Uangalizi wangu [my observation] kuhusu urais wa Rais Magufuli

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,012
112,672
Rais Magufuli keshamaliza miaka miwili kamili tokea ashike madaraka mwaka 2015.

Katika miaka hiyo miwili amekuwa akipingwa sana, akikosolewa vikali, na kudhihakiwa kwa kila namna hususan humu JamiiForums.

Kama ulimwengu ungekuwa ni huu huu wa JF basi mtu ungeweza kudhani kuwa wanaomuunga mkono Rais Magufuli ni idadi ndogo sana ya watu.

Lakini ukweli wa mambo, kwa mtazamo wangu, ni tofauti kabisa na taswira ijengwayo humu JF dhidi yake.

Huku uraiani Rais Magufuli anakubalika sana, hususan na watu wa kawaida wenye maisha ya chini na kati.

Ndiyo, wanaompinga wapo. Hawawezi kabisa kukosekana. Ila mtu ukiitumia JF kuwa ndo kipimo cha kukubalika au kutokukubalika kwake, hakika itakula kwako.

Kwa mfano, naamini kabisa ikiwekwa kura ya maoni humu JF kuhusu ‘approval’ au ‘disapproval’ ya urais wa Magufuli, atashindwa vibaya sana. Walio wengi wata ‘disapprove’.

Jambo hilo linanizidishia imani yangu kuwa kuna ‘disconnect’ kubwa tu kati ya uhalisia wa JF na uhalisia wa uraiani na mashinani.

Kwa mtaji huo, mimi naamini kabisa kuwa 2020 Rais Magufuli atashinda ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu. Itakuwa kinyume na ilivyokuwa kwa Kikwete....alishinda kwa kishindo kwenye awamu yake ya kwanza na kwenye awamu ya pili akapata ushindi mdogo sana kulinganisha na ule wa awali.
 
Usemayo yana ukweli kiasi chake tatizo watu wengi wanao muunga mkono magufuri ni mbumbu na wasio elewa hii nchi kwa sasa na wananchi wake wanapitia magumu kiasi gani kuanzia uchumi, siasa, elimu, afya na mengineyo,
ndio maana inapaswa watu wawe na elimu ya kutosha wafumbuke macho.
 
usemayo yana ukweli kiasi chake tatizo watu wengi wanao muunga mkono magufuri ni mbumbu na wasio elewa hii nchi kwa sasa na wananchi wake wanapitia magumu kiasi gani kuanzia uchumi, siasa, elimu, afya na mengineyo,
ndio maana inapaswa watu wawe na elimu ya kutosha wafumbuke macho.

Elitism at its best!
 
Mkuu ulichokizungumza ndo uhalisia.
Ndo maana mkuu hua anawapotezea tu wateme nyongo zao zisije waumiza, kiukweli anaechukulia jukwaa Kama kipimo cha kukubalika au kutokubalika kwa Magufuli imekula kwake.

Jamaa asilimia kubwa ya watanzania wanamkubali ile mbaya ,research imefanyika na inaendelea kufanyika nchi nzima.
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom