Ubunge wa kubebwa ndiyo chanzo cha Spika Ndugai kuwaelekeza Wabunge?

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,038
1,154
Ukisikia Bunge halina mvuto ni Bunge hili lililosheni wabunge wengi wa CCM, wabunge wa upinzani kiduchu Sana, wabunge hewa kama wanavyojulikana covid-19.

Mvuto umekosekana hata kama Bunge ni live Wananchi hawafuatilii mijadala Bunge kama ilivyokuwa enzi Samwel Sitta au Anna Makinda.

Wabunge wengi hawajui kujenga hoja na kusimamia, wabunge wengi hawajui kuuliza maswali, hii inapelekea Spika wa Bunge kutoa maelezo kwa wabunge namna ya kujenga hoja, na namna ya Kujadili hata namna ya kuuliza maswali.

Inatokea siku ambayo Waziri mkuu huulizwa maswali hakuna hata swali anaulizwa.

Wabunge wa upinzani licha ya uchache wao, wamemezwa na CCM, hawajielewi kwa kujenga hoja na kuzisimamia, licha ya changamoto kibao taifa linakabiliwa.

Nakumbuka enzi za akina Masumbuko Lamwai, licha ya uchache wao, walisikika na Wananchi waliwafuatilia.

Wabunge hewa a. k. a Covid-19, wapo vizuri na wanajielewa, lakini kwa sababu ni hewa wanaogopa kuleta mijadala mizito, maana watapigwa vijembe kuwa ni wabunge wa Chama gani.

Uchaguzi wa 2020 umeleta dhahama kwenye taifa hili, si kwa wabunge tu hata mawazir hawajui kujibu maswali.

Mimi nashauri wabunge wanatakiwa kutafuta maarifa kwa kusoma sana na kufuatilia mambo mbalimbali na kuweka kumbukumbu Sawa, wasipende kusikiliza tu na kuchukua posho.

Nchi hii ina changamoto nyingi mno ambazo haziibuliwi na kuwasilishwa Serikalini.
 
Karibu wabunge wote wamesaidiwa, msaada wa kwanza ulikuwa kupenya kwenye Kura za maoni ndani ya CCM, na msaada wa pili ni kutangazwa na DED kuwa mshindi bila uhalisia wowote ule. Sasa Mbunge baada ya haya yote anapata wapi nguvu (guts) za kuisimanga serikali iliyomsaidia kufika hapo alipo.

Matokeo yake linabakia bunge la ..... "Mh. Waziri kama itakupendeza naomba..."
 
Wabunge wa CCM wanajadili nguvu za kiume na mijitu inashangilia na kukenua kenua tu, yaani Mbunge hajafikishwa kileleni na mchepuko wake anaifanya kuwa hoja ijadiliwe Bungeni, upuuzi mtupu.
 
Ndugai ana inferiority complex. Anajua hili bunge ndio limefitinika kuliko bunge lolote kuwahi kutokea. Ndio maana anatafuta attention kwenye kila fursa anayopata.

Hili bunge Watanzania wamelidharau, liko Live lakini hakuna anayejali, limekuwa kama kikao cha kahawa, ndio maana anatafuta kila namna ya kulifanya liwe relevant kwenye maisha ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom