Uchafu wa st.john university adharani.

Uchafu wa st.john university adharani.

Nashawishika kuamini hizi taarifa cyo za kweli. SJUT kuna faculties/schools 6. Lakini naona maelezo yako yamebase FOCB tu. Sasa utasemaje chuo kifungwe kwa matatizo ya faculty moja?? Usidanganye watu kwa taarifa ambazo hazijakamilika bana. Usipoteze muda wako kaka. Jipange upya utuconvince.
 
Du Dunia ina raha zake wakati watu wengine wanalia wengine wanacheka haki ukiitaka duniani basi hata kufa ugome maana hutaipata.
 
kiingereza kibovu, ungetumia kiswahili ungeeleweka vizuri.
 
Ulichokiandika si habari ni hali halisi vyuoni kifupi ndio academic lifestyle ya vyuo vikuu vyote kwenye viinchi corrupt kama tanzania, sijui nani atanunua hii habari
 
Nilisoma pale,mengi yaliyoandikwa ni ya kweli na tatizo kubwa hao walimu wasio na sifa ni watoto wa vigogo wanaoishikilia chuo.Mfano huyo alotajwa Allen mtetemela ni tatizo kubwa kwanza hana sifa za kufundisha chuo pili hutofautiana sana na wanafunzi kwa kuwalazimisha watoto wa kike mapenzi.katika kipindi chetu ndie aliyempora Madee msanii demu wake,pendo sasa hv dada huyo ni marehemu.Mtetemela ni mtoto wa Askofu wa anglicana mwenye ushawishi mkubwa katika chuo hicho
 
cc: fluphenazine soma vizuri kwenye eneo la red halafu ndo urudi tena....THE SPURIOUS SJUT PROSPECTUS
We must face the truth that so far the St. John's University of Tanzania does not qualify to be called a university, because apart from all the shocking mess the university is mostly staffed b unqualified bread hunters.
The university does not have a single teaching professor, as the Vice chancellor himself is a misallocated medical teacher, occupying the place of seasoned educationist professors who would have propelled Saint John's university of Tanzania to the peak of academic excellence and intellectual prestige, replica of the light to the world by fellow Anglican universities which brought that historical mission to Central Africa. This administrative with acute deficiency in charisma and moral integrity.
The St.John's university of Tanzania has a roll of about 6000 students altogether, but for all of who it has only one associate professor, with most of the rest of the teachers being unqualified to teach in a university at all! For example the faculty of Commerce and Business studies is wont to using students who pursue Masters Degrees as senior lecturers, capacities which they are incapable of and which consequently breed the disharmony between the teachers and the students. Notable examples are;
a. Student Wilfred Kavishe who is per suing a Master's degree course is teaching Financial Report as a Senior lecture
b. Student Misu Chibona is wrongfully relied upon as Senior Lecturer in Business Mathematics!
c. Student Herman Dobogo who is per suing a Master's degree course which he has failed was a Senior Lecturer in Marketing!
d. Allen Mtetemela is a notorious tutorial assistant, but who has for four (4) years now wrongfully been a Senior Lecturer in Business Law!
e. Student Chrispin Ryakitimbo has also been offered to masquerade as Senior Lecturer in Accounting!
f. Student Anthony Magoma was per suing a Master's degree course which he failed, but was offered to teach Mathematics and Masquerade as a Senior Lecturer!
These are just few of the examples and are from only one faculty, Commerce and Business studies which practically has only one Senior Lecturer and only Five assistant lecturers, the best being either teaching or tutorial assistants, who the university has been using them as Senior lecturers. Because the senior Lecturers and assistant Lecturers are the same executives enjoying administrative designations which make it difficult for them to teach, so they leave the teaching for the Master's students, who frankly speaking lack the capabilities and resort to threats to cow down the students and sexual coercion to female students.
 
Serikali inabidi iwe makini sana na hivi vyuo binafsi, tukichemsha elimu ya juuu basi tusitegemee miujiza ya kujikomboa kiuchumi kamwe!! TCU mpoooo????
 
Nilisoma pale,mengi yaliyoandikwa ni ya kweli na tatizo kubwa hao walimu wasio na sifa ni watoto wa vigogo wanaoishikilia chuo.Mfano huyo alotajwa Allen mtetemela ni tatizo kubwa kwanza hana sifa za kufundisha chuo pili hutofautiana sana na wanafunzi kwa kuwalazimisha watoto wa kike mapenzi.katika kipindi chetu ndie aliyempora Madee msanii demu wake,pendo sasa hv dada huyo ni marehemu.Mtetemela ni mtoto wa Askofu wa anglicana mwenye ushawishi mkubwa katika chuo hicho
Demu wa Madee aliporwa kinguvu au alitongozwa?
 
Duh hiki kituo cha tuition cha St John ni noma.
 
nimeisoma na kuielewa....ila sitaki kuamini yote koz simjui aliyeandika....siku hizi elimu ni ushindani...na watu wana chuki binafsi, wako tayar kufanya lolote kuharibu kwa wengine..na ningemjua aliyeandika, ningemuuliza, amekwishachukua hatua gani baada ya kuyajua hayo yote??
na mwandishi amejipa mamlaka ya mwisho ya kuamua muoneaji na muonewa...bila ya kuskiliza pande mbili...kwa mimi niliyefanya tafiti mbalimbali nchini na kwingineko, nina uhuru wa kusema, the report and its findings are biased and one sided...yenye mlengo wa kusema mabaya ya st.john na staffs wake, bila ya kusikiliza pande ya pili....

That's real, umeongea la maana sana!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
CC: Gad Oneya:acheni siasa zisizo na mantiki, tuliokoe hili Taifa linalopoteza dira katika elimu..



]MY ADVICE:
jambo hili si lakulichukulia mzaa sababu " issues that are written hold water"..
 
Kwa taarifa niliyonayo ni kwamba leo hii mleta mada ambaye alikua Rais wa wanafunzi yupo kikaangoni mbele ya jopo la wachunguzi ndani ya chuo cha St. John.

Vivyo hivyo leo hii timu maalumu toka TCU imetia timu chuoni hapo kwa uchunguzi mahususi juu ya nini kinachoendela chuoni hapo.

My advise St. John kinahitaji muda wa kujiandaa kufundisha shada ya uzamili maana kiukweli hawana qualified waalimu wa kufanya kazi hiyo kwa sasa wahangaike na Undergraduates pekee. Pili watenge fedha za kutosha na kutafuta wafadhili ili wapeleke waalimu wao vyuo vya ndani na nje ya nchi kufanya shahada za uzamivu ili kukidhi mahitaji yao angalao kwa kila fani kuwe na angalao Senior Lecturer mmoja.

Huu ndiyo mtiririko madaraja ya wahadhiri katika vyuo vikuu Tutorial Assistants kazi yao ni kusimamia Seminars na mitihani tena Lecturers na seniors wakiwa pembeni yao maana hawa wanakua na Shada moja tu, Assistant Lecturer ana kua na Shahada la pili (Masters) Lecturer anakua na shahada ya tatu (PhD) ila hana uzoefu na hajafanya publications za kutosha au kwa maana nyingine hajaiva vya kutosha, Senior Lecturer anakua na PhD na Uzoefu Mkubwa pamoja kufanya machapisho ya kutosha; Associate Prof. anakua na PhD na uzoefu wa muda mrefu na amefanya machapisho kadhaa, ushauri wa kitaaluma, book chapters, publish in International and local Journals in his/her area of interest na conference proceedings. Full Professor anakua na PhD, ametoa vitabu kadhaa, amefanya ushauri wa kitaaluma kwa wingi, conference papers, publish in International and local Journals in his/her area of interest nk. Ili kupanda madaraja inategemeana na sheria na taratibu/vigezo vilivyowekwa na kubaliwa na Senate na Baraza la chuo husika.
 
Kikubwa mshauri mdogo wako asome kwa bidii achaguliwe udsm chuo cha wanaojielewa
 
cc: Spleen, acha kufikiri kwa kutumia makalio, TCU wanabidi wafanye maamuzi hata ya kiwa magumu kiasi gani ili watoke kwenye lawaama... Rushwa ni adui wa maendeleo, hili swala lishakua kubwa sana,wa Tanzania wengi washalifahamu kiasi cha kwamba wanabidi wawe makini sana kwa maamuzi watakayo ya chukua...
When it comes to students,i can say all of them are just like a bread but it depends what do you put in between that bread
 
cc: Spleen, acha kufikiri kwa kutumia makalio, TCU wanabidi wafanye maamuzi hata ya kiwa magumu kiasi gani ili watoke kwenye lawaama... Rushwa ni adui wa maendeleo, hili swala lishakua kubwa sana,wa Tanzania wengi washalifahamu kiasi cha kwamba wanabidi wawe makini sana kwa maamuzi watakayo ya chukua...

well said mkuu#
 
For that case, its we have students lect..students right? Then we call it a Univ....!?Well it mighty be but let see what will come out of it. This is pretty secrious guyz
 
Madudu mengine ya St. John tawi la St. Marks-Dar campus adharani...


faida ya wenye simu:


KWA: VICE CHANCELOR ST.JOHN'S UNIVERSITY OF TANZANIA DODOMA

KUTOKA: KANUTI MTIMALY ASY-AFISA RASILIMALI WATU (HRMO) ST MARK'S

Awali ya yote nipende sana kuchukua nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutujalia kuendelea kuwa na afya njema inayotufanya tuweze kufanya kazi zake za utoaji wa huduma halali hapa duniani kwa ujumla.

Vice Chancelor, napenda kuchukua nafasi muhimu kwako kutoa taarifa rasmi inayohusiana na mwenendo mzima wa utendaji usioridhisha katika chuo cha St. Marks Centre ambacho wewe mteule ulipata Baraka za kila aina kutoka kwa Maaskofu wa wadau mbali mbali kukiongoza chuo hiki kutokana na sifa ulizonazo na umahiri mkubwa wa kitaalama.



