Ubora wa UDSM upo wapi?

Ubora wa UDSM upo wapi?

UBORA WA UDSM.

Pamekuwa na msuguano mkali kuhusu ni nini hasa kinapelekea Udsm kuwa chuo bora hapa nchini na Afrika kwa ujumla.

Aidha wapo mahasimu wanaokibeza kwa kejeli na vijembe visivyo na kichwa wala miguu. Kutokana na haki ya kutoa maono basi ni wazi hawakosei kwani hutekeleza haki yao ya kutoa maoni ambayo ipo kikatiba.

Mimi ni Mhitimu wa chuo hicho bora. Ninajivunia kusomea chuo hiko. Nimeshiba kile nilichokusudia kukipata. Ninaouwezo wa pambano lolote kulingana na taaluma yangu.

Yafuatayo ni moja ya mambo yanayofanya Udsm kiwe chip Bora nchini kama si Afrika;

1. Mchakato wa udahili na wadahiliwa.
Udsm ndio chuo pekee kinachodahili wanafunzi wenye ufaulu mkubwa ukilinganisha na vyuo vingine.
60%= wanadivisheni one.
25%= divisheni two.
15%= divisheni three.

Utaona ni kwanamna gani Udsm ilivyobora kwa upande wa Input( wadahiliwa).

2. Uwepo wa Maprofesa na madokta wakutosha.
Udsm kina Ghala la maprofesa na madokta wakutosha. Ndio chuo pekee Tanzania chenye maprofesa wakutosha ukilinganisha na Vyuo vingine. Hata barani Afrika ni miongoni mwa vyuo vyenye maprofesa wengi wakutosha.

3. Miundombinu
Miundombinu kama Maktaba kubwa, Usafiri kwa wanafunzi, Hostel kwa sasa changamoto imepungua kama si kuisha, Viwanja vya michezo na burudani, vimbweta vya kusomea, miundombinu ya wa maji, Kafteria n.k.
Miundombinu hii hukifanya Chuo hiki kiendelee kuwa bora japokuwa kinakumbwa na uchakavu wa baadhi ya miundombinu kama choo na baadhi ya hostel kama hall 4&5.

4. Uwepo wa miradi Miradi.
Udsm kina miradi kadhaa ambayo imekuwa na manufaa kwa chuo na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya Miradi ni pamoja na Uwepo Wa Shuttle zinazosafirisha wanafunzi kutoka Main Campus mpaka mabibo.

Uwepo wa Mlimani Tv ambayo inatoa huduma ya habari, Matangazo ya biashara na huduma zingine. Ndio chuo pekee chenye Channel ya TV.

Pia mradi wa Mlimani City Mall inayoendeshwa na kamapuni ya Nakumati. Mlimani city imeufanya Jiji la Dar es salaam kuwa bora na maarufu.
Bila shaka mtu ambaye hajafika Mlimani City atakuwa bado hajaonja utamu wa Dar es salaam.

5. Hali ya Hewa na Mazingira yake
Hali ya hewa ya Udsm ni yakuridhisha. Udsm imezungukwa na miti kila pahala, hivyo vivuli kila mahali jambo linalofanya wanafunzi wafurahie mazingira. Pia kuna Viumbe kama tumbili ambao wanaongeza upekee wa chuo hiki.

6. Uwepo wa Wahitimu Mahiri.
Mbali na Ukongwe wa Chuo hiki na umahiri wake wa Maprofesa na Wahitimu mahiri kama Tundu Antipus Lisu, Zito zuberi Kabwe, Jakaya Mrisho Kikwete, John pombe Magufuli, Halima Mdee n.k.

Kwa kifupi Udsm bado kipo makini na ubora wa kutosha japokuwa kina changamoto zake.
 
mleta mada unaidharau udsm wakati kuna rafiki yangu ameapply apo ile course ya kuogelea ili mradi tu ndoto zake za kusoma chuo kikuu cha dareslaam zitimie[emoji28] [emoji28]
NB:Ukisema chanini wenzio wanasema watakipata lini?
 
Hahaaaaa anataka PhD ya kuogelea???
 
Naombeni wana UDSM au wakereketwa wa UDSM ifike Mahala tusibishane na hawa wa vyuo Vingine...Maana wao kila Product wanataka ku compare na ya UDSM...ieleweke tu UDSM is the Best ever University in Tanzania and EAST AFRICA
 
We umesoma wapi????? Hahaha usije kuwa umesoma chuo ambacho hata hakina maprofesa au mnakopa wa udsm halafu unakuja kutoka povu hapa.
 
UBORA WA UDSM.

Pamekuwa na msuguano mkali kuhusu ni nini hasa kinapelekea Udsm kuwa chuo bora hapa nchini na Afrika kwa ujumla.

Aidha wapo mahasimu wanaokibeza kwa kejeli na vijembe visivyo na kichwa wala miguu. Kutokana na haki ya kutoa maono basi ni wazi hawakosei kwani hutekeleza haki yao ya kutoa maoni ambayo ipo kikatiba.

Mimi ni Mhitimu wa chuo hicho bora. Ninajivunia kusomea chuo hiko. Nimeshiba kile nilichokusudia kukipata. Ninaouwezo wa pambano lolote kulingana na taaluma yangu.

Yafuatayo ni moja ya mambo yanayofanya Udsm kiwe chip Bora nchini kama si Afrika;

1. Mchakato wa udahili na wadahiliwa.
Udsm ndio chuo pekee kinachodahili wanafunzi wenye ufaulu mkubwa ukilinganisha na vyuo vingine.
60%= wanadivisheni one.
25%= divisheni two.
15%= divisheni three.

Utaona ni kwanamna gani Udsm ilivyobora kwa upande wa Input( wadahiliwa).

2. Uwepo wa Maprofesa na madokta wakutosha.
Udsm kina Ghala la maprofesa na madokta wakutosha. Ndio chuo pekee Tanzania chenye maprofesa wakutosha ukilinganisha na Vyuo vingine. Hata barani Afrika ni miongoni mwa vyuo vyenye maprofesa wengi wakutosha.

3. Miundombinu
Miundombinu kama Maktaba kubwa, Usafiri kwa wanafunzi, Hostel kwa sasa changamoto imepungua kama si kuisha, Viwanja vya michezo na burudani, vimbweta vya kusomea, miundombinu ya wa maji, Kafteria n.k.
Miundombinu hii hukifanya Chuo hiki kiendelee kuwa bora japokuwa kinakumbwa na uchakavu wa baadhi ya miundombinu kama choo na baadhi ya hostel kama hall 4&5.

4. Uwepo wa miradi Miradi.
Udsm kina miradi kadhaa ambayo imekuwa na manufaa kwa chuo na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya Miradi ni pamoja na Uwepo Wa Shuttle zinazosafirisha wanafunzi kutoka Main Campus mpaka mabibo.

Uwepo wa Mlimani Tv ambayo inatoa huduma ya habari, Matangazo ya biashara na huduma zingine. Ndio chuo pekee chenye Channel ya TV.

Pia mradi wa Mlimani City Mall inayoendeshwa na kamapuni ya Nakumati. Mlimani city imeufanya Jiji la Dar es salaam kuwa bora na maarufu.
Bila shaka mtu ambaye hajafika Mlimani City atakuwa bado hajaonja utamu wa Dar es salaam.

5. Hali ya Hewa na Mazingira yake
Hali ya hewa ya Udsm ni yakuridhisha. Udsm imezungukwa na miti kila pahala, hivyo vivuli kila mahali jambo linalofanya wanafunzi wafurahie mazingira. Pia kuna Viumbe kama tumbili ambao wanaongeza upekee wa chuo hiki.

6. Uwepo wa Wahitimu Mahiri.
Mbali na Ukongwe wa Chuo hiki na umahiri wake wa Maprofesa na Wahitimu mahiri kama Tundu Antipus Lisu, Zito zuberi Kabwe, Jakaya Mrisho Kikwete, John pombe Magufuli, Halima Mdee n.k.

Kwa kifupi Udsm bado kipo makini na ubora wa kutosha japokuwa kina changamoto zake.
Mwambie atoe sifa za chuo alichosoma yeye sasa.
 
Trump mwenyewe lugha yake inamchanganya
Screenshot_2017-11-12-04-24-38.png
Screenshot_2017-11-12-04-24-38.png
 
= Nani
= Kakwambia
= Sijui

Hii aina ya uandishi ndio mnafundishwa kwenye chuo chenu?

Je mpaka hapo mimi na wewe ni nani mpumbavu?
Upepo wa kweli umeonyesha njia sahihi ya kumfundisha mtu aliye jaa hasira namna ya kupambana nae. Ni wazi Mtanganyika wa kweli hatakujibu hovyo tena na matusi kama "...mpumbavu nk" ameacha kuyatumia. Ukitaka kuthibitisha hili, angalia jibu lake lililofuatia baada ya ukosoaji huu.
Hiyo ndio tofauti iliyopo ya products za UDSM na vyuo vingine!
 
Ukifail na ukasoma vyuo vya kata hili lazima litakuhusu na ukilibeba sana moyoni utaumia

Udsm ndio state university
We piga porojo tu
 
Kuishi kwako kote ndo unaona leo maneno ya ufupisho....duh... Complications nyingi kwelikwelii...
Fupisha kwenye barua ya kuomba kazi, au fupisha kwenye majibu ya mtihani ndipo utajua kumbe sio kila mahali pa kufupisha
 
Kwa kuongeza tu
Mimi mpka sasa sijalipia Ada na nimelipia Hostel na naishi hapa Udsm(JpM) na nasubiria kama mkopo nikikosa ila huwezi kuamini nimekuwa nikihudhuria lecture zote week nzima na naisubiri io batch4 kama sipo hapo nakalipie ili niishi kwa amani.kwa sababu ninausajili wa awali tu naweza kufungua Aris yangu lakini na shindwa kusajili cozi yangu.

Sizani kama kuna chuo kinaweza kunisaidia tatizo langu nahisi ningekuwa bado nipo nyumbani au mtaani napunyanga,ila hapa nilipofikia naona imenidhihilishia ni chuo bora Kwa Ukanda Wa Afrika Mashariki.

Hekoo Udsm

Home Of Interllectual
 
Hahaaaaa anataka PhD ya kuogelea???
Hahha [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ndoivo mkuu, unajua udsm ni chuo bora sawa hatukatai ila sasa kinacho matter ni course mtu anayoisomea apo mlimani. Yan unakuta mtu yupo tayari kusoma udsm course yoyote tu ili mradi na yeye aonekane kwenye daladala amevaa kitambulisho cha udsm.
 
nan kakwmbia cjui?;umeona upumbavu wako? unajua aina ngapi za uandishi?
huu ni mtindo wa uandishi,hata kwenye mashairi unaruhusiwa kudondosha herufi ili lengo lako litimie!
Udondoshaji wa silabi si sahihi katika lugha ya kiswahili
Udondoshaji wa silabi katika ushairi ni lazima neno linalo baki liwe na irabu lisiwe na konsonati tupu kama ulivyofanya kwenye WW badala ya Wewe

Mm naamini uliyekuwa unamwambia amekuelewe ila kwa sababu uliweka neno mpumbavu naye akaona ni vyema kunyambulisha upumbavu wako kupitia maneno uliyoandika

Wito!
Tuacha matusi tujenge hoja sote Tu wamoja
 
We cha msingi tafuta chuo chako unachoona ni Bora na kitangaze kwa maana Udsm sio wao wanaotoa orodha... Na je unajua wanatumia vigezo gani ?? Umiza ndonga we mtoto
 
Back
Top Bottom