Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Teleza ni jina linalomaanisha aina ya ubakaji unaotokea ndani ya kata ya Mwanga Kusini katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.
Jina hili lilitokana na kwamba, wakati wa usiku kuna wanaume wamekuwa wakiingia kwenye nyumba wanazoishi wanawake na kuwabaka. Watu hawa kabla ya kufika kwa mwanamke mlengwa huvua nguo zote na kubaki kama alivozaliwa, kisha wanajipaka grease ama mafuta ya kula mwili mzima. Baada ya hapo hubeba silaha aina ya kisu kikali ama mapanga, huvunja, ama hubomoa na kuingia kwenye nyumba anamoishi mwanamke kwa nia ya kubaka, kujeruhi, kuharibu mali na kuiba.
Simulizi kutoka kwa binti wa kidato cha tatu aliyeshuhudia unyama huu wa TELEZA.
Tukio hili lilitokea mwaka jana nikiwa form two. Tunaishi kwenye nyumba ya kupanga na tunapanga chumba na sebule. Tunaishi na mama yetu pekee, tukiwa watoto watano wa kike. Siku ya tukio, ndugu zangu wawili walikuwa wamekwenda kijijini. Na hapo tulikuwa na mgeni ambaye alikuja kututembelea akiwa na katoto ka kiume miaka kumi. Mtoto wa mama mkubwa. Mtoto wa kiume huyu mwenye miaka kumi alilala kwenye kochi sebuleni. Sisi wasichana tulilala chumbani na mama yetu siku hiyo alienda kulala kwenye msiba hapo jirani.
Tukiwa tumelala usiku wa manane, hatukusikia kitu chochote, japo mdogo wetu wa kiume aliyekuwa sebuleni alisikia huyu kijana jinsi alivyovunja kioo cha kwenye dirisha na kufungua mlango. Alijifanya amelala kwa woga.
Yule TELEZA alipingia ndani alienda moja kwa moja kwa yule mtoto kwenye kochi akamvua nguo na kumchunguza. Alipogundua kwamba ni wa kiume akamuacha ndo akaja chumbani kwetu.
Mimi binafsi sikumsikia akiingia chumbani bali nilimsikia akimlazimisha dada yetu (Mgeni) avue chupi na wakati huo huo akimtishia kwa panga. Ndipo na mimi nilistuka, na wadogo zangu wengine walistuka na kuanza kupiga kelele. Alitupiga kwa mapanga na mara nyingine alitukata kwa hilo panga lake. Tulizidi kulia kwa hofu maana tiyari tulishaumizwa sana.
Alipoona hatunyamazi akachukua mwiko mkubwa na kuanza kututandika nao. Wote tulikuwa tunajificha nyuma ya dada yetu ambaye aliumizwa Zaidi. Baba mwenye nyumba alisikia lakini walishindwa kutoka kwasababu walifungiwa nje pamoja na majirani wengine.
Walianza kupiga simu kwa mama, na mpaka watu wanafika tiyari tulishaumizwa vibaya sana. Dada yetu alizimia. Tulikimbizwa police na hatimaye kukimbizwa hospitali na kushonwa nyuzi tano tano kila mmoja wetu.
Tukio liliniogopesha sana. Lakini baada ya hapo jamii na shuleni ndio kuliniogopesha Zaidi. Nilitamani kuhama shule na nikamwambia mama yangu, lakini kwa kuwa hana uwezo na tiyari alishaingia gharama za kutufanyia matibabu ambayo ilibidi auze godoro moja ilibidi nivumilie tu.
Shuleni wanafunzi walinitania saana kwa kuniita majina na kwamba mimi ni mke TELEZA. Lakini nilijikaza mpaka sasa wanaonekana wamesahau, labda mara moja moja mtu aamue tu kunichokoza kwa kuniita mke wa TELEZA.
Kwasasa siwezi kubeba kitu chochote kichwani kwani nilikatwa mapanga ya kichwani. Na dada yangu alimaliza mwezi mzima akivuja damu puani. Alivyopona aliondoka.
Mama wa binti
Mimi biashara zangu ni kuuza dagaaa sokoni. Siku tukio limetokea sikuwa na pesa hata kidogo. Lakini ilibidi nikope kwa watu ili niweze kukodi tax itupeleke police ajili ya kupata PF3 kwa watoto 2 ilikuwa elfu 10,000. Kisha taxi hiyo ikatupeleka hospitali ambako walishonwa kwa elfu 30,000 kwa kila mtoto na kununua madawa kwa ajili ya matibabu.
Hizi pesa hazikuwa kwenye mpango wangu na ilibidi niuze godoro la watoto ili niweze kulipa madeni ya matibabu.
Jamii bado walisema kwamba huyu TELEZA alikuwa ni bwana wangu kwa kuwa mimi sina mume alishafariki. Na wengine waliongeza kuwa nimekula pesa za hao vijana ndio maana wamewaingilia watoto wangu. Hii sentensi ilikuwa inanihuzunisha sana kwani nilihofia kama watoto wangu wataamini wataniona mimi ni mbaya. Nashukuru Mungu walielewa tu.
NA mtoto wangu wangu wa mwisho naona tangu siku hiyo amekuwa mgonjwa kabisa. Hayuko vizuri kiakili. Maana alishuhudia tukio zima. Sasa amebaki na woga wa hali ya juu sana. Ikiingia jioni anaanza kujikunyata na kusikia baridi sana. Hayuko sawa kabisa.