Ubachela ngoma yake ni uzeeni!

Ubachela ngoma yake ni uzeeni!

Kuna watu hawapo serious kwenye hii dunia. Yaani kuanzia 1951 mpaka leo hajapata wa kuishi nae??. Babu yako kilichomponza ni ujuaji ujuaji wa kijinga kijinga. Hii dunia ukiamua kupata mpenzi huwezi kosa. Jitahidi Ukishafika miaka 40 uwe una mke/mme au mtoto au vyote kwa pamoja.
 
na unakuta watu wanarithishwa hayo mawazo, kijana unakuta anaongea maneno hayo unajiuliza huyu haya maneno ya kutaka tu respect anayatoa wapi anayatafakari kweli?, unaanzisha familia kila kitu unakataza amri yako peke yako tu, uzeeni huko watoto wakiside na mama yao ni mambo ya kawaida sana maana licha ya kwamba mlikua mnaishi nyumba moja ila bond na watoto haikuwepo
Kweli
 
Mwingine tumemuuguza majirani watoto wa kiume kila Mmoja alishika njia yake walipoona baba yao haponi. Mtoto wa kike alitoka kujifungua alipakaa sawa ndo kaja kumuuguza mzee wake akisaidiana na majirani, mgonjwa kafariki majuzi hapo hata miaka 65 hakufika nadhani na umasikini umechangia
 
Mbona wengi tu wazee wamesha fiwa na wake zao na awawezi kuoa tena ..labda hoja yako ingeongelea watoto siyo kuwa na mke .

Kwani kuna kanuni kuwa ukizeeka mke au mume wako atakuwa hai ...? Kwani haujui kuwa mume na mke ufa kwa wakati tofauti..siyo lazima wafe kwa siku moja ...wapo wazee wengi wamebaki bila ya mke baada ya wake zao kufa mbele yao..tumia akili wacha kuwa mpumbavu kama kada wa ccm
Kichwa chako kigumu sana
 
Hapo zenji Kuna sehemu kwa maza mMoja nilikua naenda kupata chakula, sasa Kuna Mzee mMoja alikua anakija kula pale ni Mzee Sanna, yule Babu anapitia kipindi kigumu sana haya mambo ya usela ujanani sijui kataa ndoa wallah yatatutokea puani, Yani ili ale mpaka ahurumiwe Yani shida tupu ukimcheki ni msela tu wa enzi hizo tusalinsana ndugu zangu vuta nyapu hata kama ni mbibi asee vuta mkuu, sikilizia kua mpole usipo kua na hela punguza Sheria kwa mkeo, we mwanamke anachangia Kodi mara anunulie chakula watoto bado we na e unataka umpe na Sheria zako, huwezi ndoa ndoa inamtaka mume mjinga, wanao umia n madogo kibaya zaidi hawa madogo wasicho kijua maisha ya mtandaoni ni fake, wanao chochea haya mambo wengi wao wamesha kata tamaa ya maisha, wengine mashoga, wengine mahanisi, Kila mtu na sababu zake Kuna mdau ni mtu maarufu huhamasisha vijana wasioe cha kushangaza ye kaoa na ana watoto wakumbwa tu, na juzi mwanae mMoja kamaliza shule form four, na ana mke, mdogo wake kaoa mwaka Jana mwishoni hakumzuia, mpaka unajiuliza shida nini, ndoa Ina gharama zake you needs to pay lakini kuhamasisha watu wasioe huko nikupingana na mungu na mafundisho yake tusifate mkumbo hata kwa utani tu.
Wanasema kula UJANA fainali UZEENI.

Ndiyo maana watu wanaomba kwa Mungu wawe na mwisho mwema.
 
Kuna wakati huwa nakaa nafikiria, hivi nisingekuwa na mke na watoto hizi mbilingembilinge za mara huyu anahitaji ada, yule anaumwa anatakiwa matibabu, mwingine anahitaji kiatu, mara mke naye anahitaji kuvaa , bado sijahakikiaha chakula kipo . Ningezikosa hizi harakati za design hiyo maisha yangu yangwkuwa ya kulemaa lemaa sana " labda"!!???

Kwa mwanaume ukishindwa kumudu majukumu ya familia sijui utaweza nini.

NB; kuoa & kuolewa. Ni aidha unaoa au unaolewa
kujifariji tu,

hata usingeoa maisha yangeendelea tu, ila suala la wewe kuoa na kujiona uko perfect kuliko ambaye hajaoa ni kujidanganya.

maisha yapo popote ulipo, ukioa, usipooa yote ni sawa furaha, huzuni, karaha na raha zitakufuata hapohapo haijalishi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom