Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
isaya mwita,

..Wassira alikuwa fisadi tangu Mwalimu akiwa madarakani. uliza vituko alivyofanya Mutex alipokuwa mkuu wa mkoa.

..kama kulikuwa na kitu kama laana ya Mwalimu basi ingempata Nyakyoma wa Gapex.

..madai ya wana Tarime ni ya msingi kabisa, lakini kama hata kabla ya kuwasilisha hoja tayari mnafikiria kufanya fujo["Tarime haitatawalika/haitakalika"] sidhani kama mtafika mbali.

..nadhani hao wenye mawazo ya maasi-maasi muwaogope kama UKOMA. badala yake mtafute watu wenye uwezo wa kujenga na kutetea hoja kwa kutumia taratibu za kisheria na kikatiba.
 
baadhi Ya Ramani Za Madini Tarime Nina Attach Hapa

Shy niliku-PM, ulipata msg yangu?

Anyway, umesema uta-attach hizo ramani za madini Tarime, mbona sijaziona mkuu?!

P.S. Weka maelezo/vielelezo chini ya hizo ramani kama utaweza (optional).
 
Gustaza Mimi Niko Njiani Kuja Tarime Kama Una Muda Na Uko Mara Tafadhali Tuonana Jumatano Asb Nitakuwa Tarime Usikose Nitakutumia Namba Yangu Ya Simu Au Naomba Kuwasiliana Na Hao Watu Wa Mtandao Wako Tubadilishane Nao Mawazo Nikiwa Huko Mara Tafadhali

Jioni Njema
 
Gustaza Mimi Niko Njiani Kuja Tarime Kama Una Muda Na Uko Mara Tafadhali Tuonana Jumatano Asb Nitakuwa Tarime Usikose Nitakutumia Namba Yangu Ya Simu Au Naomba Kuwasiliana Na Hao Watu Wa Mtandao Wako Tubadilishane Nao Mawazo Nikiwa Huko Mara Tafadhali

Jioni Njema

Shy kwasa niko nje ya nchi kwa shughuli za Kitaifa (sina uhakika nitarudi Tz lini...) Ila hao jama wa Tarime Citzens Action Group (TCAG), wengi wao ni wakazi wa Tarime wanaoishi ng'ambo. Nimebahatika kukutana nao nilipofika huku [undisclosed location/kwa protokali za ki-usalama]. Ila hao waungwana wana collaborate na locals wa huko Tarime (kwenye ground), maybe nitakupatia contacts zao few prominant locals wa Tarime (walio mstari wa mbele ktk suala hili) ili mubadilishane mawazo ukifika huko.
 
Isaymwita, kwani wewe naye ni Mtarime? Kama jibu ni ndiyo, kweli kazi mnayo! You know, hiyo cyanide inayoongelewa hapo is a very highly toxic chemical. Kuna documentary moja inaitwa "The New Gold Rush in the USA" ukipata chance itafute ndo utajua ubaya wa hiyo chemical.

In short, Toxicological studies (ATSDR, 1993) have indicated that hort-term exposure to high levels of cyanide can harm the nervous, respiratory and cardiovascular systems of animals/humans.

Plus huo mto Mara si unamwaga maji Ziwa Victoria? Hao Sato na sangara inabidi mu-waepuke kabisa!


Cyanide is a silent killer chemical! Sato na sangara zinalika kila sehemu ya tz. Watz twafaaaaaaaaaaa!!!!!
 
Gustaza Mimi Niko Njiani Kuja Tarime Kama Una Muda Na Uko Mara Tafadhali Tuonana Jumatano Asb Nitakuwa Tarime Usikose Nitakutumia Namba Yangu Ya Simu Au Naomba Kuwasiliana Na Hao Watu Wa Mtandao Wako Tubadilishane Nao Mawazo Nikiwa Huko Mara Tafadhali

Jioni Njema

Shy,

Heshima zako mkuu,

Hebu hapa tunafanyeje? maana hapa ni utata mtupu mkuu, tunajua umejaa ushauri Mkuu, kweli sijui kama itakuwaje, tunaendelea kujihoji na tena na tena, Shy tufanye nini?

Wewe wajua kwa sasa hatuna Mtetezi hapa pale mjengoni(bungeni) hakuna kinachoendelea, kiza kimetanda Mkuu,
sema neno mkuu,

Sijapata kuelewa tuanzaje hapa, tumegundua kupiga kura ni bure sijui tutanzaje hapa,
 
Cyanide is a silent killer chemical! Sato na sangara zinalika kila sehemu ya tz. Watz twafaaaaaaaaaaa!!!!!

Oh, mbona watanzania mlishakufa siku nyingi sana! In fact, Death certificates zenu zilisainiwa na government yenu wenyewe long time ago. Government inayoongozwa na dumb guys—who know so little [and probably nothing at all] on how to go about striking a balance between protecting its environment/its people & growing the economy. Cynide is a very deadly chemical huo ni ukweli usiopingika! Lakini nobody [serikalini] seems to care!

Below are some few quotes from Environmental Literacy Council zinazoelezea ubaya wa hiyo kitu inaitwa "Cyanide":

The use and disposal of cyanide solutions used to dissolve and extract gold is another environmental concern. Cyanide is a well known poison; hydrogen cyanide is acutely toxic to humans and, in its gaseous state, can be fatal at exposure levels of 100 to 300 parts per million (ppm). Cyanide is likewise harmful to wildlife such as mammals, birds, and fish which can have acute toxicity reactions to even low cyanide exposures.

The most significant risk from use of cyanide solutions in gold mining is possible leaching into soil and groundwater. There exists the potential for catastrophic cyanide spills that could inundate an ecosystem with toxic levels of cyanide. In 2000, heavy rain, ice, and snow caused a breach in a tailings dam (tailings are the cyanide-treated ore wastes, from which gold has been removed) at a gold mine in Baia Mare, Romania resulting in the release of 100,000 cubic meters of cyanide-rich waste into the surrounding watershed. Drinking water supplies were cut off for 2.5 million people and nearly all of the fish in the surrounding waters were killed.
 
Duh!
Lakini Wajomba zangu mbona madai mengi ya Tarime yanafanana sana na yale ya Zanzibar?... iweje muwe na haki ktk madai yenu lakini inapofika swala la Zanzibar nyie nyote mnakuwa upande wa serikali ya CCM.....
 
Duh!
Lakini Wajomba zangu mbona madai mengi ya Tarime yanafanana sana na yale ya Zanzibar?... iweje muwe na haki ktk madai yenu lakini inapofika swala la Zanzibar nyie nyote mnakuwa upande wa serikali ya CCM.....

Sidhani kama madai ya Tarime yanafanana sana na yale ya Zanzibar:

1.Tarime wanataka simple autonomy on just few selected things i.e. Elimu, public service, & umiliki wa maliasili wazilizobarikiwa (gold); while Zanzibar ni uroho tu wa madaraka ndo unaowasumbua. Yaani kwa maneno mengine, wanachopigania si kingene bali "secession" toka kwenye Muungano.

2.Tarime wanahoji uhalali wa maisha yao kutiwa hatarini kwa matumizi ya harmful chemicals kama cyanide na toxic nyingine zinazotokana na matuzimi ya heavy metals yingine zitumikazo ku-process/extract dhahabu; while Zanzibar wanachopigia kelele ni kama Zenji ni nchi au sio.

3. Madai ya watu wa Tarime kuhusu suala la kunyang'anywa mashamba yao bila kulipwa fidia yoyote (kuwapisha wazungu wachimbe dhababu) is indeed legitimate; while wazanzibari kudai kuwa bara inawanyonya ni nosesense maana landmass ya zenji ni sawa na mkoa wa Mara and its economy is almost equivalent na districts za bara kama vile Tarime ama Kishapu.

Have a nice day mkuu!
 
Gustanza_THE,

Mkuu ebu niwekee madai ya Zanzibar kama ulivyoorodhesha ya Tarime.. jaribu kutoandika Uroho wa madaraka kwa sabau hata mimi naweza kuona kinachogombewa Tarime ni uroho wa madaraka tu kwani hizo toxic mkilipwa fedha ndio kuna uhalali wa kuwepo hizo heavy metals au kinachotazamwa ni usalama wa wananchi wote waishio na wale wanaopita sehemu hizo?.

Lazima kutakuwa na mtu anayesukuma hoja hizi na yeye atakuwa na mamlaka makubwa na kile kinachopatikana kutokana na madini..
Nijuavyo mimi Ugonvi mkubwa wa bara na visiwani ni Ulaji na ndico nachokiona hapa. Binafsi siamini kabisa ktk ku singe out problems za sehemu moja kwa manufaa ya sehemu moja hali nchi nzima ina problem hiyo hiyo?..
Kwa nini Ujumbe wa muswada huu usiwe una cover Tanzania nzima ili ipitishwe sheria kwa ajili ya wananchi wote na sio Wa Tarime..Nionavyo mimi huu ni mwanzo wa kujigawa!
 
