Uaminifu kwenye ndoa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,368
Kwa wale walioko kwenye ndoa, neno uaminifu ni silaha kubwa kwenye mahusiano. Uaminifu ninao uongelea hapa leo maana yake ni 100% kwa mwenza wako. Hii ina maana kuwa wazi na kipato unachopata na jinsi ya kutumia.

Inashauriwa wanandoa kuwa na account tatu yaani kila mtu anakuwa na account ambayo mshahara au pesa za biashara inaingia kila mwezi. Baada ya hapo kunakuwa na joint account ambayo mnakubaliana kuwa kila mwezi wote wawili ni kiasi gani kitaingia. Hii inarahisisha mipango mikubwa ya maendeleo huko mbele, kama kununua kiwanja au gharama za elimu kwa watoto.

Kwenye hii joint account, inashauriwa kuwe na discipline ya kuchukua pesa. Kama uhusiano wenu una baraka zote na mnaishi kwa amani, hata unapoona mume ametoa laki tano juzi kutoka kweny joint account, utafahamu ni za nini au alishakutaarifu. Sasa pale laki tano inapotoka kumsaidia mama wa mchepuko ndio hatari.
 
Inamaana ukitoa laki tano kwenye joint account utafanya jitihada ya kuzirudisha pasi mwenza wako kujua au utakauka?

Hapo kwa kweli sijui.

Nachoweza kusema ni kwamba nitakabiliana na hiyo hali pale itaponitokea.

Kuanza kuelezea kwa nadharia tete nitafanya nini ni sawa na kupiga ngumi hewani.
 
uaminifu ni mpana mno na ni moja ya masomo ya utakatifu kwa wale wakristo...
Na upana wa uaminifu ni kuwa, unapokosekana inapelekea maendeleo kwenye ndoa kuchelewa. Usiwalaumu wanawake wanajenga nyumba bila kwaambia waume zao, wanakua wameshasoma alama za nyakati.
 
Na upana wa uaminifu ni kuwa, unapokosekana inapelekea maendeleo kwenye ndoa kuchelewa. Usiwalaumu wanawake wanajenga nyumba bila kwaambia waume zao, wanakua wameshasoma alama za nyakati.

Na wanaume wanaofanya mambo yao bila kuwaambia wanawake zao nao wanakuwa washazisoma alama za nyakati?
 
Na wanaume wanaofanya mambo yao bila kuwaambia wanawake zao nao wanakuwa washazisoma alama za nyakati?
Ni kitu rahisi sana kuweka uaminifu, bila uaminifu hata leo nimetoka seminar cheque yangu ninatafuta mahali pa kuiweka, mwisho ndio unatafuta mchepuko wa kuueleza issue zako.
 
Ni kitu rahisi sana kuweka uaminifu, bila uaminifu hata leo nimetoka seminar cheque yangu ninatafuta mahali pa kuiweka, mwisho ndio unatafuta mchepuko wa kuueleza issue zako.

Uaminifu kamili ni mgumu aisee.

Binafsi naamini binadamu kiasili huwa tupo waongo waongo kulingana na mazingira.

Hivyo, kwa mtaji huo, sidhani kabisa kama uaminifu wa asilimia 100 upo.

Na hiyo ni kwa sababu uaminifu ni siri ya mtu moyoni.
 
Shemeji katoa laki tano nini bila kukuambia?
Kukiwa na uaminifu hata ukikuta laki tano imeondoka utajua labda anataka kunifanyia surprise, au alikua na shida atanieleza. Lakini kama umeanza kuhisi jamaa akipokea simu anatoka nje, mkiwa ndani simu iko kwenye lock. Mhh.
 
Uaminifu kamili ni mgumu aisee.

Binafsi naamini binadamu kiasili huwa tupo waongo waongo kulingana na mazingira.

Hivyo, kwa mtaji huo, sidhani kabisa kama uaminifu wa asilimia 100 upo.

Na hiyo ni kwa sababu uaminifu ni siri ya mtu moyoni.
Ninadhani hali inabadilika mnapokuwa pamoja, au wengine wanaficha makucha wakati wa uchumba. Kama humwamini kwanini ulikubali kuolewa au kwanini ulimuoa?
 
Mwanaume inabidi utengeneze enough capital ili bibiye aweze kutumia awezavyo sio akitoa laki2 tu unauliza maswali ka kituo cha polisi. Uanaume ni majukumu na majukumu ndiyo hayo
 
Asante sana, tena walalamishi wengi ni wale wanaingiza laki mwezi huu, mwezi ujao anakwambia binamu yangu ameomba nimuongezee ada ya watoto, ok nimekuelewa mume wangu, wewe ukitoa laki tano anakua mbogo.Bufa
 
Ninadhani hali inabadilika mnapokuwa pamoja, au wengine wanaficha makucha wakati wa uchumba. Kama humwamini kwanini ulikubali kuolewa au kwanini ulimuoa?

Ni rahisi sana kuuliza hilo swali la "Kama humwamini kwanini ulikubali kuolewa au kwanini ulimuoa?"

Lakini watu wengi huwa tunaishi kwa matumaini hususan ikija kwenye mambo tusiyoyajua.

Hayo matumaini ndo sababu kuu ya kwa nini watu huoana hata kama imani iliyopo baina yao si 100%
 
Kuna tabia ambazo huwezi kuzificha kwa muda mrefu kama kudanganya, mtu akiwa mwongo mwongo na ukimjua ni vyema kuanza tahadhari, kwasababu huwezi kujua anaficha mangapi. Pamoja na kuwa transparent sana nako kuna madhara yake.
 
Unazungumzia uwongo wa kiasi gani?

Maana kwa uzoefu wangu wa maisha sijawahi kukutana na mtu ambaye hajawahi kudanganya.

Au wapo watu wasiodanganya?
 
Kwa wale walioko kwenye ndoa, neno uaminifu ni silaha kubwa kwenye mahusiano. Uaminifu ninao uongelea hapa leo maana yake ni 100% kwa mwenza wako. Hii inamaanda kuwa wazi na kipato unachopata na jinsi ya kutumia.

Inashauriwa wanandoa kuwa na account tatu yaani kila mtu anakuwa na account ambayo mshahara au pesa za biashara inaingia kila mwezi. Baada ya hapo kunakuwa na joint account ambayo mnakubaliana kuwa kila mwezi wote wawili ni kiasia gani kitaingia. Hii inarahisisha mipango mikubwa ya maendeleo huko mbele, kama kununua kiwanja au gharama za elimu kwa watoto.

Kwenye hii joint account, inashauriwa kuwe na discipline ya kuchukua pesa. Kama uhusiano wenu unabaraka zote na mnaishi kwa amani, hata unapoona mume ametoa laki tano juzi kutoka kweny joint account, utafahamu ni za nini au alishakutaarifu. Sasa pale laki tano inapotoka kumsaidia mama wa mchepuko ndio hatari.
(joint Account!!) Good idea mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom