Azpilicueta
Member
- Sep 8, 2021
- 86
- 92
Habarini za jioni wapendwa..
Kwa mujibu wa sensa kama nchi tuna idadi ya watu million 60 ambayo ni idadi kubwa kweli ukilinganisha na majirani zetu , lakini kwangu mimi hawa ni watu waliolala kwa maana kimsingi kama Taifa halina uzalishaji unaoendana na idadi ya watu 60m, nikisema uzalishaji namaanisha bidhaa za mwisho kwenda kwa mtumiaji sio malighafi.
Taifa linalotaka kukua na kukuza kipato cha wananchi wake lazima liwe na mipango ya kuhakikisha watu wake wana nguvu na wenye weledi wa uongezaji thamani rasimali zinazo wazunguka. Bila uzalishaji wa bidhaa zenye thamani na kuongeza wigo wa uzalishaji wa bidhaa kati ya Mtu na mtu umaskini hautakaa uishe kwa wananchi wa chini walioishia zao la saba au form four wasio na ujuzi wowote.
Ukizunguka dar e's salaam kuna idadi kubwa ya vijana wanaofanya shughuli siziso na kueleweka mwisho ni wizi kwa maskini wenzao, tunaishia kuwajaza magerezani ama kuwaua watanzania wenzetu waliokosa dira na kuingia pabaya.
Kwanini tusielekeze nguvu katika miradi ya kimkakati itakayogusa uinuaji wa maarifa ,uelewa na uwezo wa uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na zitakazokubalika na jamii ya nje ya Taifa letu.
Kwa mfano ,Moja kwa kuainisha maeneo gani hasa tunataka kuya angalia na kuyatafutia maarifa ya kuyatengenezea bidhaa kwa kuangalia malighafi adimu duniani na inapatikana ndani ya Taifa letu. Pili kuangalia sera zetu kwa madhaifu na ubora wake then kuja na sera imara zaidi inayo toa muongozo juu ya malighafi hizo, kuwa na Sera ya Taifa ya standardisation kwa kila eneo la uzalishaji ili kuwa na miongozo mbalimbali ya uzalishaji bidhaa zenye ubora usiomithilika machoni pa mteja.
Mwisho kuona njia itakayotumika kuwachukua vijana na kuwatumia katika miradi hiyo, lakini hasa njia itakayotumika kuwaongezea maarifa vijana hao. Tunasema tukaboresha mazingira ya Wawekezaji,lakini wawekezaji hawawezi kuja kuweka ela kwenye Taifa linalokosa skilled labor!
Unafikiri njia gani hasa tunaweza kutumia kama Taifa kupunguza watu na kuongeza rasilimali watu?