Gustanza_THE,
Mkuu ebu ipe madai ya Zanzibar kama ulivyoorodhesha ya Tarime.. jaribu kutoandika Uroho wa madaraka kwa sabau hata mimi naweza kuona kinachogombewa Tarime ni uroho wa madaraka. Lazima kutakuwa na mtu anayesukuma hoja hizi na yeye atakuwa na mamlaka makubwa na kile kinachopatikana kutokana na madini..
Nijuavyo mimi Ugonvi mkubwa wa bara na visiwani ni Ulaji na ndico nachokiona hapa. Binafsi siamini kabisa ktk ku singe out problems za sehemu moja kwa manufaa ya sehemu moja hali nchi nzima ina problem hiyo hiyo?..
Kwa nini Ujumbe wa muswada huu usiwe una cover Tanzania nzima ili ipitishwe sheria kwa ajili ya wananchi wote na sio Wa Tarime
..

Mkandara, the thing is, sehemu zingine za Tanzania hazi-face unyonyaji, uonevu ambao watu wa Tarime wana face, na pia haziko ktk risk ya kupatwa na kinachowasubiri watu wa Tarime mara tu hao wazungu watakapokuwa wamemaliza kukomba hizo gold zao na kuanza (matatizo ya kiafya yatakayoyokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendela huko Nyamongo,Tarime). Kwahiyo, sioni umuhimu wa kufanya issue ya Trime iwe applicable kwa watu wa chalinze, Mlandizi ama Kinyerezi.
 
Mkandara, the thing is, sehemu zingine za Tanzania hazi-face unyonywaji, uonevu, na pia haziko ktk risk ya kupatwa na kinachowasubiri watu wa Tarime mara tu hao wazungu watakapokuwa wamemaliza kukomba hizo gold zao na kuanza. Kwahiyo, sioni umuhimu wa kufanya issue ya Trime iwe applicable kwa watu wa chalinze, Mlandizi ama Kinyerezi.

What?.. mkuu hivi kweli unazungumza kwa uhakika ama unajaribu kutazama upande wako wa shilingi?..duh! umeniacha hoi..
Umesahau maswala ya Bulyanhuru, Songo, Mwadui, Ruvuma, Arusha kote kuna madini hivi sasa Morogoro yamepatikana mawe ya Rubis.. Misitu yetu inakatwa kila kona ya nchi, samaki ziwa Victoria hao sangara wanawanufaisha vipi wananchi?...
Wananchi wanahamishwa kila sehemu halafu wewe unasema Tarime?.. mbona haya yamewakuta majuzi tu mkuu yaani mkoa wa Marra ni nyumbani nilikokulia.
Kwa taarifa yako mkuu nilikuwepo huko mwaka jana na nina familia yangu hapo Musoma - The Kigera's na Kitundu..
 
What?.. mkuu hivi kweli unazungumza kwa uhakika ama unajaribu kutazama upande wako wa shilingi?..duh! umeniacha hoi..
Umesahau maswala ya Bulyanhuru, Songo, Mwadui, Ruvuma, Arusha kote kuna madini hivi sasa Morogoro yamepatikana mawe ya Rubis.. Misitu yetu inakatwa kila kona ya nchi, samaki ziwa Victoria hao sangara wanawanufaisha vipi wananchi?...
Wananchi wanahamishwa kila sehemu halafu wewe unasema Tarime?.. mbona haya yamewakuta majuzi tu mkuu yaani mkoa wa Marra ni nyumbani nilikokulia.
Kwa taarifa yako mkuu nilikuwepo huko mwaka jana na nina familia yangu hapo Musoma - The Kigera's na Kitundu..

Mkuu, soma tena [vizuri] reply yangu ya awali (hususani maneno niliyoyawekea 'bold':

Mkandara, the thing is, sehemu zingine za Tanzania hazi-face unyonyaji, uonevu ambao watu wa Tarime wana face, na pia haziko ktk risk ya kupatwa na kinachowasubiri watu wa Tarime mara tu hao wazungu watakapokuwa wamemaliza kukomba hizo gold zao na kuanza (matatizo ya kiafya yatakayoyokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendela huko Nyamongo,Tarime). Kwahiyo, sioni umuhimu wa kufanya issue ya Tarime iwe applicable kwa watu wa chalinze, Mlandizi ama Kinyerezi.

