SoC02 Uboreshaji wa Elimu nchini Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Saleh Mmambiia

New Member
Aug 15, 2022
2
0
UBORESHAJI WA ELIMU TANZANIA

Kwa miaka ya hivi karibuni utolewaji wa elimu nchini ya Tanzania umeimarika sana ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo serikali na taasisi binafsi zinapigania vyema katika namna ya kuboresha miundombinu ya kielimu ili kutoa elimu bora ambayo inaenda sambamba na na ulimwengu wa sasa wa sanaynsi na teknojia, mashirika binafsi yamekuwa na kipaumbele katika kuisaidia serikali kwa kutoa huduma za kielimu mijini na vijijini ili kuhakikisha ufaulu unaongezeka kwa kupata wataalamu bora nchini, hata hiyvo kumekuwa na changamoto nyingi ambazo kwa upande mwengine zinarudisha nyuma na kuzorotesha jitohada za utoaji elimu kupelekea changamoto hizo kuwa sugu na huchangia hata katika kushuka kwa ufaulu kwa baadhi ya mashule kwa maeneno mbalimbali ya mijini na vijijini.

Changamoto za kielimu na maboresho yake

1. Ili elimu iweze kuimarika lazima kuwe na mfumo wa kufuatilia na kutatua changamoto za kielimu zinazowakumba wanfunzi , walimu na wazee na miongoni mwa changamoto hizo ni

Mazingira ya shule na miundombinu ya kufundisha: Kwa shule nyingi zilizopo maeneo ya vijijini zinakosa mazingira rafiki kwa utoaji wa elimu kwa wanafunzi na kupungunguza hamasa ya kujifuna na kufundisha kwa vile shule inakosa miundombinu ya kisasa kama maabara za masomo ya sayansi na maabara za kumpyuta na baadhi ya shule kukosa uzio hivyo kuhatarisha usalama wa eneo la shule kwa vile wanayama wakali kufika karibu na maeneo ya shule.​
Usafiri: Mbali na serikali kuweka mikakati na sheria madhubuti kwa madereva na makonda kuhusu wanafunzi wapandao magari ya umma kwenda na kurudi shuleni, bado kumekuwa na kero kwa baadhi ya madereva na makonda kuwakataa wanafunzi kwa kile kutokukidhi kwa faida indapo atawapakia wanafunzi, hata wakipanda kumekuwa na maneno ambayo si ya kiungwana kwa baadhi ya madereva na makonda kwa wanafunzi hivyo kupelekea unyonge na kujihisi si sehemu ya jamii, kupelekea kuchelewa mashuleni, na inamlazimu mwanafunzi kuamka mapema zaidi tofauti na muda wa kawaida ili kuwahi gari na kuwahi kufika shuleni.​
Unyanyasaji kijinsia: Kumekuwa na kero kubwa ya unynyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi toka kwa baadhi ya walimu wao wanaokiuka maadili mbali na sheria kali zilizowekwa na serikali, baadhi ya walimu wamekuwa ndio chanzo cha matatizo ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi kama walimu kuhusika katika kuwapa ujauzito wanafunzi na kutoka nao kimapenzi kinyume na sheria.​


2. Serikali iweke viwango vya walimu wa masomo.

i. Walimu waweze kutambua uwezo tofauti wa kujifunza kwa wanafunzi.
ii. Kutambua utofauti wa kila mwanafunzi katika mila, desturi, siasa na utamaduni.
iii. Kutambua mazingira ya kujifunzia (kubadilisha nadharia kuwa katika vitendo yenye kuakisi maisha ya kila siku).
iv. Kumudu somo husika.
v. Kuweza kutumia somo katika maisha ya kila siku.
vi. Kufanya tathimini ya somo wakati wa kufundisha, baada ya kufundisha na kwa wanafunzi.
vii. Kutumia mbinu za ufundishaji mfano kama bingua bongo, jadili na elezea.
viii. Kushirikisha wazee wa wanafunzi.
ix. Kuleta mrejesho wa mitihani.
x. Kuweza kuandaa andalio la somo na azimio la somo.


