Uber, Bolt kurejesha huduma Tanzania

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,167
16,257
Arusha. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesema, kampuni za usafiri kwa njia ya mtandao Bolt na Uber zinatarajia kurejea kutoa huduma za usafiri nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Septemba 12, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Latra wametoa taarifa hizo kipindi ambacho kampuni hizo kwa nyakati tofauti, walisitisha kutoa huduma za usafiri za magari na kubaki na bodaboda pamoja na bajaji.

Suluo amesema wamesikia kilio cha kampuni hizo na wameitana kukaa meza moja kwa mazungumzo na tayari wamekubaliana kutatua tatizo ili kurejesha huduma.

"Uber walijitoa baada ya tangazo la Latra la nauli na tiketi za mtandao ambao uliwataka kutoza tozo haalali kwa amri ya kutekelezwa na wakafungua kesi Baraza la Ushindani kupinga maamuzi yetu.”

“..Bolt waliendelea kutoa huduma lakini baadae nao wakaleta taarifa kuwa wanaenda kusitisha huduma lakini tuliwaita tukiamini katika mazungumzo" amesema Suluo

"Tuliwaita wakaja na wawakilishi wao wa Afrika, tukaanza Septemba 5-8, 2022 tumemaliza mazungumzo ambapo kuna taarifa tunataka watuletee kimaandishi ili kutoa maamuzi na leo ndio mwisho wa mda tuliokubaliana na tutatoa maamuzi yatakayowasaidia wote wakiwemo umoja wa madereva teksi (TODA)," amesema mkurugenzi.

Chanzo: Mwananchi
 
At least serikali imeonesha werevu, wakati mwengine waache kukurupuka bila kushirikisha wadau.

Hofu yangu ni kwamba baada ya siku chache serikali inaweza kuingiwa tamaa tena na kurudi walipoanzia.
 
Ukiwa na Gari km Toyota Corolla Allex cc 1400 inakubaliwa kusajili Bolt, Uber na hao wengine Ping na Taxify, napia naona Taxi nyingine zina plate number za njano hii imekaaje au wanalazimisha tu? Na gharama zipoje za kujisajili kuanzia huko Latra mpaka ktk hizi kampuni za taxi mtandao.......natanguliza shukrani kwenu🙏
 
Back
Top Bottom