Rahma Nyusi
Member
- Jun 3, 2015
- 73
- 9
Habarini wana JF,
Nataka niombe kazi ya kuandikisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye daftari la wapiga kura kwa mfumo wa BVR lakini sijui wapi nipeleke Cv yangu,na pia sijajua kama maombi yamesha anza kupokelewa au bado,kama bado wataanza kupokea maombi lini,na yanapelekwa wapi?Kwani zoezi la uandikishaji wa BVR kwa mkoa wa Dar es salaam litaanza tarehe 4 July hadi tarehe 16 July kama ratiba ya NEC inavyosema.
Kwa wale wa mikoa ambayo wamesha andikishwa walipeleka maombi yao wapi mpaka wakapata kazi hiyo ya kuandikisha watu?
MSAADA WENU PLEASE!

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
MANISPAA YA KINONDONI
TANGAZO
NAFASI ZA KAZI KWA BVR KITS OPERATORS MWANDISHI MSAIDIZI KWENYE UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Afisa Mwandikishaji wa Manispaa ya Kinondoni anawatangazia wote wenye sifa kujitokeza kuomba nafasi ya kazi kuwa BVR OPERATORS MWANDISHI MSAIDIZI kwenye Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
A. Sifa za Mwombaji
a) Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea.
b) Ajue kusoma na Kuandika bila Matatizo.
c) Awe Mkazi wa Kata anayoombea.
d) Awe raia wa Tanzania.
e) Awe anajua ujuzi wa kumpyuta angalau kiwango cha cheti
B. Namna ya Kuomba
a) Barua iliyoandikwa kwa Mkono ikiambatana na Photocopy ya cheti/vyeti.
d) Mwombaji ataje Kata anayoishi ambayo anaombea kufanya Kazi hiyo.
e) Barua zote ziletwe Ofisi ya Masijala ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni iliyopo Magomeni. Maombi yatumwe kabla ya Ijumaa tarehe 19/06/2015 Saa 10.00 Jioni.
Barua zote zitumwe/zipelekwe kwa:-
Afisa Mwandikishaji,-
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ,
Box 31902, Dar es Salaam,
Eng. Mussa B. Natty
AFISA MWANDIKISHAJI
MANISPAA YA KINONDONI.
11/06/2010