3. Serikali iweke viashiria vya uongozi na utawala.

i. Mahudhurio ya wanafunzi.
ii. Kufika kwa wakati katika shule kwa walimu na wanafunzi.
iii. Ushiriki wa wanafunzi katika kujifunza.
iv. Kuhimiza wanafunzi kudurusu.
v. Kufanya mitihani na kupata tathmini.


4. Viashiria vya walimu katika ufundishaji.

i. Mwanafunzi kulifahamu somo na kuweza kuuliza maswali na kuakisi katika maisha ya kila siku.
ii. Somo kutaarishwa na kufundisha vizuri.
iii. Mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi.
iv. Tathimini na mrejesho wakati wa kufundisha, baada ya kufundisha na kwa mwanafunzi.
v. Maendeleo mazuri ya kufundisha (tathimini ya mwalimu).
vi. Matumizi mazuri ya njia za kufundishia na vifaa vya kufundishia.
vii. Mwalimu aweze kuuliza maswali yenye sifa na yanayoakisi uhalisia.
viii. Kuwe n a mazingira ya ziada ya kufundisha katika maeneo ya kufundisha kama mabango na michoro ya ukutani.


5. Kuboresha sera ya elimu, andalio la somo na azimo la somo

Serikali iweeke maboresho katika sera ya elimu ili kwenda sawa na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi na sayansi na teknolojia ya dunia kwa kujenga uwezo uwezo wa kufanya na sio kukariri ili kupata watendaji kazi katika taasisi mbalimbali.

Katika andalio la somo na azimio la somo kama ilivyowekwa kwa uwezo mkuu basi pia uwekwe uwezo maalum ambao utakizi mahitaji ya mwanafunzi mmoja mmoja na pia katika mrejesho mwalimu aweze kuhusisha somo na maisha ya kila siku.


6. Kuimarisha ukaguzi wa ndani na nje ya shule.

Kuwe na ukaguzi wa ndani ambapo mwalimu mkuu afanye ukaguzi wa ndani wa walimu wa masomo na wanafanyakaiz wengine pamoja na wanafunzi, pia idara ya taaluma za ukaguzi kukagua walimu kwa wakati husika na kwa idadi sawa na kwa walimu wote na kutoa mrejesho kwa walimu husika baada ya ukaguzi.


7. Walimu wakuu kufuata ngazi za uongozi.

i. Cheo kifuatane na miongozo ya kanuni ya kazi.
ii. Kutoa ushirikiano kwa walimu na wafanya kazi.
iii. Kuweza kutoa matokeo mazuri ya mitihani.
iv. Kufanya mafunzo ya ndani ya kuimarisha uwezo wa walimu na wafanyakakazi.
v. Walimu kuwa kigezo kizuri kwa wanafunzi( walimu kufuata maadili ya kazi na miongozo ya kijamii).


8. Kutambua kazi za mitihani ya majaribio.

i. Kumfanya mwanafunzi aweze kudurusu .
ii. Tathmini kwa wanafunzi.
iii. Kutizama maswali yaliyofanywa vizuri, yaliyofanywa vibaya, na yaliyoachwa.
iv. Kutizama matokeo yajayo( utabiri wa matokeo yajayo)
v. Mlinganisho kati ya waanfunzi.
vi. Kutengeneza ushindani.


9. Kuandaa dira, mikakati mpango kazi na mpango wa maendeleo.

Ni muhimu kwa kila shule kuandaa dira itakayoongoza ufanyaji kazi wa walimu, kuandaa mikakati ya ufaulu na kupunguza utoro mashuleni, kuandaa mpango kazi na kuandaa mpango wa maendeleo.


CHANZO
Haynes, A. (2010). The Complete Guide to Lesson Planning and Preparation, New York: Continum International Publishing Group.


Saleh Hashim Mmambiia
0774071945 / 0686686607
senatormmambiaa@gmail.com
 
Back
Top Bottom