Ubabaishaji Kituo cha Ufundi cha Tecno

Ubabaishaji Kituo cha Ufundi cha Tecno

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,760
Reaction score
3,270
Nilinunua simu ya Tecno H7, ipo ndani ya kipindi cha warranty, imeharibika, inazima bila mpangilio. Siku niliyoipeleka pale ofisini kwao Samora, NHC 2ND FLOOR, DAR walii-flash bila kujua tatizo ni lipi, simu ikaendelea kuwa na lile tatizo, wakasema niwaachie tatizo ni hardware sio software.

Baada ya kuwafuatilia walisema wameagiza spea toka China, nisubiri wiki mbili, wiki mbili zimefika wanadai bado, walichukua spea toka Kariakoo, haijafaa, hivyo nisubiri wiki mbili zaidi waagize toka China!

Nawasihi Watanzania wenzangu kujiepusha na Wachina na hizi simu za Tecno, customer care zao ni mbovu, pia uwezo wa ufundi wao na ufanisi wa simu zao ni wa mashaka.

Nawasilisha wakuu.
.
 
Pole sana always cheap cost na wachina wanadharau sana kwa watanzania wanahisi watanzania wote wanataka vitu vya bei rahis ndo maana wanatuletea fake product
 
Wanakera sana kwa kweli hata mimi ninatumia h6 imeharibika wanasema nisubiri vifaa vitoke China mpaka ss zimepita zaidi ya wiki tatu hakuna lolote
 
Kwa watumiaji wote was tecno kama kuna mtu alishawahi kuifanyia simu yake software update iwe ya OTA au kwa PC aje hapa atoe ushuhuda.
 
Kweli tecno imekua janga.yangu m3 imegoma kuwaka hata kufrashiwa imeshindikana.
 
Masimu ya cheap ndo tatizo alafu utakuta simu zingine kama BlackBerry, Samsung etc zinauzwa bei poa tu ila jitu linang'ang'ania simu la kichina..,
 
Masimu ya cheap ndo tatizo alafu utakuta simu zingine kama BlackBerry, Samsung etc zinauzwa bei poa tu ila jitu linang'ang'ania simu la kichina..,

Hapo kwenye blackberry umekurupuka. Labda sio blackberry nnaozijua mimi
 
Natumia tecno kwa mwaka wa tatu tangu nmeinunua. Cyo zote mbovu jamani pia punguzeni ujuaji wa kujifanya mnajua cmu wakati amna uwezo huo.

hahaaa haya mkuu wamekugusa mtimani, hizi simu inategemea na matumizi yako kama ni kupiga na kutuma msg tu ni nzuri sana. Kama unatumia kwa matumiz zaidi ya hapo ni majanga. kwanza ukiwasha data tu inapata moto kama pasi yaan hata nguo inanyoosha. Zinakwama kwama hata wakati wa kutype text
 
kuna tecno feki pia... mi nnayo yangu hapa nlinunua freedom posta phantom p6 mini... yaani nimenunua mwezi wa sita mpaka sasa inapiga mzigo wa ukweli yaani haijawahi kukohoa hata siku moja.
 
kuna tecno feki pia... mi nnayo yangu hapa nlinunua freedom posta phantom p6 mini... yaani nimenunua mwezi wa sita mpaka sasa inapiga mzigo wa ukweli yaani haijawahi kukohoa hata siku moja.

Mwaka ukiisha lazima ikusumbue.
 
Hapo kwenye blackberry umekurupuka. Labda sio blackberry nnaozijua mimi

Kvp mkuu, hzi BlackBerry zanazotumia vifurushi vya kawaida ziko poa tu, mfano mm natumia q5 huu mwaka wa pili yaani kama mpya, haijawahai hata kuhema juu juu
 
Poleni sana,my NOKIA C3 IS STILL WORKING SINCE 2011 NA IMESHAANGUKA SANA,NASHINDWA KUHESABU MARA NGAPI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom