Uandikishaji wa BVR kwa mkoa wa Dar es Salaam

Rahma Nyusi

Member
Jun 3, 2015
73
9
Habarini wana JF,

Nataka niombe kazi ya kuandikisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye daftari la wapiga kura kwa mfumo wa BVR lakini sijui wapi nipeleke Cv yangu,na pia sijajua kama maombi yamesha anza kupokelewa au bado,kama bado wataanza kupokea maombi lini,na yanapelekwa wapi?Kwani zoezi la uandikishaji wa BVR kwa mkoa wa Dar es salaam litaanza tarehe 4 July hadi tarehe 16 July kama ratiba ya NEC inavyosema.

Kwa wale wa mikoa ambayo wamesha andikishwa walipeleka maombi yao wapi mpaka wakapata kazi hiyo ya kuandikisha watu?

MSAADA WENU PLEASE!
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
MANISPAA YA KINONDONI

TANGAZO

NAFASI ZA KAZI KWA BVR KITS OPERATORS MWANDISHI MSAIDIZI KWENYE UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Afisa Mwandikishaji wa Manispaa ya Kinondoni anawatangazia wote wenye sifa kujitokeza kuomba nafasi ya kazi kuwa BVR OPERATORS MWANDISHI MSAIDIZI kwenye Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

A. Sifa za Mwombaji
a) Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea.

b) Ajue kusoma na Kuandika bila Matatizo.

c) Awe Mkazi wa Kata anayoombea.

d) Awe raia wa Tanzania.

e) Awe anajua ujuzi wa kumpyuta angalau kiwango cha cheti

B. Namna ya Kuomba
a) Barua iliyoandikwa kwa Mkono ikiambatana na Photocopy ya cheti/vyeti.

d) Mwombaji ataje Kata anayoishi ambayo anaombea kufanya Kazi hiyo.

e) Barua zote ziletwe Ofisi ya Masijala ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni iliyopo Magomeni. Maombi yatumwe kabla ya Ijumaa tarehe 19/06/2015 Saa 10.00 Jioni.

Barua zote zitumwe/zipelekwe kwa:-

Afisa Mwandikishaji,-
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ,
Box 31902, Dar es Salaam,

Eng. Mussa B. Natty
AFISA MWANDIKISHAJI
MANISPAA YA KINONDONI.
11/06/2010


 
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
MANISPAA YA KINONDONI

TANGAZO

NAFASI ZA KAZI KWA BVR KITS OPERATORS MWANDISHI MSAIDIZI KWENYE UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Afisa Mwandikishaji wa Manispaa ya Kinondoni anawatangazia wote wenye sifa kujitokeza kuomba nafasi ya kazi kuwa BVR OPERATORS MWANDISHI MSAIDIZI kwenye Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

A. Sifa za Mwombaji
a) Awe na Elimu ya Sekondari na kuendelea.

b) Ajue kusoma na Kuandika bila Matatizo.

c) Awe Mkazi wa Kata anayoombea.

d) Awe raia wa Tanzania.

e) Awe anajua ujuzi wa kumpyuta angalau kiwango cha cheti

B. Namna ya Kuomba
a) Barua iliyoandikwa kwa Mkono ikiambatana na Photocopy ya cheti/vyeti.

d) Mwombaji ataje Kata anayoishi ambayo anaombea kufanya Kazi hiyo.

e) Barua zote ziletwe Ofisi ya Masijala ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni iliyopo Magomeni. Maombi yatumwe kabla ya Ijumaa tarehe 19/06/2015 Saa 10.00 Jioni.

Barua zote zitumwe/zipelekwe kwa:-

Afisa Mwandikishaji,-
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ,
Box 31902, Dar es Salaam,

Eng. Mussa B. Natty
AFISA MWANDIKISHAJI
MANISPAA YA KINONDONI.
11/06/2010
 
Naomba niulize..hiyo BVR kit operator na Mwandishi msaidizi ni post mbili tofauti au?.

Nijuzeni tafadhali
 
Mo'Anna hizo ni nafasi mbili tofauti. Unapoenda pale kituo cha kujiandikisha unakutana na mtu wa kujaza maelezo yako kwenye Form #1 . Huyu anaitwa Msaidizi. Baada ya maelezo yako kujazwa kwenye F1, inapelekwa kwenye BVR Kit ambapo BVR Operator anaingiza kwenye computer kile kilichojazwa kwenye F1.

Pia Operator atakupiga picha, kuchukua alama za vidole na mwishowe ata print kitambulisho chako.
 
Last edited by a moderator:
Ila kwa angalizo. Kama haupo vizuri kwenye Computer na matumizi yake, nashauri ni busara kutokwenda kuchukua kazi hii. Kwani unaweza kusababisha msululu mrefu wa watu kutokana na Speed yako ndogo.

Pia seminar ya BVR Operator haizidi siku tatu ambazo utatakiwa kutumia kifaa chenye components zisizopungua 72 zilizounganishwa ili kupata Kit moja. Hapa kuna printer, scanner, camera, signing pad, modem ya internet, GPS device, finger prints/marks reader n.k.

Nashauri kwa ufinyu wa muda wa zoezi la uandikishaji, ni bora wakachagua watu wenye uwezo ili kuleta ufanisi.

Kingine, hakuna anayemzidi mwenzake malipo katika vitengo vyote vya hizo Kit na uandikishaji kwa ujumla.
 

Attachments

  • 1434429968354.jpg
    1434429968354.jpg
    65.5 KB · Views: 1,172
Mimi jana ndo nimetoka kupeleka barua ya maombi kwa watu wa Manispaa ya Kinondoni.
wamepokea na nimekuta na vijana wengine wanapoleka.
mwisho kwa Kinondoni ni 19 mwezi huu… halafu hapo hapo kuna tangazo linasema Jumamosi ya tarehe 20 ni usaili kwa jimbo la Kinondoni, Jumatatu 22,ni usaili kwa jimbo la Kawe na Jimbo la Ubungo ni tarehe 23 Jumanne. Hupigiwi simu,yaani nimefafanuliwa pale pale kuwa kama umeomba we kariri siku ya usaili ndo uende pale kufanyiwa usaili.

Baada ya maelezo hayo nadhani nimekosea kwenye barua ya maombi… niliandika kuwa naomba nafasi ya kazi ya BVR Kit Operator,Mwandishi Msaidizi… nikijua ni kazi moja kumbe ni tofauti kwa mujibu wa wadau wa humu… hapo vipi si nishapigwa chenga jamani!
Aiseee…
 
Jamani mimi nimeshapeleka maombi Ya uandikishaji kinondoni na wamesema usaili utafanyika tarehe 20 mwezi huu sasa wana ndugu naombeni kuuliza kwa wale wamikoani ambao wameshafanya usaili kama huu huwa wana uliza maswali gani?

MSAADA WETU TAFADHALI!!!
 
sasa huyo jamaa n eng alafu n afisa mwandikishaji jamani, mmmmhh haya bhana tutafika tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom