Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Mimi naamini kwamba JF ni jukwaa lenye manufaa mengi sana. kuna mengi yanafanyika humu ambayo tunaweza tusiyaone. hata katika kumbi za Siasa, kuna elimu inatolewa, mijadala ni mikali na kuna wanaopinga na wanaounga mkono. hiyo hali ya wengi kupinga ilikuwa zamani. naona siku hizi pengine kuna mikakati ya kuweka maprofesheno wa kujibu hoja za watu wanaoipinga serikali. lakini kuna pia wale ambao misimamo yao ni independent. wanampenda tu JPM kwa sababu anashughulikia hoja za msingi ambazo zimewakera miaka nenda miaka rudi. Ila kusema kwamba JF haina connection na uhalisia, siyo relevant sana. wanaokwenda JF ni watu wa aina fulani, lakini ina a sample, inatoa representation ya watu hao. kundi la wale wakulima nao wana JF zao. hivyo unapochambua inabidi uzingatie hiloRais Magufuli keshamaliza miaka miwili kamili tokea ashike madaraka mwaka 2015.
Katika miaka hiyo miwili amekuwa akipingwa sana, akikosolewa vikali, na kudhihakiwa kwa kila namna hususan humu JamiiForums.
Kama ulimwengu ungekuwa ni huu huu wa JF basi mtu ungeweza kudhani kuwa wanaomuunga mkono Rais Magufuli ni idadi ndogo sana ya watu.
Lakini ukweli wa mambo, kwa mtazamo wangu, ni tofauti kabisa na taswira ijengwayo humu JF dhidi yake.
Huku uraiani Rais Magufuli anakubalika sana, hususan na watu wa kawaida wenye maisha ya chini na kati.
Ndiyo, wanaompinga wapo. Hawawezi kabisa kukosekana. Ila mtu ukiitumia JF kuwa ndo kipimo cha kukubalika au kutokukubalika kwake, hakika itakula kwako.
Kwa mfano, naamini kabisa ikiwekwa kura ya maoni humu JF kuhusu ‘approval’ au ‘disapproval’ ya urais wa Magufuli, atashindwa vibaya sana. Walio wengi wata ‘disapprove’.
Jambo hilo linanizidishia imani yangu kuwa kuna ‘disconnect’ kubwa tu kati ya uhalisia wa JF na uhalisia wa uraiani na mashinani.
Kwa mtaji huo, mimi naamini kabisa kuwa 2020 Rais Magufuli atashinda ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu. Itakuwa kinyume na ilivyokuwa kwa Kikwete....alishinda kwa kishindo kwenye awamu yake ya kwanza na kwenye awamu ya pili akapata ushindi mdogo sana kulinganisha na ule wa awali.
Lakini pia there is a catch. JPM anazo ajenda zake anazozipitisha humo humo pamoja na mambo mengine. na hili linajadiliwa hata mitaani, japo kwa tahadhari kubwa. kuna wengi wanaumia kwa sera zake kiuchumi, kuna wanaoumia kwa kubomolewa. ni kweli JPM ni mjanja sana kwa kucheza na hisia za watanzania, kiasi kwamba wale wa kawaida walio wengi watamuona ni mtu mzuri sana. kitendo cha kuwaumiza matajiri kinampa sifa sana kwa walala hoi, ambao wanaasume kwamba ule utajiri utatiririka kwao. kwamba akitumbuliwa fulani, zile hela alizokuwa anafuja na kufisidi, zitawashukia wananchi. tatizo linakuja pale hao wanaosubiri mvua ya fedha ije, isipokuja ndio yale ya kikwete ya leo kupata 85% na baada ya miaka mitano kuambulia 61% au chini zaidi ya hapo.
kama unayosema ni kweli, basi tungeona kwenye zile chaguzi za marudio, ambao wapinzani walisusia. kama kungekuwa na kale kafreedom angalau ka enzi za Kikwete tu, basi tungepata picha halisi ya maoni ya watanzania vs uchambuzi wako. lakini kwa kuwa kulikuwa na matumizi makubwa ya vyombo vya dola, hiyo pia inaonesha kwamba JPM naye hana uhakika kama anapendwa mtaani, na hayuko tayari kujiweka kwenye mizani. ukiangalia anayofanya kama kufunga bunge live, kuzuia wapinzani wasifanye siasa wakati CCM wanafanya siasa, ni namna kuonesha kwamba wanatambua jinsi CCM ilivyokuwa unpopular na wanataka wapinzani warudi nyuma ili wao wasonge mbele, angalau kwa idadi ya watu, hata kama ni kwa kuwanunua.