uaminifu zero kabisa, ujanja ujanja huu hauna maana

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Mkandarasi 'aitapeli' Simba, kushitakiwa Send to a friend
Saturday, 31 December 2011 08:34
0digg

Sosthenes Nyoni
UONGOZI wa Simba umesema unakusudia kumshataki mkandarasi wa jengo la biashara la klabu hiyo (jina linahifadhiwa) kwa madai ya kukiuka makubaliano.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage aliyataja makubaliano yaliyofikiwa baina ya klabu hiyo na mkandarasi huyo kuwa ni ujenzi wa msingi wenye uwezo wa kubeba jengo la ghorofa nane.

Alisema kuwa kinyume na makubaliano hayo klabu yake kwa kuwatumia wataalamu wa kitendo cha uhandisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walibaini kuwa kuwa jengo hilo ambalo kwa sasa lina ghorofa tatu haliwezi kubeba ghorofa nyingine juu na endapo watalazimisha kunauwezekano wa kudondoka.

"Niseme wazi Simba inakusudia kumshItaki mkandarasi wa ujenzi wa jengo letu la biashara kutokana na kukiuka makubaliano.

"Nyaraka za makubaliano zipo na zinaonyesha alitakiwa ajenge msingi wenye uwezo wa kubeba ghorofa nane, lakini yeye ametudanganya," alisema Rage.

Aliongeza kuwa tayari ameshawasiliana na wanasheria wake kwa ajili ya kufungua kesi dhidi ya mkandarasi huyo.

"Nimeshawasiliana wanasheria wangu nafikiri mpaka kufikia wiki ijayo kesi dhidi ya mkandarasi huyu itakuwa imeshafunguliwa," alisema

Rage alisema kwa sasa wapo mbioni kubomoa jengo hilo na kujenga jingine litakalokuwa na ghorofa nane kwa lengo la kuongeza mapato ya klabu yake.

"Huu si wakati wa kutafuta sifa kwa kuifunga Yanga, Simba na Yanga zinafungana hata mimi sijazaliwa, wajibu wa kiongozi ni kubuni miradi, mambo ya timu kufungwa au kushinda ni suala linalowahusu wachezaji," alisema Rage.
 
Na walipokuwa wanaanza hiyo foundation mpaka wamefika ghorofa ya 3 kulikuwa hakuna usimamizi?
 
Hivi jengo lile lilijengwa mwaka gani? Huyo mkandarasi mpaka leo hajafirisika kweli!

sio lile la zamani pembeni yake kuna jipya lina gorofa moja
ambamo ndo ofice za simba zipo na chini maduka.
Rage nina wasiwasi na kauli yako au ndo unataka kumkomoa wambura!!!
 
Tatizo liko hapo, mkataba alipewa 'mshkaji'? Mbona anaongelea 'mwanasheria wangu' badala ya 'wetu'? Kisheria ni lazima kumchukua mkandarasi aliyesajiliwa na bodi ili asimamiwe na kuwajibishwa. Na anataka kumpeleka mahakamani mkandarasi wakati huo anataka kubomoa jengo! Wapi na wapi sasa, ataenda kutoa stori mahakamani ama? Ng'ombe wa maskini hazai, akizaa anazaa dume tena dume lenyewe linakuwa shoga! Kha!
Mkandarasi 'aitapeli' Simba, kushitakiwa Send to a friend
Saturday, 31 December 2011 08:34
0digg



"Nimeshawasiliana wanasheria wangu nafikiri mpaka kufikia wiki ijayo kesi dhidi ya mkandarasi huyu itakuwa imeshafunguliwa," alisema

Rage alisema kwa sasa wapo mbioni kubomoa jengo hilo na kujenga jingine litakalokuwa na ghorofa nane kwa lengo la kuongeza mapato ya klabu yake.

 
Back
Top Bottom