Elections 2010 Uchaguzi 2010: ITV sasa imekuwa chombo cha CCM?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Leo katika kipindi chake cha mapitio ya magazeti cha 06.50am asubuhi, kituo cha television cha ITV kinachomilikiwa na IPP Media kilifanya tukio ambalo sikulitegemea kwa kwa kituo hicho kinachojinadi ni cha makini.

Twajua kwa muda mrefu huwa hakipitii magazeti ya New Habari, lakini mengineyo yote huwa kinayapitia. Lakini leo asubuhi magazeti yote yaliyoandika habari za ukweli kuhusu tukio la jana la kudondoka jukwaani kwa JK hayakupitiwa. Magazeti yaliyopitiwa na kusomwa vichwa vyake vikuu vya habari vya mbele ni Nipashe, Habari Leo, Guardian, Sunday News, ambayo hayakuwa na habari ya tukio hilo kurasa za mbele.

ITV wanaficha nini? Kwa nini wanaficha ukweli? Mimi sillamikii sana kwa magazeti ya IPP kukosa kuandika habari za tukio hilo kurasa za mbele – lakini basi kituo hicho kingeruhusu watazamaji wapate habari za tukio kutoka kwenye magazeti ya wamiliki wengine.

Kwa upande mwingine nawapongeza Channel Ten katika kipindi chao cha mapitio ya magazeti leo kwa kuyapitia magazeti yote, pamoja na yale yaliyoandika habari za tukio kurasa za mbele. Magazeti haya ni Mwananchi, Majira, Tanzania Daima, Mtanzania na mengineyo.

Jirekebisheni ITV kwa kusema ukweli hasa katika kipindi hiki cha kampeni. Tuna wasiwasi mnaweza kufanya kama ya 1995 mlipoleta picha za mauaji ya Rwanda kutisha wananchi wasichague upinzani.
 
Nimeamini nchi hii imejaa MOSTERS MAMFIA hata kwenye vyombo vya habari
leo asubuhi katika taarifa zao za habari hakuna aliyetangaza afya ya Rais wetu
wanatangaza juu bila kutoa maelezo ya uhakika kama uandishi wao ndo huu wa kuganga NJAA KWELI TANZANIA HAKUNA WAANDISHI WA HABARI.

wakati wa kusoma magazeti TBC1 walikuwa na magazeti yote likiwemo TANZANIA DAIMA ambalo limeandika ukweli kuhusu afya ya JK alivyozilai JANGWANI, lakini cha kushangaza hili gazeti alikusomwa kokote

JE MAFIA WA HABARI NDO WAKO ITV NA TBC1?
 
ITV NA TBC1 wamefanya the same magazeti yaliyoandika habari za kuzilai kwa jk hayakusomwa
HAPA KUNA MAMONSTER MAFIA YANAYOTAFUNA HABARI ZA UKWELI
 
Hata mimi ilinishtua kwani nilikuwa nasubiri Tanzania Daima
 
Hata wakificha vipi habari zimeenea sehemu kubwa, jana tu tulioko mikoani tulizipata ndani ya dakika 10 tangu aanguke. Kadri wanavyoficha ndio watu hujadili zaidi.
 
Mimi Jana nilijitahihidi kuangalia taarifa za habari karibu kila station ya TV lakini hamna hata mmoja ilionyesha rais akianguka na kutoa taarifa kwa wananchi walio mpa dhamana ya kuingia ikulu. kila TV station ilizungumza ufunguzi / uzinduzi waa mafanikio wa kampeni za CCM jangwani. so kwao hiyo haikuwa news na wala si news, news ni uzinduzi wa kampeni bila kuanagalia huyu anaetaka achaguliwe tena afya yake iko vipi?

Yaani Tanzania na nchi za afrika ovyo kabisa. Naamini kwa asilimia mia angekuwa ni Dr Slaa au mpinzani mwingine kwenye TV stattion na magazeti yote hiyo ndo ingekuwa news na siyo uzinduzi wa kampeni
 
TBC walisema tu, kuwa raisi alipata muda kidogo wa kupunzika kabla ya kuendelea tena, ni aibu ya mwaka kwa vyombo vya habari kushindwa kutangaza habari za ukweli
 
Ndo maana Tanzania Daima huisha mapema kwa kugombaniwa na wasomaji. Nipashe sasa hivi inazidi kudidimia kimauzo na karibu tutaona yanaanza kuuzwa kwa kilo kama vile yale ya Habari Corporation.
 
ITV -- itawasaidia nini mnapoficha ukweli? Sana sana mtaanza kutazamwa kwa shuku kubwa. Media House kubwa kama hiyo inaficha habari? Sikutegemea kabisa kutoka kwenu, I really didn't.
 
sometimes tunawalaumu bure....

hizo ni directives wamepewa na wakaidi waone

saa mbaya hizi
 
Hell with ITV, hell with Tido Mhando TV! You all dont have independence and intergrity to be National Stations. Give us a break and learn from Citizen TV hapo nyumba ya jirani!
 
Naomba kuuliza, hivi jana vyama vingine havikuzindua kampeni?
Mbona sijaona kwenye chombo hata kimoja cha habari kwenye mtandao vilkizungumzia uzinduzi wa kampeni wa CUF, CHADEMA wala vyama vingine?
Hata hapa JF.
 
Binafsi nilidhani kuwa hivi vyombo vya habari vipo independent na jukumu lao kubwa ni kusema ukweli wa mambo kama ulivyotokea bila ya kupindisha maneno. Sasa naamini IPP media na iyo TBC wapo kwa masilahi yao binafsi zaidi kuliko ya umma. Kuanzia leo sitonunua gazeti lolote kutoka IPP media. Mda mwingi niliacha kusikiliza radio one manake haina kitu kipya tena, ni mambo yale yale miaka nenda miaka rudi, kumbe sera hizo pia zipo kwenye TV na magazeti yao, mie sitaki kuwapa support ili watimize malengo yao ni kheri kustick na magazeti yanayosema kweli, kama raia mwema kuliko kuwa mhusika wa maslahi binafsi.
 
Hivi vyombo vya habari vimenunuliwa na CCM na ndio maana wanakuwa na ubaguzi katika kutoa habari!
 
Naomba kuuliza, hivi jana vyama vingine havikuzindua kampeni?
Mbona sijaona kwenye chombo hata kimoja cha habari kwenye mtandao vilkizungumzia uzinduzi wa kampeni wa CUF, CHADEMA wala vyama vingine?
Hata hapa JF.
Kila chama kina ratiba yake ya uzinduzi, jana walikuwa ni CCM, wengine fuatilia kuanzia leo watazindua
 
Habari zilikuwa ni Dr Slaa avunjika mkono, Dr Slaa alazwa Muhi2 ! Hizi zilisomwa vizuri tu na TV na magazeti kwa kuwa zilikuwa habari.

Nilifikiri ni mimi tu nilikuwa nikisubiri kujua kuhusu afya ya mgombea na nimetoa macho kwenye Tv sikuona kitu.

Kuna mengi mbele ya kuona kwa vyombo vyetu vya habari hasa katika kipindi hiki cha uchafuzi mkuu!
 
What is happening to the President ... is almost taking place in most of Tanzanians.... Tunasaidiana kuficha.Tumezoea kuficha ficha kila kitu, hata visivyofichika !!!!! What a shame!!!! Lakini for how long ...? Rais wa Nigeria ilikuwa hivi hivi...Mpaka ikapelekea mzozo wa kiuongozi...For a President who loves his Country and Its people.... He should simply stape down!! .... AMUACHIE MTU MWENYE AFYA TIMAMU !!!!
 
KITAKIWACHO NI UKWELI NA UWAZI...KAMA KURIPOTI YARIPOTIWE YOTE BILA KUCHUJA WALA KUCHEKECHA.......sasa jana UWANJA ULIJAA SIO KAWAIDA.........NA MAMA MPENDWA MARIA NYERERE MKE WA RAISI WA KWANZA NA KIPENZI CHA WATANZANIA..ASIYE NA PAPARA WALA KIMBELEMBELE ALIKUWEPO ...!.....NILIMUONA AKISALI SANA MAMA HUYU MCHA MUNGU...!
 
Leo katika kipindi chake cha mapitio ya magazeti cha 06.50am asubuhi, kituo cha television cha ITV kinachomilikiwa na IPP Media kilifanya tukio ambalo sikulitegemea kwa kwa kituo hich kinachojinadi ni cha makini.

Twajua kwa muda mrefu huwa hakipitii magazeti ya New Habari, lakini mengineyo yote huwa kinayapitia. Lakini leo asubuhi magazeti yote yaliyoandika habari za ukweli kuhusu tukio la jana la kudondoka jukwaani kwa JK hayakupitiwa. Magazeti yaliyopitiwa na kusomwa vichwa vyake vikuu vya habari vya mbele ni Nipashe, Habari Leo, Guardian, Sunday News, ambayo hayakuwa na habari ya tukio hilo kurasa za mbele.

ITV wanaficha nini? Kwa nini wanaficha ukweli? Mimi sillamikii sana kwa magazeti ya IPP kukosa kuandika habari za tukio hilo kurasa za mbele – lakini basi kituo hicho kingeruhusu watazamaji wapate habari za tukio kutoka kwenye magazeti ya wamiliki wengine.

Kwa upande mwingine nawapongeza Channel Ten katika kipindi chao cha mapitio ya magazeti leo kwa kuyapitia magazeti yote, pamoja na yale yaliyoandika habari za tukio kurasa za mbele. Magazeti haya ni Mwananchi, Majira, Tanzania Daima, Mtanzania na mengineyo.

Jirekebisheni ITV kwa kusema ukweli hasa katika kipindi hiki cha kampeni. Tuna wasiwasi mnaweza kufanya kama ya 1995 mlipoleta picha za mauaji ya Rwanda kutisha wananchi wasichague upinzani.
Mkuu...
msomaji wa ITV anapokuwa studio hayuko huru.... macho yake huwa anapepesapepesa kwa woga kuona kama Mengi yupo karibu...
 
Back
Top Bottom