Uandikishaji wa BVR kwa mkoa wa Dar es Salaam

Uandikishaji wa BVR kwa mkoa wa Dar es Salaam

Jamani mimi nimeomba kata ya makumbusho jimbo la kinondoni,cha kushangaza jina langu halipo kwa walioitwa kwenye usaili.Na nilivyo kwenda kwenye usaili jmosi kata nyingine kama ya hananasifu waliofanya usaili walikuwa wachache kuliko wanaohitajika wakati wa makumbusho walikua wengi mpaka wengine tumekosa nafasi.
Cha kushangaza kata nyingine kama ya tandale wale ambao majina yao hayakuwepo kwa wanaotakiwa kufanya usaili lakini wamekwenda na vyeti original waliruhusiwa kufanya usaili lakini wamakumbusho wenye vyeti original hatukufanya usaili tumeandikwa majina kwa wenye vyeti tukaambiwa watatuweka kwenye kata nyingine zenye upungufu wa watu.
SASA JE HAYO MAJINA YAKIBANDIKWA TUKAANGALIE KWENYE OFISI ZA KATA YA MAKUMBUSHO AU TUKAANGALIE WAPI?KWA MANA WAMESEMA WATATUWEKA KWENYE KATA YEYOTE ILE YENYE UPUNGUFU WA WATU

MSAADA WENU KWA WENYE KUJUA TAFADHALI MANA TULIVYO WAULIZA WALIKUA BUSSY SANA HAWAKUTUPA MAJIBU YENYE KURIDHISHA WAMESEMA MUDA WAO WA KAZI UMEKWISHA KWA SIKU ILE

Hili zoezi pia kuna kuwa na upungufu wa waandikishaji wakati zoezi likiendelea. Mfano; kata fulani inahitaji kuongezewa mashine, hivyo wale ambao hawakupewa kazi mara ya kwanza hapa ndio huwa wanaitwa.
 
Kuahilishwa kwa zoezi la Uboreshaji kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani


Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuahirishwa kwa tarehe ya kuanza kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani hadi hapo itakapotangazwa tena.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Tume hiyo na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwana Julius B. Mallaba leo imesema hatua hiyo imetokana na kuchelewa kuwasili kwa vifaa vya kuandikishia Wapiga Kura (BVR), ambavyo viko katika Mikoa ambayo zoezi la Uboreshaji linaendelea.

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa Tume imelazimika kupeleka vifaa vilivyotarajiwa kutumika katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani , kwenda katika mikoa iliyoonyesha kuwa na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, hali inayotafsiriwa kuwa ni kuongezeka kwa mwamko miongoni mwa wananchi wanaojitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Awali Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya “Biometric Voters Registration” (BVR) kwa Mkoa wa Pwani ulipangwa kuanza tarehe 25/06/2015, Aidha kwa Mkoa wa Dar es salaam Uandikishaji ulitegemewa kuanza tarehe 04/07/2015.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatoa rai kwa wananchi wa Mikoa ya Pwani na Dar es salaam kuwa watulivu wakati ambapo ikisubiri vifaa vya Uandikishaji kutoka katika Mikoa itakayokuwa imekamilisha zoezi hilo.

Source: www.nec.go.tz
 
Jamani mimi wameniambia kata ya makumbusho watu wametosha kwa hiyo wataniweka kwenye kata yeyote ile kwa hiyo sijajua jina langu nikaangalie kata gani?
 
Jamani wapendwa wana JF zoezi la uandikishaji kwa mkoa wa Dar es salaam na Pwani linalotakiwa kufanyika tarehe 4 July lime hairishwa mpaka tume itakapo tangaza rasmi

Kwa ufafanuzi zaidi tembelea Mwanzo ::Tume ya Taifa ya Uchaguzi
:majani7:

:majani7::majani7::majani7:
 
Leo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa ratiba ya zoezi la uandikishaji kwa BVR kwa mikoa ya Pwani na Dar. Kwa Pwani zoezi litaanza 7/7/2015 na Dar ni 16/7/2015.

Source: ITV
 
Kwa wale walioomba Mabibo majina yametoka. Tarehe 13-14 ni seminar pale NIT.
 
Ni kweli hata manispaa yapo nimetoka pale mda si mrefu!
 
Jamani naomba anayejua kata ya kivukoni ilipo naomba anipatie direction jinsi ya kufika hapo
 
Back
Top Bottom