Ubovu wa BoT kiutendaji

Peasant educator

JF-Expert Member
Mar 13, 2020
209
187
Habari wadau.

Nina malalamiko juu ya utendaji wa BOT. Nimeshuhudia utendaji wao first hand nilipofikisha malalamiko yangu ofisini kwao na niliojionea ni vituko tu kwa ofisi hiyo kubwa na yenye reputation kubwa.

Moja: Ukifika utapishana na vikabu vilivyopambwa vizuri ambavyo vinaenda kama zawadi kutoka mabenk kwenda kwa watumishi wa BOT zikiwemo na bahasha za fedha na card sijui humo ndani.

Pili: Faili zangu nilikuwa hazionekani, yani zilipotea kwa mda wa miezi 3 kwenye mazingira ya kutatanisha. Ukiuliza unazungushwa mpaka ukate tamaa.

Tatu: Kwa uelewa wangu mdogo BOT ni kama TCRA kwa upande wa mabenki. Yani inakazi ya regulate financial institutions zote nchini ikiwemo banks na pia kulinda haki za mteja na bank. Yani pale kuna tatizo bank kwa upande wa mteja, iwe uonevu wizi na kadhalika unafika BOT kwanza ili wasuluhishe. Ila vile vikapu na bakhshishi niliongelea hapo juu ndo vinafanya kazi. Hapo ndo failizi zinapotea na ushikinoa hupewi. Utaenda miezi nenda miezi rudi unaishia ofisi moja tu ukienda kuonana na mkuu ndo kasheshe sasa. Kila siku vikao na kusema wako under capacity na file ni nyingi.

Nne: Ukijibiwa baada ya miaka kadhaa, wanapendelea bank (vikapu na bakhshishi). Hakuna uwazi hata kidogo na wanatoa hukumu wanavotaka wao bila ata copy ya ushahidi. Inshort mlalamikaji huwezi pata msaada. Unaenda kulalamika umefutwa au umetolewa kwenye account ya kampuni bila utaratibu kufatwa na bank unaiandikia official letter wajibu hawajibu na ukisema naenda BOT wanakwambia off you go. Kule nako unalalamika wanaongea juu kwajuu kuwa wamepokea vieleelzo ikiwemo resolution, barua ya kukutaarifu wewe muhusika nk. Ukiomba uineshwe wanasema INFORMATION FROM THE BANKS ARE CONFIDENTIAL . HIVI TUTAFIKA KWELI!!!!

Tano: Rushwa imetamalaki. Yani bank zinahonga na kutoa rushwa BOT kama wahandisi wanavohonga TANROADS kupata tenda. Ila bank zinahonga kupita kiasi ili maslahi yao yalindwe.

Sita: Wao kila siku wanapitisha regulation mpya ila hazifanyi kazi mpaka wakiamua na inakuaje wako undercapacity. Kwanini ofisi haina wafanyakazi? Mm sitaki kuamini kuwa BOT hamna wafanyakazi kama sio uongo ni nini? Hii ndo taasisi kubwa Tanzania ina mashaka kiasi hiki!?

Wizara ya fedha mpaka leo kelele tu hamna cha mana mnafanya na watumishi wenuwanazingua. Mnashindwa ata kusimamia miongozo yenu kwa mabenk na BOT. Nakumbuka mwaka jana mlitoa matamko sijui mara ngapi bank zipunguze riba ili mikopo iwe nafuu kwa wananchi. Sababu wizara imepunguzia mabenki riba kupitia BOT ila bank hazijafanya hivo hadi leo. Shida nini?

Kama kikwazo kikubwa ni BOT na watumishi wake basi wanakula rushwa na wana maslahi binafsi katika bank hizo ndo mana mpaka leo zoezi linashindikana!!! Lakini na wizara mnachangia!!!!

=====

Updates kutoka BoT

======

Ndugu,

Tunakiri kupokea malalamiko yako kupitia mitandao ya kijamii. Pole kwa usumbufu wowote ulioupata. Benki Kuu ya Tanzania inathamini sana wateja wake wote na si matakwa wala matarajio ya Benki Kuu kutoa huduma zilizo chini ya kiwango kwa wateja wake. Tunakuomba uwasiliane nasi, tukusikilize ili tuweze kuchukua hatua stahiki. Tafadhali tutafute kwa 0767223602.
 
Back
Top Bottom