawezi kuchagua tena hawa wezi wa ccm tena bado tunataka ccm warudishe pesa zetu Escrow..
 
Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,617
2,000
Wangapi humu mmejiandikisha kupiga kura uchaguzi ujao wa serikali za Mitaa?
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,825
2,000
CCM ya Leo Ni dhaifu kweli,kashfa Kila Kona,wananchi wamechoka na kukata tamaa na wanasiasa na siasa za Tanzania......pamoja na udhaifu wa CCM kazi bado Ni kubwa maana tunaojua madhaifu ya CCM hatupigi kura kazi yetu Ni kushinda humu JF na kujiridjisha kuwa CCM imechokwa...........ningefurahi kama Kila atakayechangia hapa kwenye huu uzi aseme kama amejiandikisha uchaguzi serikali za mitaa ili tujifariji kuwa kweli CCM 2015 inatoka madarakani.......mimi nimejiandikisha.
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Inawezekana ccm ni dhaifu kweli lakini upinzani ni mfu
funguka mkuu,inakuwaje hawa wafu wanatishia kuiangusha serikali mpaka inafikia hatua ya kuomba muafaka ili waziri mkuu asidondoshwe? inawezekana upinzani umekuwa mzimu ambao kwa imani zetu sisi washirikina wa msata,bagamoyo,mzimu huwa haufi
 
thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,344
2,000
CCM imeshakufa kisiasa maziko yake 2015 watanzania hawawezi kuchagua tena hawa wezi wa ccm tena bado tunataka ccm warudishe pesa zetu Escrow..
Ingekuwa maneno ya mitandaoni yanaua chama CCM ingeshakufa kweli, wananchi ndiyo wanajua umuhimu wa CCM kuliko hiki chama cha REGINALD MENGI na MTEI
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom