Uaminifu kwenye ndoa

Uaminifu kwenye ndoa

Unazungumzia uwongo wa kiasi gani?

Maana kwa uzoefu wangu wa maisha sijawahi kukutana na mtu ambaye hajawahi kudanganya.

Au wapo watu wasiodanganya?
Mfano kuna dada Mtanzania alikwenda ughaibuni, alijilipua Kinyarwanda, baada ya muda alipata boyfriend mzungu. Kurahisisha mambo yule dada alimwambia mzungu yeye Mnyarwanda. Basi mzungu alikutana na Wanyarwanda wakaanza urafiki akijua mashemeji. Wanyarwanda wakamwalika kwao, akaenda na girlfriend wake, wamefika kule mdada Kinyarwanda hajui, ilibidi awaambie yeye hajatoka Rwanda ila ametoka Tanzania. Wamefika nyumbani mzungu anasema kama ulinidanganya mimi na wewe mwisho wetu ni hapa. Sasa huu si ni uongo jamani.
 
Hapo umeiimarisha tu hoja yangu kwamba binadamu kiasili tu waongo.

Naamini hakuna binadamu asiye muongo.

Kama yupo nitajie.
 
Kwa wale walioko kwenye ndoa, neno uaminifu ni silaha kubwa kwenye mahusiano. Uaminifu ninao uongelea hapa leo maana yake ni 100% kwa mwenza wako. Hii inamaanda kuwa wazi na kipato unachopata na jinsi ya kutumia.

Inashauriwa wanandoa kuwa na account tatu yaani kila mtu anakuwa na account ambayo mshahara au pesa za biashara inaingia kila mwezi. Baada ya hapo kunakuwa na joint account ambayo mnakubaliana kuwa kila mwezi wote wawili ni kiasia gani kitaingia. Hii inarahisisha mipango mikubwa ya maendeleo huko mbele, kama kununua kiwanja au gharama za elimu kwa watoto.

Kwenye hii joint account, inashauriwa kuwe na discipline ya kuchukua pesa. Kama uhusiano wenu unabaraka zote na mnaishi kwa amani, hata unapoona mume ametoa laki tano juzi kutoka kweny joint account, utafahamu ni za nini au alishakutaarifu. Sasa pale laki tano inapotoka kumsaidia mama wa mchepuko ndio hatari.
Kila sehemu unasema 'inashauriwa'. Nani anayeshauri mambo ya aina hiyo?

Unachoandika hapa ni 100% theory ukimaanisha partners wote wako sawa, family status kila pande ziko sawa, mahitaji ya baba na mama pamoja na tabia zao ziko sawa. Tabia zetu zinarekebishika kutegemea partners tunaoishi nao. mume akiwa mlevi au akigeuka na kuwa mlevi baadaye, utamshawishije aweke pesa yake pamoja na mke.
 
Uaminifu unaweza kuwa mdogo pale compactable ness inapoondoka, kama vile kuanza dharau kwa familia ya mwenzako. Sasa akiwa na shida za kwao anaona azimalize mwenyewe na wakati problem shared is halved.
 
Kila sehemu unasema 'inashauriwa'. Nani anayeshauri mambo ya aina hiyo?

Unachoandika hapa ni 100% theory ukimaanisha partners wote wako sawa, family status kila pande ziko sawa, mahitaji ya baba na mama pamoja na tabia zao ziko sawa. Tabia zetu zinarekebishika kutegemea partners tunaoishi nao. mume akiwa mlevi au akigeuka na kuwa mlevi baadaye, utamshawishije aweke pesa yake pamoja na mke.
I know ni theory lakini it can be applicable, kwa msaada wa Mungu mkuu. Kupata mke mlevi ambae anasahau kweka akiba ni shetani na anahitaji kukemea.
 
Na maranyingi wanaoanza kutoa pesa kwenye joint account ni wanaume, na ukiuliza unaambiwa juzi si nilijaza petrol full tank kwenye gari yako? Lakini tulipofungua ile joint account malengo hayakuwa petrol. Tena paho ameshatoa laki tano anakupoza wewe na laki moja.
 
Inakuwaje kwa wale wamama wa nyumbani ambao hawaingizi kipato? hiyo joint account itafanyaje kazi?

ni hayo tu asante.
 
Wakati mwingine uaminifu wa pungufu ya %100 ndio kitu kinachofanya mambo yaende, vinginevyo pasingekalika.
 
Inakuwaje kwa wale wamama wa nyumbani ambao hawaingizi kipato? hiyo joint account itafanyaje kazi?

ni hayo tu asante.
Unaweza kumpa awe anaweka yeye bank kila mwisho wa mwezi na yeye awe anashirikishwa kwenye mipango ya nyumba, pia ni vizuri awe na uzoefu ili hata ukiwa na shida au ukiwa umesafiri anaweza yeye kuchukua pesa kwa niaba yako.
 
Ok good.
Nadharia yako ya uaminifu imeegemea upande wote wa mume na mke wana kazi nzuri na wanauwezo wa kuweka akiba kwa kushirikiana wote wawili.

1. Ikiwa mume ndo anafanya kazi nzuri na ndo anaihudumia familia na mke hana/hajapata kazi?.

2. Ikiwa mke anafanya kazi yenye kipato kikubwa na mume kipato kidogo sana ukilinganisha na mke yan anabangaiza kwenye shughuli zake ili mradi familia hailali njaa.
(Usiombe mke akuzidi kipato au elimu!! uwe na uvumilivu100%)
..........................................

Kumwamini mwanamke100% ni sawa na kumuamini rafiki yako ambae ni polisi kumuweka wazi na kumueleza kila kitu chako coz siku akighadhibika/ akichukia au akikasirika(au akitaka kupiga bingo) utajuta na kutafuta sura pakuiweka usipaone (observe it).

Dunia imebadilika, Kumuamini mke 100% na kumuweka wazi ni sawa na kumpa mbinu na kuusoma mchezo na akitaka kufanya lake anapita humo humo kwenye 100%
 
Watu kama wewe ndio likitokea la kutokea mali zinapotea kwasababu mke wako hajui kila kitu. Kwa kifupi ni mke anapaswa kuwa best friend wako, sasa kama unaweza kumweleza mke wako matatatizo yako ya kutokupata choo kwanini asijue bank una pesa ngapi?
 
Pesa siyo kipimo cha uaminifu.

Kuna watu wana hela na wanatoka nje ya ndoa. Mama akija juu kwanini unafanya hivyo anakuuliza ni kitu gani unakosa.

Joint account ni rahisi kucheck debit na credit lakini ngono mtu akioga akakutizama machoni utajulia wapi.
 
Back
Top Bottom