William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
- Thread starter
- #321
Wazee kama Butiku wanafaa sana kuwa washauri kwa Rais aliye madarakani. Kinachowafanya wawe na ujasiri wa kuongea bila woga ni uzoefu na uelewa wao kwa kina kuhusu masuala ya Serikali. Inasikitisha sana kuona jinsi ambavyo viongozi wanaokuwa madarakani wanavyowapuuza wazee kama wale waliokuwepo kwenye lile Kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere. Wazee wale na wengine ambao wameishakuwa viongozi wa nchi hii katika ngazi mbalimbali wanao uzoefu wanajua lipi jema na lipi baya kwa nchi yetu. Wakizungumza kwa ujasiri wanazungumza kwa manufaa ya Taifa na si kwa manufaa yao binafsi. Sidhani kwamba mtu kama Mzee Butiku, Mzee Lusinde, Mzee Mwakawago, Mzee Salim, Mzee Warioba au mtu kama Mzee Msuya na wengine wa aina yao, wanaweza wakaweka maslahi yao mbele kuwaza kuwa na agenda ya kutaka u-Rais wa nchi zaidi ya kuangalia mustakabali wa Taifa letu!!
Hata hivyo, wakigombea u-rais wanaweza kuwa marais wazuri sana kwa sababu wanajua nchi yetu inahitaji nini. Kama Mwai Kibaki ni Rais kwa nini isiwe wao?
- Mkuu heshima mbele sana, Unayosema ndiyo hasa ninayosema kwamba wa-Tanzania hatuwezi kuwapuuza hawa Butiku na Quaresi, kwa sababu wananchi wengi tunaonekana kushindwa kuelewa the impact of what they did hasa politically, ukweli ni kwamba wamem-bring down to his knees Rais wa jamhuri yetu.
- I mean huyu Rais kila analoshauriwa na tuliowapa dhamana za uongozi kitaifa hataki kuwasikiliza, wabunge wakimshauri hataki kusikia lakini get this, safari hii amewasikia hawa wawili na kujibu tena kwa hasira sana na hata kuvunja safari yake ambayo alijigamba sana kwamba haina mbadala lazima atenda Denmark, sasa hatuwezi kuwachukulia lightly hawa Butiku na Quaresi!
- Wamesimama na kuhesabiwa tena katika hiki kipindi kigumu sana kujua nani ni nani kutokana na zile tabia zetu wabongo za ukinyonga, ninasema hawa wawili Butiku na Quaresi ni lazima wasimame kugombea something politically, tena Nationally, watu kama Jasusi mlio karibu na hawa wastaafu wetu tafadhali wapeni moyo kwamba kuna wananchi tunaoheshimu mchango wao na tunadhani wanastahili uongozi tena, maana kama ndio hivi ni afadhali twende na wastaafu, kuliko damu mpya inayoogpa kusimama na kuhesabiwa!
- Ni ushauri wangu mdogo na wa bure tu!
Respect.
FMEs!