UBUNGO, DAR: Machinga wapewa siku 3 waondoke

Tatizo ni kwanini serikali hahikutenga sehemu ya wamachinga.
Mradi wa flyover ndio unawakumbusha mwazo walifanya makosa
Ndugu yangu Galapagosi unategemea barabara itajengwa vipi bila wamachinga kuondoka eneo lile. Halafu pale ni barabarani unasema wapewe eneo rasmi la biashara kwani pale ni sehemu rasmi? Maendeleo yanakuja na matatizo ilo halikwepeki cha muhimu kama kuna stahiki za kulipa walipwe lakini kwa maono yangu eneo lile sio rasmi kufanya biashara. Au unataka tusijenge fly over kupunguza foleni ili watu wauze mitumba, mboga na toys maeneo yale? Jaribu kuwaza kwa kina
 
Yeah lazima waondoke na huo sio uonevu,

Lazima flyover zijengwe hayo ndo maendeleo,

Waende kule maeneo yaliko pangwa,
 
Ndugu yangu Galapagosi unategemea barabara itajengwa vipi bila wamachinga kuondoka eneo lile. Halafu pale ni barabarani unasema wapewe eneo rasmi la biashara kwani pale ni sehemu rasmi? Maendeleo yanakuja na matatizo ilo halikwepeki cha muhimu kama kuna stahiki za kulipa walipwe lakini kwa maono yangu eneo lile sio rasmi kufanya biashara. Au unataka tusijenge fly over kupunguza foleni ili watu wauze mitumba, mboga na toys maeneo yale? Jaribu kuwaza kwa kina
mkuu nipo upande wako kabisa sikuunga mkono toka mwanzo kabisa.
 
nilidhani unapinga. Kama unaunga mkono ule mradi pamoja sana pale foleni itakuwa historia na wakiweka nyingine pale magomeni na fire basi jiji litakuwa lishafunguka
 
Vijana nchi hii sijui wamekosea nini, wanachukuliwa kama MAJAMBAZI ?

- Waliosoma hawapewi ajira ?
- Wakiwa machinga wanafukuzwa kila leo na polisi ?
- Wakifanya biashara zao ziwe rasmi hawapewi TAX HOLIDAY wala GRACE PERIOD. Hata kabla ya faida wanakabwa na TRA, TFDA, NEMC, OSHA, FIRE, BRELA, COSOTA etc

- Hivi vijana wa nchi hii WAISHI Vipi ?
acha kulia njaa mjomba,jiajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mradi mzuri ila pia serikali iwasaidie hawa vijana wenzangu bila kuathiri shughuli zao

*Akifa shekhe kazi ya Mungu*
*Akifa mlevi sababu ya Pombe*
 
Mimi sioni kama Kuna Tatizo hapa, For safety reason hawatakiwi kufanya biashara katika eneo hilo wakati ujenzi unaendelea.

Ningeomba serikali kama kuna uwezekano iwatafutie sehemu mbadala wa kufanya biashara zao, Japo hili ni changamoto kwasababu wafanya biashara hao wanafanya biashara katika eneo hili kwasababu ya uwepo wa wingi wa watu.

Maendeleo yana gharama zake, kwa hili tuvumiliane

watanzania tufike mahali tuangalie mambo kwa macho matatu, binafsi naichukia sana ccm tena sana jwahiyo nimejikuta naichukia pamoja na serikali yake lakini kwa hii hatua ya kujenga fly overs napenda kuipongeza sana serikali yetu ni nchi chache sana ukanda huu wa Africa zimefikia hatua hii.

Asante sana wahusika ila muangalie kama kua uwezekano wa kuwasaidia hao mnaowaondoa kwenye maeneo hayo. yawezakuwa ndio njia pekee wanajipatia kipato.
 
Ndugu yangu Galapagosi unategemea barabara itajengwa vipi bila wamachinga kuondoka eneo lile. Halafu pale ni barabarani unasema wapewe eneo rasmi la biashara kwani pale ni sehemu rasmi? Maendeleo yanakuja na matatizo ilo halikwepeki cha muhimu kama kuna stahiki za kulipa walipwe lakini kwa maono yangu eneo lile sio rasmi kufanya biashara. Au unataka tusijenge fly over kupunguza foleni ili watu wauze mitumba, mboga na toys maeneo yale? Jaribu kuwaza kwa kina
Kuna watu wao wameumbwa kulalamika katika maisha yao yote wawapo duniani. Na hiyo ni kansa kwenye bongo zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hapo ndiyo uwe machinga wa ubungo halafu una mjengo wa urithi Kimara. Na siku anasema machinga wasibughudhiwe ukashangilia.

Kila mmoja wetu ataguswa, vijana tulipoguswa mlisema tumezoea kuishi kidot com.

Twende kazi.
 
IMG-20170830-WA0045.jpg
IMG-20170830-WA0047.jpg
IMG-20170830-WA0045.jpg
IMG-20170830-WA0047.jpg
IMG-20170830-WA0039.jpg
IMG-20170830-WA0044.jpg
IMG-20170830-WA0041.jpg
IMG-20170830-WA0041.jpg

Leo tarehe 30 August 2017, Mstahiki Meya wa Halmashauri Ya Manispaa Ya Ubungo,amefanya mkutano wa hadhara akihutubia wamachinga,katika makutano ya Ubungo Mataa.Akiambatana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bw.John Kayombo pamoja na Maofisa kutoka ofisi za TANROANDS,JESHI LA POLISI,WIZARA YA UJENZI, MKANDARASI WA FLYOVER UBUNGO- CCI-CCE,
Wenyeviti serikali za mitaa na watendaji wa kata za Makuburi,sinza na Ubungo.

Ikiwa dhamira yake ni Kuzuia Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwaondosha kwa Nguvu wa Machinga katika makutano ya Ubungo mataa,baada ya Kulalamikiwa na Mkandarasi wa FLYOVER UBUNGO,kuwa wamezagaa sana katika maeneo hayo kiasi cha kukwamisha Ujenzi wa Mradi ikiwemo kukosa eneo la kuweka vifaa vyao kama ,vifusi na Mitambo ya Ujenzi katika Eneo hilo.

Akiongea katika mkutano huo ,Mstahiki Meya amewaomba Wamachinga wapishe kwa Amani ishara kumuunga Mkono yeye (Meya) katika jitihada za Wamachinga kushughulikiwa kero zao bila ya Jeshi la Polisi kuwapiga Mabomu,

Aidha amewaruhusu wamachinga kwenda kupanga biashara zao popote pale barabarani nje ya eneo la Mradi, watakapo ona inafaa bila ya kubughuziwa na mtu yeyote,kufuatisha kauli ya Mheshimiwa Rais Kuwa Wamachinga wasisumbuliwe ,na Kwa Wale watakao taka kurejea kituo cha Mawasiliano,Manispaa ya Ubungo imeandaa utaratibu Mzuri wa Kuponi Maalumu kwa Wamachinga wa Ubungo.

MWISHO
Pamoja na kujadiliana changamoto mbalimbali na Wamachinga Viongozi wamekubali kuwaongezea siku tatu Mbele Wamachinga ilikujipanga namna ya kuondoka Eneo la Mradi,Na pia baadhi ya wamachinga wameomba kazi za vibarua katika Mradi kwa kipindi ujenzi utakapoendelea,huku Mama lishe wameruhusiwa kubaki kuwapikia Mafundi katika Mradi kwa utaribu Maalum kama Fursa ya Kipekee kwa kina mama hao.

Imetolewa Na
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO
 
Attachments

  • IMG-20170830-WA0048.jpg
    IMG-20170830-WA0048.jpg
    79.4 KB · Views: 53
View attachment 578461 View attachment 578462 View attachment 578461 View attachment 578462 View attachment 578467 View attachment 578471 View attachment 578468 View attachment 578468

Leo tarehe 30 August 2017, Mstahiki Meya wa Halmashauri Ya Manispaa Ya Ubungo,amefanya mkutano wa hadhara akihutubia wamachinga,katika makutano ya Ubungo Mataa.Akiambatana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bw.John Kayombo pamoja na Maofisa kutoka ofisi za TANROANDS,JESHI LA POLISI,WIZARA YA UJENZI, MKANDARASI WA FLYOVER UBUNGO- CCI-CCE,
Wenyeviti serikali za mitaa na watendaji wa kata za Makuburi,sinza na Ubungo.

Ikiwa dhamira yake ni Kuzuia Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwaondosha kwa Nguvu wa Machinga katika makutano ya Ubungo mataa,baada ya Kulalamikiwa na Mkandarasi wa FLYOVER UBUNGO,kuwa wamezagaa sana katika maeneo hayo kiasi cha kukwamisha Ujenzi wa Mradi ikiwemo kukosa eneo la kuweka vifaa vyao kama ,vifusi na Mitambo ya Ujenzi katika Eneo hilo.

Akiongea katika mkutano huo ,Mstahiki Meya amewaomba Wamachinga wapishe kwa Amani ishara kumuunga Mkono yeye (Meya) katika jitihada za Wamachinga kushughulikiwa kero zao bila ya Jeshi la Polisi kuwapiga Mabomu,

Aidha amewaruhusu wamachinga kwenda kupanga biashara zao popote pale barabarani nje ya eneo la Mradi, watakapo ona inafaa bila ya kubughuziwa na mtu yeyote,kufuatisha kauli ya Mheshimiwa Rais Kuwa Wamachinga wasisumbuliwe ,na Kwa Wale watakao taka kurejea kituo cha Mawasiliano,Manispaa ya Ubungo imeandaa utaratibu Mzuri wa Kuponi Maalumu kwa Wamachinga wa Ubungo.

MWISHO
Pamoja na kujadiliana changamoto mbalimbali na Wamachinga Viongozi wamekubali kuwaongezea siku tatu Mbele Wamachinga ilikujipanga namna ya kuondoka Eneo la Mradi,Na pia baadhi ya wamachinga wameomba kazi za vibarua katika Mradi kwa kipindi ujenzi utakapoendelea,huku Mama lishe wameruhusiwa kubaki kuwapikia Mafundi katika Mradi kwa utaribu Maalum kama Fursa ya Kipekee kwa kina mama hao.

Imetolewa Na
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO
Wakipatika viongozi kama hawa 20 tanzania itapiga hatu mbele kwa kasi sana. Saruti sana msitahiki meya BJ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waje kariakoo wachague barabara moja waipendayo wapange biashara mambo yaendelee coz nimepata kariakoo juzi duh ni shida nimkuta foleni ya miguu
 
Back
Top Bottom