St Lunatics
JF-Expert Member
- Aug 29, 2015
- 6,644
- 11,201
Kuna mbeba boksi mmoja nchi za Ulaya alikwenda huko kutafuta maisha sasa baada ya miaka kama saba(7). Alifanikiwa kupata uraia wa nchi hio ndio akaanza kufanya mipango ya kuivuta familia yake yote huko ughaibuni (mkewe na watoto wake). Katika kuanza mipango akatakiwa kujaza form zote na kwenda kwa daktari kwa kupima afya na kuangaliwa DNA kama hawa watoto wake wa kuwazaa (biological kids) kweli.
Mkewe alikuwa ndio mtu wa mwanzo kufanikiwa katika kupata visa ya huko Ughaibuni wakabakia watoto wake wanne(4). Baada ya kama wiki jamaa akaitwa aende ofisi ya ubalozi kwasababu aliambiwa kuna masuala anatakiwa kuulizwa. Bila ya kukosa siku ya appointment yake jamaa alifika ubalozini na zamu yake ikafika na kuanza kuhojiwa.
Katika kuhojiwa akaulizwa unataka kuidanganya serikali kwa kuforge document za birth certificate za watoto? Jamaa akasema hapana hao wote ni wanangu wa kuwazaa na mke wangu. Mtoto wa kwanza akiwa na miaka 15 wa pili 13 wa tatu 10 na wa mwisho ni miaka 9 watatu ni wa kiume mmoja wa kike.
Ndipo officer wa ubalozi akatoa zile karatasi za daktari za DNA na kumuonesha jamaa na zina alama za Negative kwa watoto wote. Mbeba boksi akaanza kulia na machozi yakimtoka huku yule mfanyakazi wa ubalozini akijaribu kumfariji, hapo jamaa na kumwambia yule afisa wa ubalozini kuwa cancel application zote za mkewe na watoto wake na kuondoka zake. Huyu jamaa hakurudi tena kwa mkewe na kufanya safari ya kurudi zake ughaibuni sasa ni mwaka wa 2 huu hajawasiliana na mkewe wala wanawe.
Dada zetu kuweni na huruma za kuwabambika waume zenu watoto wa wanaume wengine.