You know, there is an old African saying which say:“If you want to go fast, go alone. If you want to go far, go together.” Tarime inataka kwenda fast maana wanatambua kuwa they don't have another ten years kuwasubiri watanzania wengine wasio na uchungu na nchi yao wazidi kujikongoja. And I support them 100%.

Umesahau maswala ya Bulyanhuru, Songo, Mwadui, Ruvuma, Arusha kote kuna madini hivi sasa Morogoro yamepatikana mawe ya Rubis.. Misitu yetu inakatwa kila kona ya nchi, samaki ziwa Victoria hao sangara wanawanufaisha vipi wananchi?

Yes, nakubalina na wewe, ila hao wananchi wa hayo maeneo bado wamelala usingizi. It's hard to change their thinking overnite. Maybe Tarime ikifanikiwa, hao wengine wataiga, kisha nao waanze mapambano kujinusuru...
 
Gustanza_THE,
Basi mkuu kam kweli umeona wananchi wa sehemu nyingenezo wamelalaisipokuwa Wakurya, wakati wananchi wa sehemu hizo wamekufa kwa mamia wakililia haki hizo hizo unazozitaka then sioni sababu kabisa ya kulipeleka swala hili serikalini.
Hao wajumbe wa wilaya yenu wanaweza kabisa ku solve tatizo hili...Kwa sababu matatizo yenu hayawahusu watu wa Chalinze wala Msalala why bring to the table hali haiwahusu...Kama kweli hii ndio presentation yenyewe mkuu mtatoka watupu hakuna hekima hata kidogo..
Mnachokifanya nyie ni marudio ya sehemu nyingi sana na makosa makuybwa sana....Chukueni usia wangu.
 
Basi mkuu kam kweli umeona wananchi wa sehemu nyingenezo wamelala isipokuwa Wakurya, wakati wananchi wa sehemu hizo wamekufa kwa mamia wakililia haki hizo hizo unazozitaka then sioni sababu kabisa ya kulipeleka swala hili serikalini.

Mkuu, kukataa kuwa watu wa sehemu nyingine za TZ hawajalala usingizi ni kujaribu ku-deny the obvious.Kumbuka Lowassa alipojiuzuru kwa tuhuma za ufisadi, wananchi wake walimpokea kwa vifijo na nderemo. Same to Andrew Chenge. So kukataa kuwa wananchi wa sehemu zingine hawajalala usingizi, wakati miaka yote hiyo hawajawahi kuwapangua wabunge mafisadi toka kwa majimbo yao [wananchi waTarime wameisha prove tayari kuwa wako capable ku-punish wajingawajinga wa CCM ] inaonyesha kuwa hutaki kukubaliana na ukweli.

Hao wajumbe wa wilaya yenu wanaweza kabisa ku solve tatizo hili...Kwa sababu matatizo yenu hayawahusu watu wa Chalinze wala Msalala why bring to the table hali haiwahusu...

Kwa taarifa nilizozipata toka kwa baadhi ya wakazi wa kudumu wa Tarime, wajumbe wa wilaya ya Tarime wanajitahidi sana kutatua matatizo ya wananchi wao, ila wanapata kauzibe toka kwa mapandikizi toka serikali kuu (RC & DC) hence kurudisha nyuma jitihada zao. Ndio maana wamefikia conclusion kuwa maybe wakiwa na autonomy power ya kufanya decisison zao wenyewe bila interference toka serikali kuu, then jimbo lao litapiga hatua kubwa mbele.

Kama kweli hii ndio presentation yenyewe mkuu mtatoka watupu hakuna hekima hata kidogo. Mnachokifanya nyie ni marudio ya sehemu nyingi sana na makosa makuybwa sana.

Mkuu, I didn't expect such a response from someone like you! Usiseme kuwa hekima haipo, hekima ipo mkuu, ila tatizo ni wewe ambaye umevamia hii mada na pre-conceived notion kwamba matatizo ya ya Tanzania yatakuwa solved pale tu watanzania wote watakapoamua ku-join mikono [which is ok for people to have different point of view] hali ukisahau kuwa miaka nenda rudi hii approach ime-prove kuwa nothing but a greatest failure of epic proportinal [esp. kwa nchi za dunia ya tatu]. Nitarudia tena hii quote: "If you want to go fast, go alone. If you want to go far, go together." I think wewe unataka twende far as a nation, ila taifa kwa sasa haliko tayari, and Tarime nao hawana muda wa kusubiri.
 
