Uaminifu uliotukuka

Uaminifu uliotukuka

ha ha ha ha lakini ukiangalia hiyo picha vizuri huyo mwingine amemuamini mwenzake kwa 100%


Achana na picha, tulipokua shule taa ya bwalo la chakula iliungua. Ikabidi niitwe kuibadilisha, tulikosa ngazi ila palikua na meza haina mguu mmoja.
Kuna jamaa akajitolea atashikilia hapo pasipokua na mguu, kikawekwa kiti juu ya meza nikapanda, nikamaliza kazi vizuri, taa ilipowaka jamaa si akaachia meza kwa kujisahau. Hadi leo chembe moyo haijakaa sawa kutokana na lile tukio, nilianguka mbavu za kifuani ndio zikawa egemeo.....fulcrum
 
Achana na picha, tulipokua shule taa ya bwalo la chakula iliungua. Ikabidi niiwe kuibadilisha, tulikosa ngazi ila palikua na meza haina mguu mmoja.
Kuna jamaa akajitolea atashikilia hapo pasipokua na mguu, kikawekwa kiti juu ya meza nikapanda, nikamaliza kazi vizuri, taa ilipowaka jamaa si akaachia meza kwa kujisahau. Hadi leo chembe moyo haijakaa sawa kutokana na lile tukio, nilianguka mbazu za kifuani ndio zikawa egemeo.....
Pole sana mkuu ingawa stori yako inachekesha lakini pia inafundisha
 
Wote mnawaamini sana watu wengine kiasi cha kukabidhi maisha yenu kwao.

Kama umewahi kumeza dawa au kuchomwa sindano au kufanyiwa upasuaji ujue ulimuamini daktari kwa kumkabidhi maisha yako.

Kama angekosea dozi au aina ya dawa au upasuaji si angesababisha kifo chako?
 
Back
Top Bottom