Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utaendelea katika Mkoa wa Dar es Salaam, kuanzia Machi 17, 2025 hadi Machi 23, 2025.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri leo tarehe 17 Machi, 2025 ametembela vituo mbalimbali vya kuandikisha Wapiga kura vya Jimbo la Kibamba Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam kuona zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyoendelea.
Uboreshaji wa Daftari mkoani Dar es Salaam unafanyika kwa siku saba hadi tarehe 23 Machi, 2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele ametembelea vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mkoani Dar es Salaam, leo Machi 17,2025 katika siku ya kwanza ya zoezi hilo mkoani Dar es salaam.
Uboreshaji wa Daftari mkoani Dar es Salaam umeanza leo na utadumu kwa siku saba hadi Machi 23,2025.