Nipende kushawishika kwa kusema kuwa baada ya uteuzi wa kipekee uliopata sisi sote kwa ujumla tuliochini ya St. John's university tulikutegemea sana kuwa utafika katika kituo ch St. Marks centre ili nasi tukufahamu, tukukaribishe, tukuelekeze matatizo yetu, napia tuweze kukupa pongezi kwa uteuzi huo muhimu kwako binafsi na kwa Kanisa Anglicana Tanzania.


Taarifa nilizonazo ni kwamba ulipita mara moja tu na kusalimiana na viongozi na wanafunzi wachache kitendo ambacho mpaka leo hii unapoisoma taarifa hii wafanyakazi wote wa St. Marks centre tuna shindwa kujielewa au hata kukuelewa wewe binafsi jinsi ulivyoweza kutuweka kando sisi wafanyakazi centre nzima kwa ujumla wake.


Vice chancellor, na hakika na utaratibu wako uliojiwekea hususani wa kupokea matatizo makubwa au hata madogo kutoka vituo vilivyo chini ya St. John University ndio maana nimeonelea ni vyema kuchukua maamuzi haya magumu kukuandikia moja kwa moja. Labda niombe radhi za kabla endapo hilo utaliona kuwa ni kinyume na utaratibu wako.


Vice Chancellor, Kituo kimekuwa na mlolongo wa matatizo makubwa ya kiongozi na kiutendaji mara tu baada ya wazo hili kubuniwa na kuibuliwa na Maaskofu wa Anglican Tanzania kuwa na chuo kikuu chini ya kanisa la Anglicana hapa Dayosisi ya Dar-es-salaam.


Aidha mtazamo mkubwa zaidi wa Maaskofu ulikuwa kutoa Elimu ndani ya jamii bila kujali dhehebu la mtu, rangi na hata ukabila na spirit hii ndiyo inayoendelea hadi hivi sasa. Aidha, utakubaliana na mimi kuwa hata wao Maaskofu wameweza kujiweka kando kidogo kwa nafasi ili pasitokee aina yoyote itakyowahusu wao katika maswala ya utoaji wa huduma, na pale panapojitokeza kwa aina yoyote ukengeukaji wa maadiliutaratibu umewekwa chini ya ofisi ya chapline kuweza kutatua matatizo ya kiroho kwa wafanyakazi na wanafunzi ila si kwa matatizo ya tabia za viongozi kiutendaji na kiutendaji na kiongozi ikiwa na maana Vice chancellor ndiye mwenye jukumu na mamlaka katika kuchunga kondoo.


Vice chancellor, nikukumbushe kuwa Muungano halali wa kukiunganisha kituo hiki kitaaluma ulifanyika ikiwa ni pamoja na kufuata utaratibu mzima unaotumika na Serikali ya Jamhuri ya muungano Tanzania chini ya chombo chake kiitwacho TCU ambacho ilikilazimu kituo cha St.marks kufunya mabadiliko makubwa ya uongozi kwa ngazi mbalimbali kulingana na sifa stahili za kitaaluma. Hatua hii iliweza kuondoa wale wote ambao hawakua na sifa zinazostahili kwa nafasi walizopewa. Aidha baadhi ya walimu waliweza kusitishwa kwa ajira zao majina ya wote ambao ajira zao zilisitishwa yamehifadhiwa ili kukuthibitishia hili. Ushaidi upo


Vice Chancellor,kwa masikitiko makubwa sana napenda kukujulisha kuwa tabia hii ya kuwateua na kuwaweka Viongozi wasio na sifa Zinazotakiwa na TCU katika nafasi/post zinazohitaji elimu ya PhD zimekuwa zikiendelea kwa makusudi hapa St. Marks centre huku wewe binafsi ukilifumbia macho sula hili. Kwa mfano nafasi ya ukurugenzi wa mipango na fedha kwa makusudi kabisa inashikiliwa na mtumishi ambaye hana sifa za Phdna sioni kama kuna jitihada zozote za kutafuta mtu mwenye sifa stahili sababu ni muda mrefu nafasi hii imekuwa ikikaimiwa bila sababu ya msingi. Ushaidi wa suala hilo upo.


Aidha nipende pia kushawishika kuwa inawezekana kabisa uteuzi wa kaimu Mkurugenzi wa Mipango wa fedha tuliye naye hapa St. Marks hakuwa umekidhi vigezo na sifa za kuhamishiwa hapa St.Marks kushika nafasi hii. Pia nipende kufikiri zaidi kuwa hata utumishi wake hapo ST John's si wa muda mrefu licha ya sifa za nafasi ya kaimu Ukurugenzi aliopewa inawezekana uteuzi huu ulikuwa haukuzingatia suala la utumishi wa angalau muda mrefu ndani a chuo chako hapo St john's nashauri ukalitazame vizuri suala la uteuzi ili uweze kujiridhisha kwa vigezo na sifa za mhusika.


Vice Chancellor, katika hali halisi picha hii inaonyesha dhahiri kuwa kituo cha St Marks umekipa kisogo bila kutambua nafasi uliyonayo katika hiki huku kikiburuzwa na migongano mingi ya kiutendaji ambayo kwa utabiri wangu kamwe haitaweza kumalizika bali kitachoendelea chuki kati ya viongozi na wafanyakazi.


Vice Chancellor, nina hakika kabisa kuwa unafahamu wazi kituo cha St Marks bado hujakipa kipau mbele kupata kiongozi au viongozi wanaostahili hususani kwa nafasi ya CENTRE DIRECTOR na mkurugenzi wa mipango na fedha ( DEPUTY DIRECTOR PLANING & FINANCE) je hali hii itakuwa mpaka lini? Je utakuwa tayari kuacha kituo hichi kiwa na baadhi ya viongozi wasio na sifa za kielemu ( PhD holders) katika nafasi za ju?, je ki taaluma kituo hiki kitajikita wapi katika ushindani wa kielemu hapa Tanzania, Aidha dhana hii ya kutoshughulukiwa kwa matatizo ya sifa za kielemu kwa viongozi kinaweza kuwaweka viongozi wetu wa kiroho yaani Maaskofu kuvunjika moyo wa kuona kituo hiki hakitendewi haki.



Vice chancellor, ufumbiaji macho wa matatizo ya kituo hiki cha St. Marks hivi sasa umekipa taswira isiyotazamika miongoni mwa wafanyakazi wote kuanzia walimu ( academic staff) na wafanyakazi wa kawaida ( supporting staff) na wakati mwingine kujuta kujiunga nasi kutokana na vitendo vya mabavi visiyozingatia taratibu za kazi kwa kiasi cha hali ya juu kabisa.


Vice chancellor, kwa tabia hii na mwenendo huu usiompongeza mungu kwa waja wake mimi binafsi bila kushawishiwa na mtu yeyote hapa St. Marks nimeamua kukufahamisha vitendo ambavyo kwa namna yoyote haviwezi kuachiwa viendelee kufanyika ndani ya kituo hiki bila kukujulisha wewe binafsi na kutoa taarifa pia kwa Maaskofu ambao ndiyo wenye dhamana kubwa ya chuo hiki.




Vice Chancellor, kumekuwa na ukiukwaji mkubwa na udhalilishaji wa kitaaluma wa makusudi unaofanywa na kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Fedha na hivi sasa idara ya rasilimal watu (Human resource Mgt) imekuwa ikipuuzwa kwa majukumu yake mengi ya kila siku.


Kufanywa na ofisi isiyohusika. Kwa Mfano, hivi sasa utaratibu mzima wa utoaji wa barua za uthibitishwaji wa wafanyakazi wapya umekuwa ukifanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa mipango na fedha.

Kitendo hiki kimeleta migongano mikubwa sana hapa St. Marks kwa sababu taratibu nyingi na sheria za kazi zimekiukwa kutokana kazi husika kufanywa na ofisi isiyohusika kwa makusudi na bila kupata ushauri kutoka ofisi ya HR au Mshauri wa Kisheria aliyeopo chuoni.


Kitendo hiki tayari kimeshaashiria kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wameachishwa kazi bila ya kuzingatiwa kwa sheria za kazi kuanza kutafuta haki katika taasisi mbalimbali za kisheria hapa nchini, na kimtazamo halisi kesi hizo hazitakuwa na picha nzuri kwa St John's university pamoja na kanisa la Anglicana Tanzania kwa ujumla.



Vice Chancellor, ubabe na mabavu yanayoendelea kutumika kwa wafanyakazi bila kujali rika na hekima imepelekea barua mbalimbali zenye lugha mbaya zisozokuwa na heshima na kiungwana na zenye aina uzalilishaji kuandikwa baadhi ya wafanya kazi ambao ni waalimu. Kitendo hiki kimeamsha malumbano ya chini kwa chini hapa chuoni bila sababu ya msingi wowote. Ushaidi wa suala hili lipo.



Vice chancellor, mimi binafsi niseme kuwa nimepata bahati pia ya kupitia vipindi vyote vya Uongozi ambavyo vimekuwa vikipokezana vijiti hapa St. Marks na katika maamuzi niliyokuwa nikiyashuhudia kwa macho yangu ni kufutwa kwa taratibu mbalimbali za kiutendaji na kuheshimiana miongoni mwetu sisi wafanyakazi na viongozi waliopo kwa wakti huo.

Cha ubabe na makusudi utaratibu wa kupata Kampuni ya ulinzi hapa chuoni Kimsingi tulipaswa kufanya ushindanishi wa makampuni mbalimbali ili kupata kampuni iliyo bora na makini na kwa utaratibu wa wazi zaidi. Kilichotokea ni kwamba bila kuzingatia utaratibu wa ushindani Kaimu Mkurugenzi wa mipango na fedha ameamua yeye binafsi kuipa nafasi kampuni hiyo ya Tell security bila ushindani wowote.


Aidha, ilitegemewa kupata Kupata kampuni yenye gharama nafuu zaidi baada ya ushindani kufanyika. Kilichojitokeza kwa makusudi chuo kiniaingia ya kulipia hiyo huduma ya ulinzi kwa zaidi ya SHS MILIONI TANO kwa mwezi licha kuweka mazingira ya uzio kwa sehemu kubwa ya chuo. Kitendo hiki kimeleta picha mbaya kwa st. Marks kwa sababu kila mfanyakazi amekuwa akioji ni utaratibu upi uliotumika kupata kampuni ya ulinzi ya kufanyika kwa ushindani. Ushahidi wa suala hili upo.



Vice Chancellor, hivi sasa kituo cha St. Marks kimekuwa kikikiuka makusudi suala la kuipa kipau mbele Idara ya uhasibu ambayo ndiyo yenye dhamana kubwa ya kudhibiti matumizi ya fedha za chuo na serikali.


Kaimu Mkurugenzi wa mipango na fedha kwa makusudi ameweza kumuhamisha mfanyakazi kutoka idara ya uhasibu na kumpeleka idara ya ukutubi ( LIBRARY) kwa kigezo kuwa kituo kimeongeza mtandao wa kazi hivyo muhusika huyu itamlazimu kufanya kazi za kiuhasibu akiwa library. Napata shida sana kulielewa suala hili vizuri kwa kuzingatia kuwa uhamisho huu usio na tija kufanyika yawezekana kabisa kuwa kuna dalili mbaya ndani ya idara ya uhasibu.


Pia mtumishi mwingine ameweza kuachishwa kazi bila kufuata taratibu za kisheria hayo yote yamekuwayafanyika bila ofisi ya HUMAN RESOURCES kushirikishwa. Vitendo kama hivi kimsingi havileti tija katika Taasisi kama hii iliyoko chini ya kanisa. Suala hili Ushahidi upo.



Vice chancellor,Kutokana na ubabe huu unaofanywa na kaimu Mkurugenzi wa mipango na fedha hivi sasa ofisi ya fedha imebaki na wafanyakazi wawili tu ambao kati ya hao mmoja wapo ni ndugu yake ana Diploma ya education ( Mr. Iyunge).


Hivyo basi huyu ambaye ni ndugu wa kaimu mkuu Mkurugenzi ndiye amekuwa Mhasibu mkuu, mpelekaji fedha benki, mlipaji malipo ote ya wazabuni na mambo mengine. Utaratibu wa namna hii unatoa maswali mengi kwa wanataaluma wa masuala ya fedha ndani ya kituo hiki cha St. Marks na inaleta picha isiyo nzuri katika suala la uwajibakaji wa fedha za chuo yawezekana ndugu hawa wanaweza kabisa kufanya kabisa mambo ambayo athari zake zitaweza kubainika baadaye sana na kukosa mtu wa kumchukulia hatua.Suala hili ushaidi upo.




Vice chancellor,kwa masikitiko makubwa nipende kukumbusha kuwa kamati ya kushuglukia mabadiliko ya mishahara ya wafanyakazi iliweza kuundwa hususani kwa wafanyakazi wa St. Marks.


Kamati husika imeweza kufanya kazi yake na hatimaye kufikia kukamilishwa kwa zoezi hilo. Cha kushangaza ni kwamba zoezi hili tangu lilipokuja Dodoma kushughulikia mishahara ya wafanyakazi napenda kukujulisha kuwa Kaimu Mkurugenzi wa mipango na fedha amekuwa akileta migongano mikubwa isiyo na tija kwa wafanyakazi.


Kwa mfano mpaka hivi sasa kuna baadhi ya wafanyakazi ambao wameahidiwa kuwa mishahara yao itakuwa katika uchunguzi kwa muda usiojulikana na maamuzi yatakayofikiwa hayatatakiwa kuhojiwa huku wenzao wakifaidi mishahara hiyo mipya. Ushaidi wake upo.



Tabia hii ina sura ya kukomoana na inaonyesha wazi tabia yenye kila aina ya ukatili kwa wafanyakazi wasio na hatia yoyote kwake na hivi sasa hili swala la mishahara kwa baadhi ya wafanyakazi lilipelekwa ofisi ya RAAWU tawi lakini kaimu Mkurugenzi wa mipango na fedha amekataa katu kutoongea na uongozi wa RAAWU Tawi ambalo liko madarakani kisheria za nchi. Ushahidi wa suala hili upo.



Vice chancellor, kumekuwa na vitendo ambavyo kwa ukweli haviwezi kabisa kumpendeza mungu ambavyo baadhi yetu tumekuwa tukivishuhudia vikifanya kwa hila na kaimu Mkurugenzi wa mipango na fedha kuamua kubadili matokeo ya interview/usaili kwa wafanyakazi ambao wameweza kufanya vizuri na kushawishi kufutwa kwa washindi walioshinda kihalali hususani katika nafasi ya Dean of students hapa St Mark's.


