Mgogoro wa Ardhi Ubungo, Wananchi waomba Waziri kuingilia kati. Wananchi 76 Wanalilia ardhi yao|Mkuu wa Wilaya Ahusishwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
835
1,000
Salaam Wakuu,

Wakazi Ubungo Walionyang'anywa ardhi yao, Wanaomba Serikali kuingilia kati ili Warudishiwe ardhi yao.

Pia wanaomba wawaondoe watu walio wekwa kwenye maeneo yao kwa nguvu na Mkuu wa Wilaya. Pili Viongozi wote walio shiriki hujuma dhidi yao kwa maslahi yao wawajibishwe.

Hapa chini ni Maelezo yao kuhusu Chimbuko la Mgogoro

=====

TAARIFA FUPI KUHUSU ARDHI YA TEGETA "A".

"Eneo hili lipo Zone C"mtaa wa Tegeta "A" kata ya Goba Manispaa ya Ubungo; Eneo lote kwa jumla lina ukubwa kati hekari 52 na 53 ambapo baadhi yalikuwa ni maeneo ya wazazi wetu na kujenga nyumba tulizoishi. Nusu ya eneo hili ilikuwa ni Pori lisilo endelezwa tangu miaka ya themanini, taratibu watu walianza kuingia kufyeka Pori kadiri miaka ilivyoenda.

Tarehe 26/1/2016 Polisi walikuja eneo hilo na kukamata watu 19 nikiwemo mimi nakutufungulia Kesi ya kuvamia ardhi ikidaiwa kwamba eneo hilo ni la BENJAMINI MUTAGWABA. Kesi ilianzia Mahakama ya Mwanzo Kimara na baadaye ikaombwa kuhamishwa ndipo ikafunguliwa upya Mahakama kuu kitengo cha ardhi kwa namba 188/2016 mbele ya Mh. Jaji Mgaya na ikatolewa amri ya zuwio tar.29/6/2016 kwa eneo hilo, amri ambayo ilitaka watu wazuiliwe kuingia kwa kuondolewa mpaka Mahakama itakapotoa uamuzi badala yake tar.20/10/2016 walikuja Yono action Mart kwa usimamizi wa polisi Wakabomoa nyumba zetu zote. Tulienda kwa Mkuu wa Wilaya Mh. PolePole naye atusikiliza na alitushauri pia.

Tulikubaliana kuchanga fedha za kumlipa wakili ambaye tulimpata kusimamia Kesi yetu ila Mkuu wa wilaya Mh. Kisare Matiko alituzuwia akasema ni kosa kuchangishana fedha bila kibali na kwamba tunawatakia watu akaagiza baadhi yetu tuwekwe Mahabusu, na tulilala Polisi siku nne tulivyo tolewa tukaendelea kuchanga ndipo tena akamwagiza OCD wa Mbezi anikamete na nikawekwa Polisi kwa siku tano.

Wakati misukosuko hiyo inatokea sisi tulitii amri ya Mahakama ya kutoendeleza eneo hilo, ndipo nyuma yetu wameletwa watu wengine kwa utambulisho wa mwenyekiti wa mtaa na kupewa Ushirikiano na mkuu wa Wilaya.

Wakaingiza greda kuchonga barabara, wakachimba kisima kirefu, wakaingiza umeme, na zaidi ya yote wameedelea na ujenzi bilà hofu yoyote katika eneo lenye zuwio. Mwishoni mwa mwaka Jana tulibaini kwamba wakati Kesi inaendelea walifanya upimaji wa eneo hilo wakati Kesi iko Mahakamani.

Mara kadhaa Tulilalamika kwa Mwenyekiti, na kwa Mtendaji wa Kata na tukienda Kwa mkuu wa Wilaya tunaitwa Matapeli tunaotaka kudhulumu wananchi wake hivyo yeye atatukomesha na hataki wananchi wake wabugudhiwe.

Tarehe 13/7/2020 Mahakama ilamua kwa kuyatupilia mbali madai ya Winner's Chaper kwa kushindwa kutimiza matakwa ya kisheri kuhusu Kesi hiyo ikiwemo suala la (Speed trac) hivyo kesi ikatupwa. Tulipoka Mahakamani tuliandika barua Polisi, Mtaa, na kata ili kukutana kwenye maeneo yetu, na kila tukifika kwenye eneo hilo Kuna watu wanatuambia, hatuna chetu hapo, maamuzi yote ni Mkuu wa Wilaya na yeye kawaambia wakae hapo.

Hivi karibuni tar 07/12/2020 nilipeleka pale tofali na Cement nikiwa na fundi wakatushambulia wakaita Polisi, Polisi wakaja na kuamuru niondoe vifaa hivyo vya ujenzi na wakirudi wasivikute hapo.

Tulienda kuriport shambulio Polisi Goba ili tukatibiwe ila Polisi walikataa kufungua Kesi wakasema mpaka mkuu wa kituo awepo, tulimsubiri kwa masaa manne tukampigia simu akasema tumpigie tena jioni saa 12 kama atakuwa karudi, ndipo tukapata msaada wa kiongozi mmoja wa Polisi aliyeko Dodoma akawasiliana na mkuu wa kituo ndipo tukapewa PF3 na kwenda hospitali. Siku Watuhumiwa walipokamatwa mkuu wa Wilaya alimwagiza mjumbe kwenda kuwatoa usiku huo huo.

Chakusikitisha ni kwamba kila tukijaribu kwenda kwenye eneo hilo tunafukuzwa na kutishiwa kufungwa jela, pia, inatajwa kwamba Mkuu wa Wilaya na baadhi ya wasaidizi wake Pamoja na OCD wametengewa maeneo ila wam

ewaweka watu wayashike badala yao. Maeneo hayo yanaendelezwa na kulindwa kwa nguvu kubwa ya Polisi na kwa kutumia kivuli Cha wananchi.

Nihitimishe kwamba Kuna Kesi mpya imefunguliwa tena dhidi yetu, safari hii wameongeza wadaiwa kutoka 76 hadi 138 na walioongezwa hata hawafahamiki tunadhani hii ni mbinu inayotumika ili waendelee ujenga lote maelezo mengine Pamoja na baahi ya nyaraka muhimu tukijaliwa kuonana nitakupatia.

Ahsante.

Ameandikwa na Mwenyekiti wa Wadai haki

Macarius Turuka

Na

Katibu Deodatus Buyokwe

1610346028282.png

1610346098928.png
 

baiser

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,147
2,000
Kiufupi inawezekana hilo eneo lilikuwa na mwenyew ,ninyi mkafikiri ni pori basii baada ya mwenyewe kuja ilibd muongee nae kiume awauzie sababu mlishajenga

Sasa ninyi mkaoana jamaaa ni hayawani ndo haya yaliyotokea

Hakuna eneo halina mmiliki bro
 

Nrangoo

JF-Expert Member
May 22, 2017
2,089
2,000
Kiufupi inawezekana hilo eneo lilikuwa na mwenyew ,ninyi mkafikiri ni pori basii baada ya mwenyewe kuja ilibd muongee nae kiume awauzie sababu mlishajenga

Sasa ninyi mkaoana jamaaa ni hayawani ndo haya yaliyotokea

Hakuna eneo halina mmiliki bro
tena ni juzijuzi tu hapo miaka ya 80 alafu eneo liwe pori kwamba halina mmiliki kweli, tena Ubungo??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom