Mimi sioni kama Kuna Tatizo hapa, For safety reason hawatakiwi kufanya biashara katika eneo hilo wakati ujenzi unaendelea.
Ningeomba serikali kama kuna uwezekano iwatafutie sehemu mbadala wa kufanya biashara zao, Japo hili ni changamoto kwasababu wafanya biashara hao wanafanya biashara katika eneo hili kwasababu ya uwepo wa wingi wa watu.
Maendeleo yana gharama zake, kwa hili tuvumiliane
watanzania tufike mahali tuangalie mambo kwa macho matatu, binafsi naichukia sana ccm tena sana jwahiyo nimejikuta naichukia pamoja na serikali yake lakini kwa hii hatua ya kujenga fly overs napenda kuipongeza sana serikali yetu ni nchi chache sana ukanda huu wa Africa zimefikia hatua hii.
Asante sana wahusika ila muangalie kama kua uwezekano wa kuwasaidia hao mnaowaondoa kwenye maeneo hayo. yawezakuwa ndio njia pekee wanajipatia kipato.