Gustanza_The,
Mkuu hapa bado hujanipata hata kidogo..
Lowassa alipojiuzuru umesema wananchi wake walimpokea kwa shangwe sasa nambie kule kwao kuna madai gani yanayohusiana na rasilimali?..Issue hii hapa haihusiani na viongozi wachache Mafisadi ambao Tarime inataka kuwaondoa isipokuwa wananchi hawa kunufaika na rasilimali zao..
Kisha chukulia mawazo yangu kama ni usia mzuri na sio Upinzani kwa sababu swala hili linahitaji kuungwa mkono na wananchi Watanzania ili linapokwenda lipate kusikilizwa na pengine kupitishwa. Nacvhofanya ni kuwajengea hoja nyie ili ipate uzito na sio kukataa kile mnachojaribu kudai.
Ni Busara sana ku raise issue kwa kutumia maslahi ya Taifa yaani muswada mzima uhusu swala zima la mgawanyo wa pato la Taifa linalotokana na rasilimali zetu kisha, Hekima inaingia pale mtakapo tumia Tarime kama mfano na mwanzo wa harakati nzima za kuhakikisha kwamba wananchi wa Tarime watapata mnachokiomba. Sasa itakapo fika hawa wazungu kuingia hapo mtaweza kutumia hoja yenu kukataa uwekeshaji huo hadi solution imepatikana kuhusiana na mgao wa rasilimali zetu...
Hapo kila mbunge, kila mjumbe na wananchi kwa ujumla watakuwa nyuma yenu wakifahamu kufanikiwa kwa hoja nzima kutanufaisha wananchi wote. Lakini hadi sasa hivi madai yenu kila ninapoyasoma yamelenga kujitenga sawa sawa na Wazanzibar ambao wanaomba kitu ambacho hakiwezekani..
Kwa sababu Tanzania hakuna swala la Indigenous kiasi kwamba kamati nzima itayolitazama swala hili watakumbana na kutengwa kwa watu wenye asili fulani. Tarime imejaa watu wa makabila chungu nzima wengine wahamiaji na wengine wamenunua ardhi kwa hiyo huwezi kutoa sababu ya kimsingi kuonyesha tofauti ya wananchi wa Tarime na mikoa mingine. Sii ajabu Lowassa na Karamagi wamenunua ardhi huko hivyo utetezi wako hauzingatii upana wa hoja nzima.
Nakuombeni rudini mezani opangeni upya madai yenu yaweke ktk hali ambayo hayta mimi hapa naesoma naweza kuona mantiki ktk madai haya nje ya kutafuta kujitenga tena kwa kuonyesha kuwa nyie ati ni wabora zaidi kuliko Watanzania wengine.. Ni madai yasiyokuwa na msingi sawa kabisa na Wazanzibar!..
Have a good day mkuu!
 
Kwakweli issue ya Tarime ni ya ajabu. Naona wanataka kutekeleza sera za CHADEMA wakati CCM ndo ipo madarakani.

Hii haiwezekani, ni sawa na CCM (baadhi) zenji wanavyotaka kutekeleza sera za CUF huko Zanzibar!
 
FairPlayer,Mkandara,Gustanza_The,Isaya-Mwita,

..madai kama ya wana-Tarime yangetolewa na wachaga basi "pasingetawalika" hapa Jamii Forums. wangeitwa majina ya kila aina, na pengine kutukanwa matusi makubwa-makubwa.

..katika Tanzania ardhi ni mali ya umma. sheria ya ardhi na rasilimali zake kuwa mali ya umma aliiteta Baba wa Taifa, na unaweza kutafuta hotuba zake kuona hoja aliyojenga.

..walioathirika na sheria hiyo Tanzania siyo wana Tarime peke yao, wako wananchi wa maeneo mengi tu walioathirika.

..nasubiri kwa hamu kusikia hoja nzima itakapokamilika na kuwasilishwa. inaweza kupanda mbegu nzuri ama mbaya kwa taifa letu.

NB:

..hivi mgunduzi wa Tanzanite alipewa nini na serikali yetu zaidi ya cheti/karatasi??
 
"Divide and Rule" Hiyo ni statement ya wananchi wa Tarime au wachache waliopewa ahadi? Tanzania wapi tunaelekea?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom