Ubadhirifu Ofisi ya CAG

Ubadhirifu Ofisi ya CAG

Naomba mnieleweshe wadau. Hivi ni nani anakagua hesabu sa CAG?
Hili ni jipu kubwa sana serikalini!! Wakianza ukaguzi katika taasisi ya umma wanatoa vitisho kwa lengo la kupata rushwa na wakiona hamtishiki basi watatoa hoja ambazo hazina miguu wala kichwa!!!

Kwa kifupi ofisi hii haikaguliwi na taasisi yo yote nchini na pia CAG mwenyewe ana kinga ambayo hata Rais hawezi kumchukulia hatua!!!
 
Naona huko Mtanzania kuna mradi wa kumchafua Prof.Asad,walianza na kwenda nje bila kibali.Na huyo afisa wa CAG anayetumiwa tutampata tu,asidhani yupo salama
Mkuu mimi sikutaka kuzungumza mengi lakini jambo hili li wazi, mlengwa mkuu wa upuuzi huu ni huyo Prof. wa watu!!! Hawana hata aibu vyeo havitafutwi kwa njia ya kihuni na fitina - piga kazi kwa uwadirifu mambo mengine yatajipa yenyewe.
 
Mimi naona kuna kila dalili la kutaka kumchafua Prof. Na tatizo kubwa ni watu wamekatiwa mirija waliyokuwa wakitumia kuinyonya serikali. Lakini baada ya muda ukweli utajulikana. Mungu yupo!!!
 
Ajira zimekua kama kufanya biashara kuaharibiana ili mwingine apate soko..hata kama ni mtendaji mzuri..habari ipo ipo tuu harafu ipo front page...
Mkuu na kibaya zaidi unaweza kukuta sataka zima ni an inside job - afisa/mafisa walio ajiriwa katika ofisi ya CAG ndio wanasambaza disinformation hizi kwa lengo la kumchafua CAG - wasitumie hasira zao za kushindwa kupewa Cheo cha u CAG kwa kimbilia kumchafua Prof. wakumbuke Rais ana uhuru wa kumtehuwa yeyote kutoka nje au ndani ya Ofisi ya CAG na silazima atakoke ndani ya Ofisi ya CAG, kwa hiyo msimpige vita Professor wa watu.
 
M
Isome uielewe.. Mbona ipo straight forward!!
CAG kakiri kw kusema akipatikana mtoa siri atafukuzwa kazi mara moja!
Majungu tu has a gazeti LA mtanzania pro umewekwa na Mungu na atakae kuondowa ni Mungu. Wewe ni msomi wa hali ya juu hivyo vidagaa visikubabaishe piga kazi tu na hichi kipeperushi achana nacho
 
Kama kweli kuna utaratibu wa kununua magari na Ofisi yake imekiuka pamoja na ushauri walipewa na GPSA hapo hamna cha kupakana matope ni Ubadhirifu . hata suala la safari alizoenda taritabu lazima zifuatwe kama alikiuka naye ni jipu
 
Tuna safari ndefu sana wabongo! Bado hatuna nia wala utashi wa kuuita uovu/ubadhirifu kwa jina lake! Ili uovu ukemewe au utetewe unategemea "nani mhusika"! Kama ofisi ya CAG imefanya ubadhirifu, utabakia ni ubadhirifu tu hata kama watu watamtetea vipi hapa Jukwaani! Na kama ni majungu, ofisi yenyewe ya CAG ina wajibu wa kulishitaki gazeti husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake!
 
Kuchafuana ni sifa yetu watanzania, uwezo wa kuchimbana na kutafuta habari za mtu tunao tena mkubwa sana, lakini uwezo wa kufanya research za kimaendeleo ili tuweze kufaidika na rasilimali zinazotuzunguka ni zero. Inasikitisha sana.
 
Kila mtu auchukue mzigo wake mwenyewe kama amefisadi na yeye atumbuliwe tu.
 
*Yakarabati nyumba ya kigogo kwa mamilioni

*Yanunua samani, gari kinyume na utaratibu

OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, imeingia katika kashfa nzito na kudaiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za umma.

Hatua hiyo inakuja wakati Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli inapambana na kudhibiti matumizi makubwa pamoja na vita dhidi ya ufisadi.

Ofisi hiyo ambayo inaongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Profesa Juma Assad, imethibitika kufanya matumizi hayo pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

MTANZANIA limebaini katika uchunguzi wake kuwa tangu Profesa Assad alipoteuliwa kushika wadhifa huo Novemba 5, 2014 na kuapishwa Desemba 2 mwaka huo na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ofisi hiyo imebariki mambo kadhaa kinyume na maadili na majukumu yake.

UKARABATIWA NYUMBA

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo MTANZANIA inazo, Aprili mwaka jana Ofisi ya CAG ilianza mchakato wa kukarabati nyumba ya Serikali Plot namba 973 iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam inayotumiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.

Chanzo cha kuaminika kililiambia MTANZANIA kuwa kwa mujibu wa taratibu, nyumba zote za Serikali zipo chini ya Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) na taratibu zote za ukarabati hufanywa na kusimamiwa na wakala huyo.

“Lakini hapa kwetu hali ilikuwa tofauti kabisa, ofisi ya CAG iliamua kufanya yenyewe ukarabati huku ikijua kabisa inakiuka utaratibu na ikatoa kazi hiyo kwa kampuni bila hata kutangaza zabuni, hata kampuni husika haikuwa na mkataba wowote na ofisi ya CAG.

“Cha kushangaza zaidi kampuni hiyo ya M/SAfriq-Engineering and Construction Co. Ltd si ya kigeni, ni ya Waswahili wenzetu, lakini ililipwa gharama za kazi kwa dola za Marekani badala ya shilingi ya Tanzania.

“Na si kwamba ililipwa kwa wamu kama ilivyo kawaida, bali wao walilipwa jumla ya dola za Marekani 102,570 kwa mkupuo, tena hata kabla ya kuanza kazi, ambapo pamoja na gharama zikiwamo kodi za Serikali, jumla ilifika Sh milioni 281.8,” kilisema chanzo chetu.
Mtaalamu mmoja wa majengo katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam (jina tunalihifadhi), ameliambia MTANZANIA kuwa kiasi hicho cha fedha kinatosha kujenga nyumba nzuri ya kisasa ambayo inaweza kutumiwa na ofisa yoyote mwandamizi wa Serikali.

Kabla ya Profesa Assad kuingia katika nyumba hiyo, ilikuwa ikitumiwa na CAG aliyestaafu, Ludovick Utouh.


UNUNUZI SAMANI ZA NDANI

Pamoja na hali hiyo ofisi hiyo ya CAG ilikiuka sheria na taratibu za Serikali kutokana na kiongozi wa taasisi hiyo ya umma kulipwa posho ya Sh milioni 18 kwa ajili ya kununua samani za ndani ambazo hubadilishwa kila baada ya miaka mitano.

Katika kutekeleza stahiki yake hiyo, Profesa Assad alikwenda mwenyewe Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kwa ajili ya kununua samani hizo za ndani Desemba 27, mwaka juzi.

Inadaiwa katika safari hiyo CAG alikiuka sheria na taratibu za Serikali kwa kutumia zaidi ya Sh milioni 18, ambazo zinaruhusiwa kwa “KUNDI A” la viongozi kwa mujibu wa waraka wa Idara Kuu ya Utumishi (Ofisi ya Rais) namba 1 wa mwaka 2014.

Baada ya kununua samani hizo, ofisi yake ililipa fedha za ziada kiasi cha Sh milioni saba kwa ajili ya kuzisafirisha, pamoja na dola za Marekani 4,265 (sawa na shilingi milioni 9) kwa ajili ya kodi, visa na gharama nyingine za usafiri.


UNUNUZIWA SHANGINGI

Mei 13, 2015 ofisi hiyo ya CAG ilimwandikia barua Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) barua yenye kumbukumbu namba FA.242/305/01 yenye kichwa cha habari; “UNUNUZI WA GARI MOJA KWA AJILI YA MATUMIZI YA CAG TOYOTA LAND CRUISER GX-V8 200 HIGH.”

Baada ya Mtendaji Mkuu wa GPSA, J. Mwambega kupokea barua ya ombi hilo, alimjibu kwa barua ya Mei 15, mwaka jana, yenye kumbukumbu Na. CAD.124/318/01/64.

Sehemu ya barua hiyo ambayo nakala ilipelekwa kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha inasomeka; “Napenda kukujulisha kwamba ombi lako la ununuzi wa dharura halikubaliki kwa sasa kwa sababu upo utaratibu ulioandaliwa na Serikali kwa ajili ya ununuzi wa magari ya viongozi.

“Kwa kuzingatia hilo, nakushauri ulipie gharama za ununuzi wa gari hilo US $ 84,480.05 kupitia akaunti ya GPSA – UNUNUZI WA MAGARI KWA PAMOJA yenye Na. 0250095100500 ‘US$ Account’ iliyopo benki ya CRDB Bank (Plc) Tawi la Vijana, Dar es Salaam.”

Pamoja na maelekezo hayo, ofisi hiyo ya CAG ilikiuka maelekezo ya Mtendaji Mkuu wa GPSA na kununua gari hilo kwa dharura, ambapo malipo yalifanyika Mei, 15, 2015.

SAFARI YA SEYCHELLES, CHINA

Septemba 5, mwaka jana maofisa kadhaa akiwamo Profesa Assad walisafiri kikazi kwenda nchini Seychelles, ambapo Septemba 11, waliondoka nchini humo na kwenda Dubai, Septemba 12 waliondoka Dubai kwenda Nanjing (China), Septemba 19, waliondoka Shanghai kwenda Beijing na Septemba 22, waliondoka Beijing kurejea Dar es Salaam.

Uchunguzi umebaini kuwa ukiacha safari ya Seychelles ambako kulikuwa na mkutano wa wakaguzi wa hesabu, safari ya China haikuwa na uhusiano na majukumu ya kiofisi, ambapo tiketi za ndege ziligharimu Sh milioni 26.4.

Mbali ya CAG, ofisa mwingine kutoka ofisi yake, Edwin Rweyemamu, naye alisafiri kwa mzunguko kama huo, ambapo tiketi yake iligharimu Sh mil 21.7.

Ofisa wa tatu ambaye hakwenda Seychelles, lakini aliambatana na CAG kwingineko ni Elibariki Lyatuu, ambaye tiketi yake iligharimu Sh milioni 21.4.

Wote walisafiri kwa kutumia daraja la “Business Class” ambapo jumla ya gharama za tiketi zote tatu ilikuwa Sh mil 69.6, gharama ambazo zinatajwa kuwa kubwa kulinganisha na gharama halisi za safari kwenda nchi hizo, gharama ambazo hubadilika kutegemea na msimu wa safari.

Uchunguzi wa MTANZANIA ulibaini fedha hizo zilikopwa kutoka fungu la fedha za Umoja wa Mataifa (UN) zinazotumika katika shughuli mbalimbali ya ukaguzi wa hesabu, ambapo ofisi ya uhasibu ilisema katika dokezo.

Dokezo hilo linasomeka; “Lipa Sh 69,659,200 kwa ajili ya tiketi za safari ya CAG na ujumbe wake nchini Seychelles na China. Fedha hii ilipwe toka UN, lakini tukumbuke kuirudisha mara tutakapopokea mgawo wa fedha ujao.”

KAULI YA CAG

MTANZANIA ilipomtafuta Profesa Assad na kufanya mahojiano naye Alhamisi iliyopita ofisini kwake, alikataa kujadili au kuzitolea ufafanuzi tuhuma dhidi yake.

“Kwanza unajua ni makosa kuwa na nyaraka za ofisi ya Serikali, sasa kama ukiandika basi na sisi tutachukua hatua. Pia hayo yote uliyosema mimi sihusiki, watafute watendaji wakupe majibu,” alisema Profesa Assad.

Pamoja na kutoa majibu hayo, alisema atahakikisha anampata mfanyakazi anayetoa siri za ofisi na kumfukuza kazi mara moja.

Baada ya mwandishi kuagana na CAG na kuondoka, akiwa nje ya ofisi hizo, ofisa mmoja ambaye alihudhuria mahojiano hayo, alimwita na kumwomba nakala ya nyaraka husika, ambapo alipewa, lakini hakuna majibu au maelezo yoyote ambayo yalitoka baada ya hapo.

MAJUKUMU YA CAG

Kwa mujibu wa sheria, majukumu ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ni pamoja na kuhakikisha wizi, upotevu na ufujaji wa fedha na mali za umma unadhibitiwa mapema, kwa kufuata taratibu za uhasibu na kanuni za fedha.