Ki msingi suala hili linanipa taabu sana katika maisha yangu hapa St. Marks kwa vile naamini kabisa mungu aliweza kuwekwa kando na kushindwa kufanya haki kwa mfanyakazi aliyeshinda usaili huo jina limehifadhiwa na Ushaidi upo wa suala hili.



Vice chancellor, yawezekana kabisa taarifa hii inaweza kujaribu kukupa angalau mwenendo wa vitendo vinavyoendelea kufanyika hapa St Marks lakini mimi binafsi napenda kusema kuwa vitendo hivyo havina tija kabisa na kamwe havimpendezi mungu kabisa mimi ndivyo ninavyoamini kwa imani yangu.


Katika hatua za kukiendeleza kituo cha St. Marks michakato mingi imeweza kufanyika na haya ote yalitokana na maelekezo kutoka TCU.


Lakini cha Kushangaza ni tabia ile ile ambayo utoaji wa kazi zote za uzabuni wa ujenzi zimekuwa zikitolewa kwa kampuni moja tu ya BONDENI CONTRACTOR ambayo ililetwa na kaimu Mkurugenzi kuwa mzabuni huyu anapata kazi hata kama ni kazi ndogo. Niseme wazi toka kaimu Mkurugenzi wa mipango na fedha afike hapa St Marks kwa Uhamisho wa ndani tumekuwa tukishuhudia kila kazi ya ujenzi ikifanywa na kampuni hiyo. Hii tabia haileti sura nzuri kwa kituo hiki.


Aidha maamuzi ya mabavu yamekuwa yakitumika kwa wajumbe ambao si wazoefu katika masuala ya ujenzi na kazi nyinginezo. Pia wakati mwingine kamati ya ujenzi imekuwa ikikubali kupitishia au kuipatia kazi kampuni ya Bondeni hata kama kisa cha bei alichowasilisha ni cha juu ikilinganishwa na wazabuni wenzake. Suala hili ushahidi upo katika ofisi ya Estate.



Vice chancellor,katika kukuthibitishia kuwa kaimu mkurugenzi wa fedha na mipango kuendelea kutoijali idara ya Rasiamali watu ( Human Resource Mgt) ameweza kutangaaza nafasi za kazi mbalimbali, ofisi yake kupokea maombi ya waombaji wa kazi hizo, kufanya uchambuzi wa maombi hayo lakini baada ya kuonekana kazi hiyo kuwa kubwa na aliyekuwa akimtumia kufanya kazi hiyo kutokuwa na uwezo ndipo alipoamua kuiwasilisha kazi hiyo idara ya Rasiamali watu.



Huu si utaratibu wa kazi katika chuo kikuu kama hiki tulipo aidha huu ni udhalilishaji wa makusudi kwa idara zinazostahili kufanya jukumu hilo. Ushaidi juu ya sula hili upo.



Vice chancellor,pengine nishawishike kwa kusema kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na fedha tayari alishakuwa na nia isiyo njema kujiamulia kutangaza kazi isiyo stahili kwani baada ya uchambuzi wa mwisho wa majina ya waombaji kazi kufanyika na kuwasilishwa katika ofisi yake aliweza kuongeza jina la mtu ambaye hakuwa ameteuliwa na idara a Rasimali watu ( HR office).


sababu iliyomfanya kuamua kwa mabavu kuliongeza jina hilo ilitokana na sisi idara ya Rasimali watu kumkatalia na kumtaka afuate utaratibu ndipo alipoamua kwa mabavu kuliongeza jina hilo la bintikwa kuandika kwa mkono licha ya majina mengine kuchapwa kwa computer. Je huu ni utawala bora ambao Serikali ya Jamhuri ya Tanzania chini ya Raisi Jakaya Mrisho kikwete unavyotaka? Kukiuka taratibu za ajira kwa kiasi hicho? Suala hili ushaidi upo)


Vice Chancellor, pamoja na mabavu yote hayo yanayokiuka kanuni za kazi na utawala Bora binti huyo aliweza kufanyiwa usaili na jina lake ni miongoni wa majina aliyotumiwa kwako/Human office kwa kupendekezwa kuajiriwa kwa nafasi ya SUPPLIES OFFICER. Isitoshe baadhi ya wajumbe walipinga binti huyo kupendekezwa kwa kigezo cha kukosa sifa a taaluma hiyo kwa vile hakuwa ametambuliwa na Bodi husika.


Aidha Bursor wa St John's MR. F Mayayi aliweza kujaribu kutoa vigezo stahili kwa ajira ya binti huyo lakini jibu lilitolewa na kaimu Mkurugenzi huyo kwamba sifa akiwa katika kipindi cha probations. Ushahidi wa suala hili upo.



Vice Chancellor, TUNU kubwa ya kituo cha St Marks ni kuwa na wafanyakazi ambao wanapaswa kuheshimwa, kuthaminiwa, kusikilizwa japo hata kama mchango wao si mkubwa ukilinganishwa na watumishi wengine cha kushangaza ni kwamba Kaimu Mkurugenzi wa fedha na Mipango kutoa matamshi ya kashfa dhidi yao wakati wanapokua na shida mbalimbali. Baadhi ya matamshi yaliyoweza kutoka katika mdomo wake ni ST MARKS HAKUNA WAFANYAKAZI ILA KUNA WASHANGILIAJI TU ISIPOKUWA WALIMU NA WANAFUNZI TU.


Hii si tabia ya kumpendeza Mungu hata kwa MAASKOFU wenye dhamana ya chombo hiki kwani kila mtu aliumbwa kwa mfano wake iweje mtu mwingine afike hatua ya kutoa kashfa kiasi hicho. Ushaidi upo umehifadhiwa. Nafikiri kiongozi husika alijifunza mengi mazuri kwa wafayakazi ambao leo wanaita washangiliaji tu wakati anaingia hapa St. Marks.


Vice Chancellor, kumetokea malalamiko ya kazi ya ujenzi wa uzio ( fance) malalamik ambayo yaliweza kuwahusisha baadhi ya wafanyikazi kuwa gharama iliyotumika kujingea uzio huo ni kubwa, Aidha wafanyakazi husika waliitwa kwa mahijiano ambayo yaliweza kuhusisha CHAPLINE wa chuo.



Kwa mtazamo wangu ni kwamba ilikuwa ni namna tu ya kumsafisha Kaimu Mkurugenzi husika kwasababu kilichotakiwa ni kufanyika kwa uchunguzi wa kina kutoka kwenye vyombo vyenye taaluma ya ujenzi na si kumsafisha mtu. Kitendo hiki kimeleata chuki kubwa miongoni mwa wafanyakazi husika.



Stahili kama hii ya kusafishana haina tija bali ni kuona mtu mmoja akihutumiwa kutimia fedha za serikali isivyo stahili.


Nipende kushauri ofisi yako kulipa kiupambele suala hili kwa vile lina mianya ya sura isiyopendeza kiutendaji. Wafanyakazi waliohusika na sakata hili wapo hadi hivi sasa bado hawaelewi hatima yao.


Vice chancellor, Nafikiri utakubaliana na mimi japo kwa upande mmoja wa maelezo yangu kiwa hivi sasa St Marks Centre kwa makusudi tunashuhudia Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na fedha akikiuka taratibu za kifedha kwa kumlundikia majukumu yote ya kifedha kaimu mhasibu ambaye ajira yake ni change sana hapa chuoni.


Aidha nilitegemea sana angeweza kupata ushauri wneye manufaa zaidi ju uamuzi wake wake huo. Hii ni hatari sana kwa jinsi fedha za serikali/chuo zinavyoweza kusimamiwa. Nipende kuamini kuwa dhamana ya kutunza fedha inahitaji sana kupewa mtu ambae amefanyiwa uchunguzi wa kutosha na kujiridhisha na mwenendo halisi wa tabia hususani katika maswala ya fedha licha ya sifa za kielemu alizo nazo mtu.


Aidha nipende pia kujaribu kuungana na Wenzangu kuwa Mhasibu aliyeko anamahausiano ya kindugu na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na fedha na kama ndivyo hivyo basi ni imani yangu kuwa mpango huu umesukwa maalum kupeana nafasi zente mashiko ya kifedha. Pia inanifanya niamini kuwa ni mpango mahususi wa kucheza na fedha za chuo na kuwaondoa wale wafanyakazi waadifi katika idara hiyo ya fedha ili siri ziweze kuvujishwa kwa vyombo husika. Suala hili ushaidi upo.




Vice chancellor, katika kufuata sheria za utawala bora hapa nchini Tanzania kituo cha St Marks kiliweza kufungua tawi la chama cha wafanyakazi kulingana na sheria inaosimamia uanzishwaji wa vyama vya wafanyakazi ili kutumia chombo hiki kusikiliza hoja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hoja hizo zinasikilizwa nakupatiwa ufumbuzi kwa njia ya majadiliano ( COLLECTIVE BURGAINING) cha kushangaza ni kwamba Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na fedha ameamua kibabe kutotoa nafasi kwa Viongozi wa rawuu Tawi kuongea nae kuhusu masuala ya wafanyakazi ambao kero yao kubwa ni upendeleo wa ulipaji wa Mishahara.

Imeweza kubainika wazi kuwa wafanyakazi wa idara wa fedha hususani wale wapya wengine ambao walitanguliwa kuajiriwa. Huu ni ukiukajikwaji na ni uvunjaji wa sheria za kazi na siamini katu kama kuna mtu aliye juu ya sheria ambae anaeweza kujifanyia mambo anavyotaka yeye. Suala hili ushahidi upo.



Vice chancellor, wakati mwingine sisi wanadamu kwa kumwogopa Mungu tunapaswa sana kuwa na Huruma kwa watumishi ambao waliweza kutoa mchango wao wakati chuo hiki kikiendelea kukua na hatimaye kufikia hatua ya kumaliza muda wao wa utumishi hapa st Marks cha kushangaza ni kwamba wastafu wenzetu wameshindwa kabisa kuenziwa kwa kupewa nafasiya upendeleo wa kulipiwa malipo ya mifuko ya Pension.


Ki msingi halali a kifedha haikuwa nzuri kwa kipindi hicho cha utumishi wao hapa St Marks na ndio maana chuo kilishindwa kabisa kulipa michango kwa muda mrefu takirbani miezi mingi. Lakini kilichotokea ni kwamba kaimu Mkurugenzi wa fedha na Mipango ameamua kulipa malipo ya mifuko ya pension kwa kipindi ambacho hakiwajumuishi wastaadu hao.


Aidha kwa huruma tu ameshindwa kabisa kuwalipia wastafu hao fedha ambazo zingeingia katika mifuko ya pension ili nao waweze kulipwa ujira wao.


Naomba sana suala hili lipewe kipaumbele kwa vile kila mfanyakazi wakati wa kustaafu nap engine tusijione sisi ambao baada ya kustaafu huko tulikokuwa na kubahatika kupata ajira ikiwa nje ya muda wa kustaafu kuwa ni watu ambao hatuwezi kukutana na shida kama hii. Ushahidi wa suala jili upo.




Vice chancellor,baada ya kujaribu kukujulisha haya machache ningependa kutoa maoni yangu japo si lazima uyazingatie, Nashauri sana kwako kujaribu kuitazama safu ya uongozi hususani kayika centres ambazo ziko chini yako. Aidha ni imani yangu kuwa kwa muda uolikwisha kukaa katika nafasi Teule umeweza kujifunza mengi na pengine tayari ulishaanza kazi rasmi ila nishawishike kusema kuwa sisi wafanyakazi wa St Marks bado hujatuwekwa karibu nawe.


Yawezekana kabisa haya machache ambayo nimejaribu kuyaeleza yangeweza kuelezwa kwako mapema sana ili kutafuta njia ya kuyatatua kuliko hivi sasa hali ilivyo. Pengine yawezekana katika masula yahusio sifa za kielemu kwa nafasi za DEPUTY DIRECTORS, MASUALA YAHUSUYO TARATIBU ZA AJIRA, UPEANAJI WA VYEO VYENYE SURA ISIYEFUATA SHERIA ZA FEDHA HUSUSANI UHASIBU, UPENDELEO WA MISHAHARA na mengine mengi ambayo ninaamini kabisa wafanyakazi endapo utaamua kuonana nao watakujuza.Aidha, nishawishike pia kukujulisha kuna kila aina ya misuguano na pengine ungeweza kupata taarifa nyingi endapo ungeamua kufanya njia yoyote ambayp itakupatia taarifa nyeti zaidi kwa kuongea na watumishi mmoja mmoja au vinginevyo.


Mimi binafsi nimeamua kukupatia taarifa hizi huenda ikawa mara yako ya kwanza kuona mtumishi anaamua kujitolea kukupatia maswala ambao pengine kwa uwezo wako binafsi usingeweza kuyapata kamwe. Naamini kabisa kuwa uamuzi huu unaweza kabisa kuyagharimu MAISHA YANGU au HATA AJIRA YANGU.


Nipende kukumbusha kuwa sisi wakristo tulushuhudia Bwana Yesu AKISULUBIWA MSALABANI basi na mimi niko tayari kusulubiwa kwa kusema ukweli ili iwe chachu ua kuelekea huko kwenye uzima wa MILELE kwa huu ukweli ambao nimeamua kuuweka wazi kwenu ninyi Viongozi wa VIONGOZI WA ST JOHN'S UNIVERSITY OF TANZANIA HUSUSANI ST MARKS CENTRE NA KANISA ( MAASKOFU).



Kwa kumaliza napenda sana kuchukua nafasi hii kukujulisheni ninyi nyote MAASKOFU na VIONGOZI wote wa St john's university of Tanzania na St Marks centre kuwa nitakuwa tayari kutoa ushaidi wa maswala yote niliyoandika wakati wowote, mahali popote nchini, katika chombo chochote hata kama ni chombo cha DOLA endapo mtaona kuwa manufaa ya mimi kufanya hivyo. Aidha nina imani kubwa kuwa wafanyakazi nao wanaweza wakawa na kujifafanyia mambo ya UKENGEUKAJI WA MAADILI YA DINI HUKU TUKIWA KATIKA NYUMBA ZAKE.

Ni imani yangu kuwa kuongoza wafanyakazi hususani kwa karne hii ya utandawazi hakuna sababu yoyote ya kutumia mabavu yasiyo na tija vinginevyo kunaweza kusababisha machafuko ambayo yatakipelekea St Marks kufungwa aua kutopata wanafunzi kutokana na picha mbaya​
 
Back
Top Bottom