Uasi mkubwa unakuja CCM

Exactly, lile tamko la JWTZ siyo la kawaida hii nchi haipo shwari kama watu wanavyodhani na ninaposema haipo shwari nina maana ndani ya vyombo vya usalama kuna tatizo.
Itakuwa, hata Magufuli alipokuwa hoi na hata mauti kumkuta, wakubwa wanakuambia yupo ofisini akiendelea na kazi.

Siwezi shangaa kama kutakua na mikwaruzano ya chini kwa chini na mivutano.
 
Ni uasi ambao haujapata kutokea ndani ya chama cha mapinduzi CCM.. Baada ya kukaa madarakani muda mrefu sana ni kama kuna kikundi ndani yake kimejikuta kinajiona wao ndio ELITES wa hii nchi, na lolote ama chochote kinachofanyika ni lazima kipate kibali chao
Imefika mahali kikundi hicho kilichojitengenezea ukwasi na mtandao wa ajabu wenye ufadhili mkubwa wa matajiri waliojatajirikia ccm ambao si watanzania asilia kwa asilimia 100.. Kina uwezo wa nani awe nani kwenye nafasi gani

Ujio wa mwendazake ulifanikiwa kwa kiasi chake kuudhoofisha huu mtandao wa hiki kikundi lakini naye akaaza kuharibu kwa kuanza kutengeneza himaya nyingine mpya ya upande mmoja tena kwa ukatili mkubwa sana
Hapa kitisho kilikuwa wazi ni vita kati ya himaya mpya ya mwendazake vs mtandao kongwe THE ELITES ... Halafu sasa hiki kirusi kipya cha visiwani chenye vinasaba vingi na The elites! Hili linakolezwa na fununu zisizothibitishwa kwamba Taifa la Tz liko chini ya watoto wa familia moja.. 'Baba mmoja'... Ni TUHUMA!

Yaliyotokea ya mhimili mwingine mpaka kupelekea kujiuzulu, kauli ya mkuu wa kaya kuhusiana na 2025, uteuzi wa baraza jipya la mawaziri, na makatibu wakuu pamoja na wengine wote kuna tafsiri moja tuu... Uasi ujao na vita mpya kati ya sukuma gang, mtandao wa the elites , visiwani na bara na chawa wenye maslahi kwa kila upande..
Kila kundi liko chimbo likijiandaa kivyake... Ni mchezo wa kuwindana...uasi mkubwa waja...na ndio nafasi pekee ya walio nje ya mfumo ku take cover!
Swali fikirishi.
Hivi Makamu wa Rais wa SSH yuko wapi mbona hatumsikii hata kumwona kwenye dhifa. Ako masomoni au?
 
mnapenda kutafuta sababu ya kumkosoa mwendazake kila sehemu inapotakiwa kusifia hata kama nafsi zenu zinakiri alifanya jambo la maana.

embj nikuulize,jamaa katika baraza lake hawa erites walikuwepo kwa sababu zipi kama hakuwa na mpango nao!!!

yeye hakutaka mazoea ya kix3nge kama ya sasa mtu kujiona chama ni mali yake,mpaka kufikia kujimilikisha mali za chama.
 
Waziri kutishiwa bastola hadharani na baadae waziri huyo kufurumushwa sio kosa.
Hawa watu hawajui magu aliharibu mifumo kwa upande flan japo alikula mfupa uliowashinda wengine.. Kuna wkt magu aliharibu mtake msitake.

Kwa mfano, kujitenga na magharib ni kosa.

Kutengeneza makundi ni kosa gang hizi ni upuuzi.

Kutoshinikiza katiba na kuilinda yye aliikiuka kuivunja

Kutengeneza wahuni..wakina sabay na makonda...

Kuua upinzani ni kosa kubwa sana
wa
 
Back
Top Bottom