Ubora wa Taifa lolote hutegemea ubora wa mawazo ya watu wao

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Leo sina mengi nawakumbusha ya kwamba ubora wa Taifa lolote lile hutegemea sana na ubora wa mawazo ya watu wanaounda Taifa hilo pamoja na nidhamu ya watu wao. Kwa kuwa mtu ni mawazo anayofikiri na jamii pia huundwa na mawazo basi kama jamii yetu sio bora tuangalie upya mawazo yetu.

Tujenge upya Taifa letu, familia zetu na jamii yetu katika fikra sahihi. Baadae yetu itategemea ubora wa fikra zetu na maamuzi yetu tutakayofanya kwa faida ya kesho. Naona Taifa hili kufika mbali ikiwa tu tutabadili mwelekeo wa mawazo yetu.
 
Sina hakika sana kuwa sisi kama taifa tunao watu wanao fikiri sawa sawa!!!
Nikiangalia kuanzia Ikulu,bungeni,makanisani na misikitini aina ya viongozi na wanao ongozwa,sioni mwisho mwema wa taifa letu!!!
 
Leo sina mengi nawakumbusha ya kwamba ubora wa Taifa lolote lile hutegemea sana na ubora wa mawazo ya watu wanaounda Taifa hilo pamoja na nidhamu ya watu wao. Kwa kuwa mtu ni mawazo anayofikiri na jamii pia huundwa na mawazo basi kama jamii yetu sio bora tuangalie upya mawazo yetu.
Ni ukweli usiopingika ubora wa taifa utokana na mawazo ya jamii katika muda, tatizo ni nani anahusika na responsibility kwa sasa ndani ya Tanzania. The primary influencer yaani wazazi wengi bado wana rely na tradition socialization huko vijijini to input thoughts kwa vizazi vijavyo.

Mara tu waanzapo shule vijana wa leo na kuchanganyika na vijana wa kutoka sehemu zengine ambao wana-different background they find themselves needing to adjust their thought to have common ground with their fellow student.

Inturn their earlier primary socialization processes begin to be challenged with many other ideologies that exist and they have to pick and choose what should guide them in the next phase of adulthood, the choices they encounter are religious ones ambayo imezalisha udini, lifestyles (choices) which are highly influential with orgins of foreigns propaganda mfano (tabia ya watu kujiona ma-celebrity or aspire to be considered one) whilst adapting the lifestyles of other cultures and thinking largely (hili uonekane wa juu) and also our mainstream medias and their thirst for gossips, lies and moral corruption reporting also exacerbate in the dilution of our moral at the same time corrupting the minds and its thinking procedures (valuable information to feed the minds reasoning).

With all the ideologies that exist minus the government intervention through nationalism propaganda at schools levels and on national medias, Tanzanians are largely confused of their belonging and their identification as a whole matokeo yake udini, ushamba (OK mimi binafsi Im not all that lakini mungu wangu kuna watu ninaowajua vizuri kabisa picha wanazotaka kuzitoa kwa watu azilingani kabisa na uwezo wao kibaya zaidi when these people believes on their own hype). And this is a serious national problem hata ukiingia jukwa la siasa utaona dharau watu wanazotupiana kutokana na lifestyles zao au social positions they hold, we have a big problem here because many minds aspire for unrealistic or goals of attaining those status at any cost (wake wa wazungu, emphasis ya kuonekana unajua kizungu, tabia za kuchagua watu wakuongea nao, etc) as this is one way one earns social respect.

Dhana ya kujitambulisha kuwa mimi ni mtanzania kwanza inapotea ndani ya tanzania, madhara yake undugu mshikamano
nao unapotea (Chadema have little to be blamed with their tactics) na serikali ya CCM for the remainder kwa kupuuzia sanaa za nyumbani na kuja na sera mbadala za propaganda ya utanzania hili watu waweze kufikiria kitaifa sio tu baina ya majirani bali hata walinzi wa mariasili waweke utaifa mbele.

Ndipo hapo napomuona JKN alikuwa a genius of his time he managed to build a strong nation waliofuatia ilikuwa kuendeleza utanzania ambao tayari ulikuwa umeshawekewa strong foundation, wao sanasana wajikite kwenye maendeleo ya kiuchumi na kuendeleza propaganda zilizoachwa.

Sasa hata makashimakashi ya mbio za mwenge unawashinda na kuelezea the symbolism of such a patriotism festival wakati naambiwa huko vijijini mwenge ukupita ilikuwa ni kama national day (JKN huyo huyo nchi akaenda kumuachia kilaza this is where i dont understand him) leo ndio tunachovuna amna mawazo ya pamoja zaidi ya ki-maslahi (hiwe kisiasa, maendeleo ya tmu, iujirani mwema let alone utanzania).

That is just the social aspect of thinking sasa ukitaka kuongelea dhana nzima ya maendeleo ni maelezo mengi. Maana hili hivyo vitu vije lazima taifa liwe na watu wenye akili (enough investment is needed) thereafter every thing gets political with policies and government investment, many of us can not influence those changes, well unless you speak directly to Mr President and on regular bases you might be able to influence on those changes by advising him on how to shape the mindset (a lot of money is needed though).
 
Watu huweza kutengenezwa kuwa na FIKRA BORA juu ya taifa lao! Kujenga FIKRA bora si mchezo wa kubahatisha, ni HESABU TU! Tangu kuzaliwa kwake mtoto, aone na asikie nini na kipi asione wala kusikia? Ajifunze na Afundishwe nini?

Yaani kipi kiwe ni general experience ya watu wetu, AISHI NINI NA KIPI ASIISHI?

Hicho ndicho kitakacho-shape FIKRA BORA ama MFU! Ndio maana imeshanenwa na haitaacha kunenwa kuwa, ITIKADI KUU YA TAIFA ndio muarubani wa matatizo yetu YOTE, iwapi? Kwanini tunaipuza? Imani ya kuwaandalia watoto wetu mema inatoka wapi? Tusitegemee Viongozi zaliwa toka FIKRA MFU kutufanyia lolote jema, ni SISI WENYEWE na muda ni LEO. Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu. Ubunifu haujawahi kufika mwisho!

Mungu wetu anaita sasa!
 
Aksante wakubwa kwa michango yenu.

Mambo mengi mliyoyaongea yako sahihi. Lakini mimi naamini Viongozi wana nafasi kubwa katika kujenga general thinking ya jamii yetu na kuna uhusiano mkubwa kati ya ubora wa mawazo ya viongozi na character ya nchi. Mwelekeo wa Taifa letu utategemea sana ubora wa viongozi tulionao.

Lakini pia Elimu pia inahusika hapa. Aina ya elimu tunayowapa wananchi wetu je ni yenye kujenga mtazamo gani kwa watu wetu juu ya Taifa letu? Vyombo vyetu vya habari kama mtu mmoja alivyosema vina wa vinawalisha nini watu wetu? Je ni watu wa aina gani wanaviendesha? je wanauelewa wa kutosha wa kutoa maarifa kwa umma? Wanasiasa wanawalisha mitazamo gani wananchi?
 
Ubora wa mawazo ya watu unaonekana kutoka kwenye ubora wa mnawazo ya viongozi wao.

Dah! Mkuu Kichuguu heshima mbele...usipotee sana namna hiyo.....

kwa faida ya wengi......unaweza ukai-qualify hiyo statement yako?

kwa mfano wa lile swali...."Kwa nini Tanzania ni Maskini"...je laweza kuwa kiwakilishi cha statement yako.... regardless of the answer being negative or positive....
 
Dah! Mkuu Kichuguu heshima mbele...usipotee sana namna hiyo.....

kwa faida ya wengi......unaweza ukai-qualify hiyo statement yako?

kwa mfano wa lile swali...."Kwa nini Tanzania ni Maskini"...je laweza kuwa kiwakilishi cha statement yako.... regardless of the answer being negative or positive....

Mzee Ogah, ngoja nijaribu kidogo.

Viongozi wa nchi ni watu walionadi mawazo yao kwa wananchi wakati wa kuomba kura. Sasa iwapo wananchi walikubaliana na mawazo hayo na kuwapa kura basi mawazo ya viongozi hao ndio reflection ya mawazo ya wananchi. Inawezekana wewe na mimi hatukubaliani na mawazo ya viongozi hao ila kwa misingi ya demokrasia, mawazo ya wananchi wengi ndiyo mawazo ya nchi: UNFORTUNATELY.

Siamini kuwa kuna uwezekano wowote wa wananchi kuwa wamehadaliwa kwa vile wamekuwa wakiendela na maisha yaoa kama kawaid hadi leo kama vile hakuna lolote serikalini linalowahusu.
 
Mzee Ogah, ngoja nijaribu kidogo.

Viongozi wa nchi ni watu walionadi mawazo yao kwa wananchi wakati wa kuomba kura. Sasa iwapo wananchi walikubaliana na mawazo hayo na kuwapa kura basi mawazo ya viongozi hao ndio reflection ya mawazo ya wananchi. Inawezekana wewe na mimi hatukubaliani na mawazo ya viongozi hao ila kwa misingi ya demokrasia, mawazo ya wananchi wengi ndiyo mawazo ya nchi: UNFORTUNATELY.

Siamini kuwa kuna uwezekano wowote wa wananchi kuwa wamehadaliwa kwa vile wamekuwa wakiendela na maisha yaoa kama kawaid hadi leo kama vile hakuna lolote serikalini linalowahusu.

Kuna tatizo kubwa la ufahamu wa kuchanganua mambo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom