John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 713
- 1,241
MOD: Nitaomba baada ya siku chache uinganishe hii na ile thread ya siku za nyuma kuhusu sakata la mgogoro wa Kibamba. katika jimbo la Ubungo
Sakata hili lilimfanya Magufuli akiwa Waziri wa Ardhi kwenda Kibamba na Wananchi wakampatia Orodha ya Mafisadi katika Sakata zima hili. Magufuli alikabidhi orodha hiyo kwa Polisi; Swali la Kujiuliza- Nini Kilifuatia?
NEW TWIST: Jumamosi tarehe 24 Mei, Shirika lisilo la Kiserikali la UDI liliandaa Semina ya Wananchi na kuwaeleza kuhusu Haki zao katika Muktadha wa sakata zima; ripoti ya Semina hiyo inapatikana hapa:http://ubungo.blogspot.com
Kufuatia semina hiyo, Jana Waziri Mpya wa Ardhi alikwenda Kibamba na Polisi; kwa ujumla baadhi ya polisi wameanza kupita kuwashikinikiza wananchi kusaini nyaraka. Lakini kubwa zaidi habari nilizozipata toka kikao kimoja cha ndani cha kiserikali ni kwamba wanatafuta namna ya kuwakamata waliowasilisha mada katika Mkutano huo na kuwabambikizia kesi ya uchochezi.
Mengi yataendelea kuibuka; lakini yote yanazunguka katika ufisadi katika matumizi ya bilioni kadhaa zilizotumika kuwalipa wananchi fidia kichele na pengine kwa kutumia nyaraka za kughushi.
Mjadala uendelee.
JJ