Uangalizi wangu [my observation] kuhusu urais wa Rais Magufuli

Nyani Ngabu Kilicho wazi Ni kuwa wapingaji wa Magufuli wengi wait Ni manazi wa chadema/ukawa hasa bavicha na ambao wengi ndiyo wanachama wa humu. Tazama tu hata topics zao Na pia wao ndio waanzishaji Na wachangiaji
 
Mkuu ulichokizungumza ndo uhalisia.
Ndo maana mkuu hua anawapotezea tu wateme nyongo zao zisije waumiza, kiukweli anaechukulia jukwaa Kama kipimo cha kukubalika au kutokubalika kwa Magufuli imekula kwake.
Jamaa asilimia kubwa ya watanzania wanamkubali ile mbaya ,research imefanyika na inaendelea kufanyika nchi nzima.
Wewe pamoja na Nyani Ngabu kama kweli Maghufuli anakubalika kwa kiasi hicho !!!
Uoga wa tume huru ya uchaguzi wa nini ?!
Uoga wa katiba mpya ya nini ?!
Kwanini awadhibiti wapinzani wake ?! Kwanini atumie dola dhidi ya wapinzani wake ?!

Haya ni maoni yenu Lumumba mtu hawezi kupinga. Lakini reality si hivyo.
 
Nchi hii kwa sasa hakuna upinzani kuna genge la wahuni,lazima wadhibitiwe, upinzani ulikwisha 2015, mlipokula matapishi yenu
 
Watu wa JF ndio hao hao wa mitaani, tofauti ni kuwa humu JF wanahakikishiwa usalama wao ndio maana wanaongea hata ya moyo (naamini hakuna anayewalipa), uraiani watu wanahofia maslahi na familia zao!

JF humu ni siri na 2020 kura zitakuwa za siri, tatizo ni namna uchaguzi wenyewe unavyoshughulikiwa!

Siamini kwenye mtazamo wa mleta mada!
 
Watu wa JF ni asilimia ngapi wa wapiga kura?
 
inategemea unamkubali kwa kulinganisha vitu gani, kwa kweli kuna mambo mengi anafanya mazuri japo anaweza asiwe anatumia njia ambayo tungetaka au kupenda wengi wetu lakini matokeo yake yanakuwa na faida zingine za muda mrefu na nyingine za muda mfupi.

Tatizo ni hapo kwenye mambo machache anayofanya vibaya au watu wake wanapotaka kumfurahisha na wengi kufuikiri ni maagizo yake ndio utata unapoanza.

JF ni ya watu wanaojitambua uelewa wao na upeo wa kuchambua mambo kidogo upo juu kulinganisha na kundi kubwa lililopo mtaani. Haimaanishi humu napo wapo wanaofuata upepo au mkumbo, bila kutulia na kufikiria wao kama wao.

Kwamba ni mkali, dikteta na hana simile, tunamuonea tu kwa sababu hivyo ndivyo alivyo, kila nafasi aliyoishika au kuitumikia amechapa kazi katika mwendo huo huo, ni kosa kufikiria angebadilika kisa amekuwa rais.

Mwisho, kuhusu ushindi wa 2020 siwezi kuongea sana, hii ni kwasababu kuna tofauti kubwa sana kati ya kushinda kwa wingi wa kura na kutangazwa mshindi na tume ya uchaguzi.

Na mimi haya ni maoni yangu binafsi
 
mimi naamini kabisa kuwa 2020 Rais Magufuli atashinda ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu. Itakuwa kinyume na ilivyokuwa kwa Kikwete....alishinda kwa kishindo kwenye awamu yake ya kwanza na kwenye awamu ya pili akapata ushindi mdogo sana kulinganisha na ule wa awali.
Naunga mkono hoja, 2020 sio Magufuli tuu ndiye atashinda kwa kishindo, bali CCM itarudisha karibu majimbo yote, isipokuwa Kigoma kwa Zitto.

Nchi inarejea kuwa nchi ya chama kimoja, na hili sisi wengine tuliisha lizungumza kitambo
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Paskali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom