Ubungo Kibangu umeme unasumbua

Jan 23, 2020
13
6
Wadau! Walioko ubungo Riverside na kibangu yote (kwa mzee wa upako) hii sasa ni kero jamn kila wakati mgao sehemu hii tu hasa wakati wa usiku? Ama kuna siri gani nyuma ya pazia?

Sasa najiuliza hii ubungo ni kubwa sana lakin eneo moja tu kila wakati tena usiku? Nikero kwasababu kwa mazingira yalivyo hakuna mtu anaweza kulala ndani usiku pasi feni au A/C. Nimepita mtaani wakati narudi nyumbani muda sio mrefu nimekutana na situation ambayo imenifanya nikandika uzi huu, watu wameketi vibarazani na nje ya milango yao ilihali wanahitaji kupumzika keshowaweze kuendelea na miangaiko mingine!

Mwisho! Kweli kama kunawezekana kubadili hii ratiba ya kuukata umeme usiku tu jamni naomba upande wa ubungo Riverside na kibangu yote ipumzishwe kidogo.
 
Tanesco NI sikio la kufa, kama umepanga tafuuta pa kuhamia, na kama ndio kwako jipange na solar Tu, Tanesco walishashindwa kazi kitambo Tu.
 
Back
Top Bottom