Pre GE2025 DSM Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Dar es Salaam Kufanyika Machi 17-23, 2025. Wapiga Kura wapya 643,420 kuandishwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Sep 4, 2024
172
192
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Dar es Salaam utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 17 hadi 23 Machi, 2025 ambapo wapiga kura wapya 643,420 wanatarajiwa kuandikishwa.

1741170398698.png
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndugu. Kailima, R. K kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Machi, 2025.

"Leo tupo hapa Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa huu, ambapo zoezi litafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 17 Machi, 2025 na kukamilika tarehe 23 Machi, 2025 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni," amesema Jaji Mwambegele.

Amesema mkoa wa Dar es Salaam ndio wa mwisho kwenye awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Dafatri ambayo ilizinduliwa mwezi Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika kwenye mikoa 28 na kwamba mikoa ya Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga inatarajiwa kukamilisha zoezi hilo tarehe 07 Machi, 2025.

"Hadi leo tarehe 05 Machi, 2025 Tume imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari katika Mikoa 28. Kwa mujibu wa ratiba, kwa sasa Tume imeanza maandalizi ya mzunguko wa 13 ambao ni mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu unahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Aidha, zoezi la uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa wa Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga unaendelea tangu tarehe 01 Machi, 2025 na utakamilika tarehe 07 Machi, 2025," amesema Jaji Mwambegele.

Akiwasilisha mada kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndugu. Kailima, R. K amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

"Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na wapiga kura 4,071,337," amesema.
 
Tume iongeze muda wa uandikishaji kutoka siku 7 hadi 14. Hapa Morogoro zoezi linasuasua sana kutoka na vifaa kushindwa kufanya kazi. Kwa siku wanaandikishwa watu wasiozidi 50 huku wengne zaidi ya watu mia wakirudishwa kutokana na giza na machine kushindwa kutoa picha zenye ubora. Lakini pia mashine ipo moja ya kuhudumia huku baadhi ya vituo kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura. Pia kushindwa kuweka kituo kwenye shule za sekondary kumesababisha kuongeza foleni kwenye vituo vya kiraia kwa kuletewa wanafunzi zaid ya 400. Mpaka sasa upo uwezekano mkubwa kwa wananchi kutopata vitambulisho vya kupigia kura kutokana na muda mdogo uliowekwa
 
📢 VIJANA WA DAR ES SALAAM – NI WAKATI WETU! TOKA, NITOKE - TWENDE TUKAJIANDIKISHE

🔥 MIAKA 18+...!! TOKA, NITOKE – TWENDE TUKAJIANDIKISHE! 🔥

🗓 TAREHE: 17 - 23 Machi 2025
📍 ENEO: Mkoa wa Dar es Salaam

Twende tukajiandikishe, maana maendeleo hayaji yenyewe – tunayachagua sisi..!!

#KaziNaUtuTunaSongaMbele
#KijanaNaKijani
#TunazimaZoteTunawashaKijani
#TokaNitokeTwendeTukajiandikishe
 
Attachments

  • IMG-20250310-WA0590(1).jpg
    IMG-20250310-WA0590(1).jpg
    69.4 KB · Views: 2
Ujinga huu hicho kitambulisho ni kwa ajili ya nini

Kusumbua watu
Kupotezea watu muda
Be smart
 
📢 VIJANA WA DAR ES SALAAM – NI WAKATI WETU! TOKA, NITOKE - TWENDE TUKAJIANDIKISHE

🔥 MIAKA 18+...!! TOKA, NITOKE – TWENDE TUKAJIANDIKISHE! 🔥

🗓 TAREHE: 17 - 23 Machi 2025
📍 ENEO: Mkoa wa Dar es Salaam

Twende tukajiandikishe, maana maendeleo hayaji yenyewe – tunayachagua sisi..!!

#KaziNaUtuTunaSongaMbele
#KijanaNaKijani
#TunazimaZoteTunawashaKijani
#TokaNitokeTwendeTukajiandikishe
mawaidha mujarabu kabisa kwa wakati muafaka na kwa mustakabali wa taifa na maendeleo yetu na taifa letu,

well done gentleman 💪👊
 
Ujinga huu hicho kitambulisho ni kwa ajili ya nini

Kusumbua watu
Kupotezea watu muda
Be smart
Kama hakina maana kwako kaa kimya, usipende tukuone mjinga. Na hiyo hajalazimisha. Mpaka kasema vijana mtoke maana yake anahimiza, hajamlazimisha mtu aisee. Kaa kimya, usionekane mpumbavu.
 
Kuna maana gani ya kuwa na kitambulisho cha mpiga kura ikiwa kila mara natakiwa kujiandikisha?
Kama kitambulisho unacho kaa nyumbani tulia subiria daftari. Ni muhimu kuregister eneo ulilopo. Kama utapiga kura. Kama huto basi unakausha tu.
 
Mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam. Jiandikishe kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 17-23 Machi, 2025 ili kushiriki Uchaguzi Mkuu.
images.jpeg
 
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Dar es Salaam utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 17 hadi 23 Machi, 2025 ambapo wapiga kura wapya 643,420 wanatarajiwa kuandikishwa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndugu. Kailima, R. K kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Machi, 2025.

"Leo tupo hapa Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa huu, ambapo zoezi litafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 17 Machi, 2025 na kukamilika tarehe 23 Machi, 2025 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni," amesema Jaji Mwambegele.

Amesema mkoa wa Dar es Salaam ndio wa mwisho kwenye awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Dafatri ambayo ilizinduliwa mwezi Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika kwenye mikoa 28 na kwamba mikoa ya Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga inatarajiwa kukamilisha zoezi hilo tarehe 07 Machi, 2025.

"Hadi leo tarehe 05 Machi, 2025 Tume imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari katika Mikoa 28. Kwa mujibu wa ratiba, kwa sasa Tume imeanza maandalizi ya mzunguko wa 13 ambao ni mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu unahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Aidha, zoezi la uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa wa Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga unaendelea tangu tarehe 01 Machi, 2025 na utakamilika tarehe 07 Machi, 2025," amesema Jaji Mwambegele.

Akiwasilisha mada kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndugu. Kailima, R. K amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

"Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na wapiga kura 4,071,337," amesema.
Siku ziongezwe watu bado ni wengi hawajaboresha taarifa
 
  • 5811771-84b12f6d5ff81d807821a183416ac2ed.mp4
    648.4 KB
Back
Top Bottom