Ubunge sio the Comedy; Kwako Steve Nyerere

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
UBUNGE SIO THE COMEDY

Na, Robert Heriel

Ujumbe huu ni mchungu lakini naomba ufike kama nilivyokusudia, pengine maneno yake yakawa makali. Hivyo natoa angalizo; Kama unaroho nyepesi na mihemuko ya karibu tafadhali usisome.

Kuna kitabia cha kipuuzi Baadhi ya wasanii wanacho, yaani mtu akishahisi amekuwa maarufu anaona tayari ameshafuzu kupewa ubunge. Jambo ambalo sio sahihi.

Ubunge sio the Comedy, ubunge sio bongo movi sijui bongo fleva, Ubunge sio kukata mauno na kuimba imba matusi. Tunajua mambo hayo yamewasaidia kuwapa umaarufu, tunafahamu mambo hayo ndio yanaendesha maisha yenu na familia zenu. Lakini Watanzania hatutakubali usanii wenu ndio iwe ticketi ya kutuongoza sisi Watanzania kwa nafasi ya Ubunge.

Hatutaki bunge la vichekesho, bunge la vikatuni, bunge la watu wanaopenda kiki. Bunge hilo hatulitaki.
Mifano tunayo ya wabunge ambao ni vikatuni, yaani mbunge akichangia hoja anaongea vioja na vituko akitafuta umaarufu wa kipuuzi. Tena wabunge wengine ni watu wazima kabisa lakini ni vikatuni.

Hatutaki waheshimiwa Vikatuni, yaani ukiangalia bunge utadhani unatazama Tommy na Jerry hiyo hatutakubali.

Tupo Karne ya 21 hatutatumia kigezo cha kujua kusoma na kuandika katika kuchagua viongozi. Vigezo vifuatavyo tutazingatia:
1. Maadili na Uzalendo
2. Uchapakazi
3. Elimu kuanzia kidato cha sita kuendelea.
Wewe kama huna vigezo tajwa hapo mwaka huu utausikia kwenye bomba. Jamii makini haiwezi ongozwa na jitu ambalo halina maadili na uzalendo, jitu ambalo halijaenda shule, jitu sio lichapakazi.

Watanzania sasa wameamua kuleta mabadiliko, na mabadiliko hayaletwi na Vikatuni, the comedy, sijui waigizaji gani huko. Angalau kikatuni kiwe kimeenda shule, au comedian aliyeenda shule, au hata Mwanamuziki aliyeenda shule. Lakini kama shule hakuna huna nafasi katika bunge mwaka huu.

Jamii jinga ndio itachagua vikatuni, itaongozwa na watu wasioenda shule, wapiga domo tuu. Hivi mtu ambaye hajaenda shule atashauri nini kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia, hatuwezi kurudishwa enzi za zama za mawe.
Steve, Shilole, harmonizer, na wengineo ambao shule ni ndogo muache kutuletea ukatuni.

Nitashangaa majimbo husika ikiwa yatakubali kuongozwa na watu wasio na elimu. Nitashangaa chama kitakachowapitisha watu wasio na elimu awamu hii.

Hatutaki wagonga meza bungeni, hatutaki waongea utumbo bungeni, hatuna muda wa kuwachagua.

Nafurahia majimbo yanayojielewa, majimbo yanayotaka mabadiliko chanya, ndio maana wanachagua watu wenye elimu ili kuhamasisha watoto waendelee kusoma. Na ndio maana kuna utofauti wa maendeleo baina ya jimbo na jimbo.
Huwezi ongozwa na Mtu asiye na elimu akaleta mabadiliko chanya ndani ya jamii. Ni upuuzi mtupu.

Wasanii wote wasiosoma piga chini.
Sijui Steve Nyerere Piga chini
Sijui Shilole Piga chini
Sijui Harmonizer garagaza chini
Wote wa Darasa la saba B piga chini.
Sijui Msukuma piga chini.
Na wote wa namna hiyo piga chini.

Tanzania ya viwanda haitaletwa na wabunge ambao hawajaenda shule. Ni uongo wa mchana.

Hata kama Katiba inasema kila mtu anayohaki ya kugombea uongozi ilimradi ajue kusoma na kuandika lakini tuangalie ilisema lini na sasa hivi tupo wapi.

Hatutaki kuongozwa na wajinga sisi.

Nimemaliza.

Taikon wa Fasihi, niko njiani kuelekea Same kuchukua fomu ya ubunge.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Steve kwani hata hiyo comedy anaweza? He can't lead himself, alafu atafute ubunge amuongoze nani? Elimu ni key katika uongozi, hata ukiwa mwalimu wa sekondari kwenda juu or Bachelor inakupa uelewa kuongoza vema, nitashangaa sana mtu ambaye hata mwenyewe hajielewi alafu atake ubunge, that is a total joke.
 
Mwaka 2015 Kingwendu nae aligombea ubunge Kisarawe.

Tanzania watu wana masihara sana. Au sijui ni bunge wanalidharau ndio maana wanapata guts za kugombea ubunge? Nadahani Bunge lingekuwa imara, kali, serious na la kiweledi watu wangejipima kabla ya kugombea.
 
Tena alishinda akauza jimbo
 
Nitawashangaa ndugu zangu wa Iringa kwa kweli
 
Mwaka 2015 Kingwendu nae aligombea ubunge Kisarawe.

Tanzania watu wana masihara sana. Au sijui ni bunge wanalidharau ndio maana wanapata guts za kugombea ubunge? Nadahani Bunge lingekuwa imara, kali, serious na la kiweledi watu wangejipima kabla ya kugombea.

Ni jamii jinga ndio itaongozwa na wasioenda shule
 
Huyo Steve hata akili ya kawaida ya kuzungumza hana ni mropokaji kwanza nashangaa e fm wamempa asome magazeti, yaani unakutaka kunataarifa anasoma ambayo inataka kuchangia hoja hawezi he no nothing kwakwel ni ujinga mtupu kabisa.
 
huyo steve hta akili ya kawaida ya kuzungumza hana ni mropokaji kwanza nashangaa e fm wamempa asome magazeti .yan unakutaka kunataarifa anasoma ambayo inataka kuchangia hoja hawezi he no nothing kwakwel ni ujinga mtupu kabisa.

Akili yake imemdanganya kuwa anaweza danganya wananchi Wakampa kura
 
Anaweza akawa ajaenda shule lakini akawa na tija.Kutokwenda shule pana fact nyingi tusiwalaumu yawezakuwa wazazi hawana uwezo, changamoto za mazingira,nk.ishu ni reasoning na tija.

Wapo wenye PhD wengi tumeona vituko vyao, badala ya kuitumikia Jamii wanamuabudu mtu kisa tumbo.
 
Ubunge sio the Comedy, ubunge sio bongo movi sijui bongo fleva, Ubunge sio kukata mauno na kuimba imba matusi. Tunajua mambo hayo yamewasaidia kuwapa umaarufu, tunafahamu mambo hayo ndio yanaendesha maisha yenu na familia zenu. Lakini Watanzania hatutakubali usanii wenu ndio iwe ticketi ya kutuongoza sisi Watanzania kwa nafasi ya Ubunge.
Such a nice and strong message to the audience. Nimeipenda sana hii
 
huyo steve hta akili ya kawaida ya kuzungumza hana ni mropokaji kwanza nashangaa e fm wamempa asome magazeti .yan unakutaka kunataarifa anasoma ambayo inataka kuchangia hoja hawezi he no nothing kwakwel ni ujinga mtupu kabisa.
Hivi ni kijana au mzee?
 
Na kile kisura chake kama nyani, hata simjadili.

Anajua yupo kwenye chama cha kubebwa na tume ndio maana.
 
Hatutaki bunge la vichekesho, bunge la vikatuni, bunge la watu wanaopenda kiki. Bunge hilo hatulitaki.

Mifano tunayo ya wabunge ambao ni vikatuni, yaani mbunge akichangia hoja anaongea vioja na vituko akitafuta umaarufu wa kipuuzi. Tena wabunge wengine ni watu wazima kabisa lakini ni vikatuni.
Ukitaka kuoina seriousness ya nchi yoyote ni kwenye mambo kama haya. Wakati jirani zetu Kenya wakitaka mbunge au seneta awe na digrii ya kwanza na kuendelea sisi huku tuko busy kushikilia kigezo cha darasa la saba what a fuckin mistake.

Na ndio maana hata kimaendeleo wametupiga bao sana kwa sababu bunge lao na senate yao imejaa vichwa vinavyofikiri na sio wagonga meza kama sisi tulionao huku. Naiunga mkono hoja yako kupinga bunge la vikatuni
 
Back
Top Bottom