Uaminifu ni chanzo cha mafanikio

Iam me empire

Member
Jul 20, 2021
5
3
Mfalme alipoona umri umeenda aliamua kutafuta mtu wa kumrithisha Ufalme wake.

Mfalme alikusanya vijana 10 na akawaambia atawapa mtihani yule atakae faulu ndiyo atakuwa mrithi wake.

Mfalme aliwapa vijana hao mbegu za mahindi na akawaambia kila mmoja aende nazo nyumbani akazioteshe, akawapa muda wa wiki 3 warudi na mbegu hizo zikiwa zimeota.

Katika nyumba moja kijana alishangaa kuona mbegu amezipanda na kumwagilia vizuri lakini hazikuota, alirudia tena hata hivyo hazikuota tena. Familia walihuzunika sana na marafiki wa kijana huyo walimshauri akanunue mbegu zingine ila wazazi wake wakakataa kwa kumuogopa Mungu.

Baada ya wiki 3 kufika vijana wote walirejea nyumbani kwa mfalme wakiwa na mbegu zikiwa zimeota vizuri na walijipanga mstari na mfalme akaanza kupita akikagua mbegu kwa kila kijana, vijana wote 9 walikuwa wameotesha mbegu zao vizuri ispokuwa kijana mmoja ambaye alikuwa amesimama mwisho kwa wasiwasi na uoga.

Mfalme apomfikia akamuuliza kwanini wewe haukufanikiwa kuotesha mbegu zangu?

Kijana, kwa unyonge akajibu: mfalme mimi nijaribu kuzipanda lakini hazikuota.

Mfalme akacheka na kusema wewe ndio unafaa kuwa mrithi wangu.

Mbegu zote nilizowapa zilikuwa zimechemsha na mbegu ikichemshwa huwa haioti.

Kwa hiyo wote walioziotesha ni wadanganyifu sasa hatupaswi kuwa na mfalme muongo, mfalme anatakiwa kuwa mkweli na mwaninifu.

Kijana alivishwa taji.

Tunaishi kwenye jamii na watu wenye mafanikio makubwa sana. Wengi wao wapata hayo mafanikio kwa njia zisizo halali.

Wangapi wanasomesha watoto wao kwenye shule za ghalama, wana majumba na magari yakifari waliyoyapata kwa njia za kishetani na kuna wangapi wana vyeo vya juu kwa vyeti feki.

Pongezi kwa wote waliotumia ghalama zao halali kujipatia mafanikio walionayo.

Tafadhali tuweni waamifu kwa Mungu wetu na tutafute riziki kwa njia harali vinginevyo tutaotesha mbegu zilizochemshwa.

Uaminifu Uaminifu uaminifu
 
Mkuu umejichanganya mno. Umesema uaminifu ndio chanzo cha mafanikio ila hapo hapo umekiri kuna watu wamefanikiwa kwa vyanzo ambavyo sio vya kiuaminifu.
 
Lengo ni uondokane na umaskini iwe kwa kamali kuuwa ushirikina na mengineyo umaskini haufai
 
Yaani mada umeileta mwenyewe na umeipinga mwenyewe

unasema umainifu huleta mafanikio halafu chini unasema waliofanikiwa wengi wamepata kwa njia haramu

hahahahah
 
Yaani mada umeileta mwenyewe na umeipinga mwenyewe

unasema umainifu huleta mafanikio halafu chini unasema waliofanikiwa wengi wamepata kwa njia haramu

hahahahah
Iyo inaonesha kuwa kuna watu watumia njia sahihi na wengine wanatumia njia isiyo sahihi kupata mafanikio
 
Halafu hawo watu waaminifu wanaishi wapi kwa sasa hivi, CCM mbona waliiba Uchaguzi na wako madarakani.?
 
Back
Top Bottom