Majukumu mengine ni kusaidia utendaji wa mara kwa mara kwa kutathmini taratibu za fedha, ili kuhakikisha kuwa zinafaa kwa wakati uliopo na zinakidhi makusudi ya kuwapo taratibu hizo.


Chanzo: Mtanzania

Si ndio CAG huyu huyu ambaye tunaambiwa amejenga msikiti ndani ya ofisi ya umma na kutumia pesa ya umma kusafiri kwenda Nairobi kuhudhuria mhadhara wa siasa kali?! JPM kazi anayo.
 
Makafiri washaanza kumchafua Alhaj Assad
Gazeti la Mtanzania linamilikiwa na Habari Corporation, na hi ni miongoni mwa makampuni ya bwn Rostam Aziz. Sijui naye ni kafiri? well, kama profesa Assad sio kafiri halafu kapiga mihela ya namna hiyo; kwa viwango vya UKAFIRI kama ulivyosema basi bora kua KAFIRI asiyemjua Mungu kuliko kumjua Mungu halafu unapiga namna hiyo. Sorry nimekumbuka, zipo dini nyingine zinafundisha kua, ukimuibia kafiri au serikali sio dhambi bali dhambi kumuibia "mwenzio" Sina hakika kama na wewe ni muumini mwa dini hiyo.
 
😳😳Kama naota vile yaani CAG anahitaji CAG kumCAG duh...............Kama ndiyo mambo yalivyo basi tukubali hakuna ofisi ya CAG kuna ofisi ya wapigaji.

Sitaki kuwalaumu tena BANDARI wala TRA pigeni tu maana nani ataMCAG, CAG
 
Gazeti la Mtanzania linamilikiwa na Habari Corporation, na hi ni miongoni mwa makampuni ya bwn Rostam Aziz. Sijui naye ni kafiri? well, kama profesa Assad sio kafiri halafu kapiga mihela ya namna hiyo; kwa viwango vya UKAFIRI kama ulivyosema basi bora kua KAFIRI asiyemjua Mungu kuliko kumjua Mungu halafu unapiga namna hiyo. Sorry nimekumbuka, zipo dini nyingine zinafundisha kua, ukimuibia kafiri au serikali sio dhambi bali dhambi kumuibia "mwenzio" Sina hakika kama na wewe ni muumini mwa dini hiyo.
Kaka WIZI hauna mlokole,Kafiri,muislam swala tano wala muislamu swala moja.Mwizi ni mwizi tu.Tusiweke dini kwenye hili.Awajibike CAG na watu wake ,dini yake haiwajibiki hapa.

Ningeomba kwenye hili tutafute ukweli tuweke IMANI za dini zetu pembeni
 
Naona huko Mtanzania kuna mradi wa kumchafua Prof.Asad,walianza na kwenda nje bila kibali.Na huyo afisa wa CAG anayetumiwa tutampata tu,asidhani yupo salama
Kaka issue ni ukweli wa matumizi mabaya ya fedha za umma,kama ametumia madaraka yake vibaya tusimtetee kwa sababu ya IMANI yake.Imani yake ni yake yeye na Mungu wake,siye tutambana kama ametumia vibaya fedha za umma
 
Kaka WIZI hauna mlokole,Kafiri,muislam swala tano wala muislamu swala moja.Mwizi ni mwizi tu.Tusiweke dini kwenye hili.Awajibike CAG na watu wake ,dini yake haiwajibiki hapa.

Ningeomba kwenye hili tutafute ukweli tuweke IMANI za dini zetu pembeni
Nimekuelewa vizuri sana mkuu lakini pia umeyasoma maandishi ya mtu niliye quote? Badala ya yeye kujikita kwenye story analaumu mwandishi kwa maana ya IMANI yake, this is why nilimkumbusha kua mmiliki wa hilo gazeti wapo dini 1 na yeye mwenyewe na huyo mtuhumiwa.
 
Naona huko Mtanzania kuna mradi wa kumchafua Prof.Asad,walianza na kwenda nje bila kibali.Na huyo afisa wa CAG anayetumiwa tutampata tu,asidhani yupo salama
Hii ni vita ya wazi juu ya Prof.Assad!kuna sura hazitakiwi serikalini kwa njama za kuunga unga
 
Back
Top Bottom